Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Uchaguzi ujao mtafanya peke yenu mshinde kwa 200% maana wapinzani waliposhiriki mlipata 100%.....
CCM sio kama haitaki upinzani No!,ni wapinzani ambao kwa sasa wanaitwa "wapingaji"ndio hawaitaki CCM, badala yakuja na sera mbadala na kuwauzia wananchi wao kila wakisimama jukwaani wao ajenda yao ni "tutaitoa CCM madarakani"na vijikashfa vya hapa napale.
 
Ushauri au maoni haya ya Mr.Mkiki ni dalili za WAZI kwamba sasa watu wamechoka.CCM sikio la kufa halisikii dawa.
 
Mkuu rais ni binadamu kama mimi na wewe, lakini anaapa. Sio kila mtu anayeapa.

Hizi ni taratibu za kiuongozi za dunia nzima, na hazijaanza leo wala jana, kabla Yesu hajazaliwa zilikuwepo na akaziacha. Mimi na wewe tutaziacha pia. Huwezi kuzikwepa. Hakuna mtu anayemuabudu binadamu mwenzake. ni suala la maadili ya kimaisha, ambayo tutakufa na tutayaacha yakiendelea kuwaongoza watakaokuwepo nyakati hizo.

Ni suala la heshima tu, na sio zaidi ya hapo.

Ni kweli ila ww umevuka kiwango cha heshima umehamia kwenye kujipendekeza na kuogopa hata kukosoa udhaifu wake kisa ni rais, na hata wale wanaothubutu kumkosoa, unawatafsiri kama wakosa nidhamu huki ukijificha kwenye rais kutukanwa as if ni jambo lilifanyika au linafanyika 24/7-365 a year.

Hii tabia ya kufumbia macho uovu eti kisa ni cheo cha rais inazigharimu tawala nyingi hasa nchi za kiafrika. Ndio maana unamtaja rais kwamba ni mtu mkubwa na sifa ya ukubwa ni hasi kwamba anaweza kukupoteza! Seriously hii ni sifa ya maana ya kutuonyesha uwezo wa rais? Kujipendekeza na kujitia upofu kwenye maovu sio jambo jema.
 
CCM sio kama haitaki upinzani No!,ni wapinzani ambao kwa sasa wanaitwa "wapingaji"ndio hawaitaki CCM, badala yakuja na sera mbadala na kuwauzia wananchi wao kila wakisimama jukwaani wao ajenda yao ni "tutaitoa CCM madarakani"na vijikashfa vya hapa napale.
Ndo siasa ulitaka wasemeje hatutaki kuitoa ccm madarakani!!!?.....Ummalizapo adui ndio mwanzo wa adui mpya.....jipangeni kutafuta adui mpya miongoni mwenu...maana Sina hakika Kama Upinzani watakuja simamisha mgombea Tena....kwa katiba hii nasema Sina hakika.....
 
Ndo siasa ulitaka wasemeje hatutaki kuitoa ccm madarakani!!!?.....Ummalizapo adui ndio mwanzo wa adui mpya.....jipangeni kutafuta adui mpya miongoni mwenu...maana Sina hakika Kama Upinzani watakuja simamisha mgombea Tena....kwa katiba hii nasema Sina hakika.....
Point yangu hujaipata ndio maana ccm iwatawala milele.
 
CCM sio kama haitaki upinzani No!,ni wapinzani ambao kwa sasa wanaitwa "wapingaji"ndio hawaitaki CCM, badala yakuja na sera mbadala na kuwauzia wananchi wao kila wakisimama jukwaani wao ajenda yao ni "tutaitoa CCM madarakani"na vijikashfa vya hapa napale.

Usitake kujitoa ufahamu kwa kubeba utetezi dhaifu. Usidhani watu wanaoshabikia upinzani ni wajinga kwamba wanafurahia tu ccm kutolewa madarakani. Kwanza lengo la chama chochote cha siasa ni kukamata dola. Na kwenye kukamata dola lazima watumie sera na mbinu mbalimbali na hilo sio kosa kwani ndio kanuni ya mchezo. Hapa unataka kuonyesha wapinzani wao wakipanda jukwaaani hawaongei chochote cha kuhusu wananchi bali ni kuitoa ccm tu madarakani.

Bunge lipo na hansard zipo, huko huwa wanatoa bajet zao kivuli na michango yao iliyovutia wananchi. Ccm ndio tunaishangaa haitaki kuachia madaraka kwa kisingizio cha kuleta maendeleo as if ni pesa toka mfuko wa ccm ndio zinazoleta maendeleo. Matokeo yake ndio hapo kura wanazidiwa wanatumia dola kulazimisha wao ndio waongoze. Sasa hivi watu hawataki kupiga kura kwakuwa haziheshimiwi, na sababu ni ccm kujitangaza bila ridhaa yao.
 
CCM sio kama haitaki upinzani No!,ni wapinzani ambao kwa sasa wanaitwa "wapingaji"ndio hawaitaki CCM, badala yakuja na sera mbadala na kuwauzia wananchi wao kila wakisimama jukwaani wao ajenda yao ni "tutaitoa CCM madarakani"na vijikashfa vya hapa napale.
Kwaiyo

unataka wafanye Fujo na kuhatarisha amani ya nchi? Tutawadeal
Amani ndiyo kichaka chenu cha kufanyia maovu.
 
Point yangu hujaipata ndio maana ccm iwatawala milele.

Kutawala milele sio shida, unatawalaje hapo ndio issue. Hats rais Kamuzu Banda wa Malawi alijitangaza atakuwa rais wa milele wa Malawi aliweza? Mugabe naye aliamini atafia madarakani mpigie simu leo yuko ikulu ipi? Huu mtindo wa ccm kulazimisha kukaa madarakani, leo hii chini ya awamu ya tano nchi yetu kwenye jumuiya ya kimataifa tuko kundi moja na nchi kama Burundi, Rwanda, Uganda na Congo. Hii ni aibu kwa kipindi cha miaka chini ya mitatu nchi kuingia humo. Hapo kama hakuna tatizo kuna nini?
 
Usitake kujitoa ufahamu kwa kubeba utetezi dhaifu. Usidhani watu wanaoshabikia upinzani ni wajinga kwamba wanafurahia tu ccm kutolewa madarakani. Kwanza lengo la chama chochote cha siasa ni kukamata dola. Na kwenye kukamata dola lazima watumie sera na mbinu mbalimbali na hilo sio kosa kwani ndio kanuni ya mchezo. Hapa unataka kuonyesha wapinzani wao wakipanda jukwaaani hawaongei chochote cha kuhusu wananchi bali ni kuitoa ccm tu madarakani.
Sijawahi hata kuona japo kipeperushi tu cha ilani ya chama cha upinzani.
 
Sio wewe tu hata Jiwe anaamini hivyo....atatawala milele.
Ndivyo CCM wanavyoamini.Ndiyo maana mara wanapo ona wanatikiswa kisingizio chao ili wabaki madaraki ni "amani ya nchi".Lakini wapinzani kuuawa,kuchomwa visu,mapanga ,kupotezwa na kila aina ya mateso kwao haina maana yoyote.Wapinzani HAWASTAHILI AMANI YA NCHI WANAOIHUBIRI.

Halafu "Ati njooni kwangu ninyi nyote mnausumbuka na kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha".Huku ni kunajisi maandika Matakatifu.
Labda kama wanamwamini mungu wao na siyo Mungu MFALME WA AMANI anayeabudiwa na KUTUKUZWA NA WATU WEMA NA WATENDA HAKI.
 
CCM sio kama haitaki upinzani No!,ni wapinzani ambao kwa sasa wanaitwa "wapingaji"ndio hawaitaki CCM

Jeshi la Polisi mnalo ni kitu gani kime washinda kuwapeleka Mahakamani na hatimae kuwafunga hao mnao waita kuwa ni Wapigaji ?

, badala yakuja na sera mbadala na kuwauzia wananchi wao kila wakisimama jukwaani wao ajenda yao ni "tutaitoa CCM madarakani"na vijikashfa vya hapa napale.

Dhumuni Kuu la Chama chochote ni kushika Dola ili kitimize yale kinacho Ahidi ktk kampeni na kuongoza Nchi.Nikukumbushe tu Malaika Mkuu amesha sema ,nna nukuu Sehemu ya alicho wahi kukisema " CCM ita Tawala Milele".Na huyu tumuweke Kundi gani ?
 
Rais wa CCM na CCM yake, na polisi wake na wateule wake na vyombo vingine vya kisheria na dola, hawaamini katika demokrasia. Wao wakisikia Chadema wanachukulia kama ni waasi au magaidi. Kwa hiyo wanapambana kwa njia zote zisizo za kidemokrasia, bila kujali dhuluma wanayofanya kwa wananchi wanaotumia muda wao mwingi kwenye kwenye mikutano ya kampeni na kwenye foleni, wakisubiri kupiga kura. Mbaya zaidi, CCM wako tayari kufanya mauaji kwa viongozi na wafuasi wa Chadema, tena wakishirikiana na vyombo vya dola na viongozi wa serikali ya CCM.
Jambo wanalopaswa kufahamu Chadema, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha.
Sikuwahi kukubaliana na wanaosema Watanzania hatuwezi kuheshimiana kwa sababu hatukuwahi kumwaga damu wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa nakubaliana nawo. Sihamasishi kumwaga damu, lakini nakubali kwamba dhuluma inafanyika kwa sababu hatuheshimiani, na hatuheshimiani kwa sababu hatujatoana damu.
Dhuluma wanayofanyiwa Chadema itaendelea, kama wao wataendelea kusubiri siku ambayo CCM watakubali kukaa mezani, hiyo siku haiwezi kutokea. Hakuna mazungumzo kati ya mtu anayepoteza (looser) na mtu anayefaidika (beneficiary). Mazungumzo na suluhu vitakuja vyenyewe ikiwa wote mnapoteza.

Kila kukicha tunasikia kiongozi wa CDM amechinjwa, mara amepotea, mara amekatwa katwa mapanga na kutupwa mtaroni, mwingine ametiwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya, wengine wanachomwa visu....hatusikii wa CCM wakifanyiwa hayo. Kwa hali hiyo, hakuna suluhu, kwa sababu anayepoteza (CDM) analialia, mnufaika (CCM) anafurahi. Lakini kama wote watalia, suluhu itakuja bila kuitwa.

Jambo wanalopaswa kufanya Chadema ni kujiandaa kifedha na kiintelijensia kabla ya 2020, la sivyo hawatapata jimbo hata moja.
Kujiandaa kifedha ni rahisi kuliko kujiandaa kiintelijensia. CCM hawana intelijensia zaidi ya kutegemea vyombo vya kiserikali. Lakini kama Chadema itawekeza kiuhakika kwenye intelijensia, ni Jeshi la wananchi pekee ndio litaweza kuidhibiti. "Jeshi" tu ndio chombo cha kogopa, na kuheshimu kiasi.
Idara ya usalama imejaa 'corrupts' na 'ignorant'. Wachache wanaojitambua hawawezi kufanya ujinga wa CCM, na hata wakirubuniwa hawawezi kufanya ujinga wa CCM kwa ufanisi wa kutosha. "Mtu anayefanya kazi kwa kurubuniwa au kulazimishwa hawezi kuifanya kwa ufanisi wa kutosha".
Zaidi wanaojitambua ndani ya vyombo vya dola, watakuwa radhi kutoa ushirikiano kwa Chadema kuliko CCM.
Na kwa hiyo, Chadema ikitaka kuunda intelijensia imara, itahitaji watu wa kujitolea. Ogopa mtu anayejitolea kupambana. Lakini pia anayejitolea anaweza kuwa 'ametumwa'.
Anyway! Jambo la msingi ndio hilo, kujiandaa. La sivyo, hakuna jimbo litaenda Chadema mwaka 2020. Kwanza hakutakuwa na uchaguzi zaidi ya vituko, na kama kweli Chadema wanataka kuirudisha nchi kwenye mstari, ni vema kujiandaa na vituko hivyo. Haipaswi hata kidogo kusubiri "Rais Mstaarabu" ili kupambana, hapana. Anayestahili "kupigwa" ni mtu asiye na ustaarabu. Mwaka 2020 unapaswa kuwa mwaka wa kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu tunavyofanyiana watanzania wenyewe kwa wenyewe. Na njia pekee iliyobaki ya kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu, ni kuwafanyia hao wahusika, vitendo visivyo vya kistaarabu.

Msimamizi anayetangaza matokeo ya uongo, halafu akaendelea kuishi kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Mkuu wa polisi anayetuma polisi kutishia watu, kupiga raia na kusaidia CCM, akiachwa aendelee kula maisha kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Kila kiumbe kinachofanya ujinga, kikaachwa kiendelee kuishi kwa raha mustarehe, kitarudia ujinga wake.

Kiongozi wa tume ya uchaguzi anayetumiwa na CCM kudhulumu demokrasia akiachwa aendelee kula maisha, atarudia tena.

Hao, wanatakiwa kukomeshwa, ili iwe funzo kwao na kwa wengine wenye tabia kama zao, na iwe funzo kwa anayewatuma.
Ukitaka kuua Nyoka, kata kichwa, ukishindwa, kata hata mkia, uwezekano ni kuwa atakimbia lakini tayari umempumguzia nguvu.

Nani mwenye uwezo wa kuwakomesha, bila kujiingiza katika mgogoro wa kisheria? Ndio hapo pa kuandaa intelijensia imara. Lawama ni bora kuliko fedheha, na katika hili anayestahili lawama ni CCM, na fedheha ni kwa Chadema. Mwaka 2020, Chadema ni vema walaumiwe kuliko kufedheheka.

Hata hivyo viongozi wakubwa wa Chadema hawapaswi kujiingiza katika hayo, kwasababu watakamatwa na kufungwa mara moja.
Na sisi wengine, tu waumini wa ubinadamu, ni rahisi zaidi kuachana na siasa kuliko kufanya hayo, hatuwezi hayo.

mr mkiki.
Mkuu, umeangalia upande mmoja wa ccm bila kuangalia jinsi ndani ya cdm hakuna demokrasia[emoji12] ! Kama wanataka demokrasia ianzie ndani yao cdm. Charity begins at home.
 
Dhumuni la chama chochote kilichopo madarakani ni kung'ang'ania dola isichukuliwe na wapinzani.

Kama vile CCM inavyo vitumia Vyombo vya Dola na Taasisi zake kusalia Madarakani kupitia Katiba inayo toa Mwanya kwa Taasisi hizo kutumika kirahisi.
 
Ww kutokuona kitu hakumaanishi kitu hicho hakipo. Huu ni utetezi wa kijinga.

Achana nae huyo anae ulizia kipeperushi wakati CCM wamejaza Makabati yenye Ilani lkn utekelezaji wake ukawa Ziro..
 
Ww kutokuona kitu hakumaanishi kitu hicho hakipo. Huu ni utetezi wa kijinga.
Sijawahi kuwasikia chadema majukwaani wakiongelea sera mbadala zaidi ya kuishambulia ccm.
 
Back
Top Bottom