Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Kama vile CCM inavyo vitumia Vyombo vya Dola na Taasisi zake kusalia Madarakani kupitia Katiba inayo toa Mwanya kwa Taasisi hizo kutumika kirahisi.
Kile kipindi kongamano lilikaa likasema kuwa tuende kwenye kura za maoni ya katiba mpya,viongozi wenu walijibu kuwa wana uhakika wa kuchukua dola wakichukua watabadili katiba ndio UKAWA ukazaliwa.
 
Kile kipindi kongamano lilikaa likasema kuwa tuende kwenye kura za maoni ya katiba mpya,viongozi wenu walijibu kuwa wana uhakika wa kuchukua dola wakichukua watabadili katiba ndio UKAWA ukazaliwa.

Hebu Soma ulicho andika kwanza mwenyewe kama ume kielewa ,maanake sijui hata ulikuwa una maana gani au ulitaka tujue nini ..
 
Sijawahi kuwasikia chadema majukwaani wakiongelea sera mbadala zaidi ya kuishambulia ccm.

Unasema hujawahi kuwasikia cdm wakiongea sera, sio kwamba hawaziongei ila hizo sera sio hitaji lako bali hitaji lako ni kuhakikisha ccm inabaki madarakani, hivyo yoyote anayezungumzia ccm kutoka madarakani ndio inabaki kichwani mwako.
 
RemarkableJauntyArchaeopteryx-size_restricted.gif
 
Kile kipindi kongamano lilikaa likasema kuwa tuende kwenye kura za maoni ya katiba mpya,viongozi wenu walijibu kuwa wana uhakika wa kuchukua dola wakichukua watabadili katiba ndio UKAWA ukazaliwa.
Ungejikita kwenye mada zaidi mkuu
 
Juhudi zako za kushinikiza ugaidi dhidi ya serikali halali iliyowekwa madarakani kwa njia ya kidemokrasia mimi siungi mkono hoja zako.
Pia, hebu sema ninafuraha sana watu wanapopigwa risasi na kuuwawa. Tamka ni juhudi zangu na pia naunga mkono
 
Pia, hebu sema ninafuraha sana watu wanapopigwa risasi na kuuwawa. Tamka ni juhudi zangu na pia naunga mkono
Sasa hivi hata mtu akifia gesti mnasema ni ccm,hakuna ushahidi kuwa watu wanaopigwa risasi kuwa wamepigwa na ccm.
 
Niko Fonti Feji.
Ila ukweli ndio huo, Chadem ni magaidi tu nao halali yao ni kupigwa tu. Tutawapiga na kuwapiga kila pale mtakapokuwa mnaenda kinyumé na taratibu za Nchi. Chadema hawana haki na nchi yetu.
Wana usajili sawa na wa CCM na wanachama wake ni waTZ kama wewe mkuu.
Ila mkuu akitaangaza kuwa nchi ni ya wanaCCM pekee na wengine ni wahamiaji basi uzi wako hapo juu utakuwa na maana sana.
 
Kwa hiyo wewe mkuu unataka VITA!
Mkuu sehemu yoyote huku duniani kama kuna machafuko jua kabisa kuna ukiukwaji ama wa haki za kibinadamu, ref kupotea kwa Ben Saanane, kuuliwa kwa Alfonce Mawazo kupigwa risasi kwa kamanda Lisu..
Uvunjifu na ukandamizwaji wa kisheria kama unavyoona wanavyofanya wateule wa rais. Kuwekwa mahabusu kwa diwani wa kitunda bila sababu za msingi. Kukataza wana siasa kufanya siasa wakati wamepewa haki hiyo na katiba, chaguzi zisizo za huru na haki.

Hayo yote hupelekea anayeonewa kuchoka na kutumia njia mbadala. Mwana Muzic Peter Tosh aliwahi kuimba....

Equal right n justice
 
Ni kweli ila ww umevuka kiwango cha heshima umehamia kwenye kujipendekeza na kuogopa hata kukosoa udhaifu wake kisa ni rais, na hata wale wanaothubutu kumkosoa, unawatafsiri kama wakosa nidhamu huki ukijificha kwenye rais kutukanwa as if ni jambo lilifanyika au linafanyika 24/7-365 a year.

Hii tabia ya kufumbia macho uovu eti kisa ni cheo cha rais inazigharimu tawala nyingi hasa nchi za kiafrika. Ndio maana unamtaja rais kwamba ni mtu mkubwa na sifa ya ukubwa ni hasi kwamba anaweza kukupoteza! Seriously hii ni sifa ya maana ya kutuonyesha uwezo wa rais? Kujipendekeza na kujitia upofu kwenye maovu sio jambo jema.
Hakuna anayejipendekeza, kwa taarifa yako tu ukiondoa Mwalimu Nyerere enzi zile nikiwa mtoto, sijawahi kuwa karibu na rais yoyote yule kati ya hawa waliomfuatia. Sina ndoto ya ukuu wa wilaya, ukurugenzi wala uwaziri. Najaribu tu kutumia haki yangu ya kutoa maoni kadri ninavyoyaona mambo ya nchi yetu.

Sihitaji cheo wala kitu chochote, ninachopinga ni hiki anachokisema mleta mada kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha, yaani ni kama anahamasisha watu waingie mtaani wafanye fujo!!.

Bado naamini tatizo lipo kwenye namna vyama vya upinzani vinavyokosa watu wanaoweza kuja na ideas mbadala kiasi ambacho CCM ikaonekana haifanyi la maana kwa wananchi. Baada ya uchaguzi wa 2015 CCM imefanya mapinduzi mengi ya ndani ya chama, CDM na wengine wameshindwa kuja kivingine, na inawagharimu.
 
Rais wa CCM na CCM yake, na polisi wake na wateule wake na vyombo vingine vya kisheria na dola, hawaamini katika demokrasia. Wao wakisikia Chadema wanachukulia kama ni waasi au magaidi. Kwa hiyo wanapambana kwa njia zote zisizo za kidemokrasia, bila kujali dhuluma wanayofanya kwa wananchi wanaotumia muda wao mwingi kwenye kwenye mikutano ya kampeni na kwenye foleni, wakisubiri kupiga kura. Mbaya zaidi, CCM wako tayari kufanya mauaji kwa viongozi na wafuasi wa Chadema, tena wakishirikiana na vyombo vya dola na viongozi wa serikali ya CCM.
Jambo wanalopaswa kufahamu Chadema, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha.
Sikuwahi kukubaliana na wanaosema Watanzania hatuwezi kuheshimiana kwa sababu hatukuwahi kumwaga damu wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa nakubaliana nawo. Sihamasishi kumwaga damu, lakini nakubali kwamba dhuluma inafanyika kwa sababu hatuheshimiani, na hatuheshimiani kwa sababu hatujatoana damu.
Dhuluma wanayofanyiwa Chadema itaendelea, kama wao wataendelea kusubiri siku ambayo CCM watakubali kukaa mezani, hiyo siku haiwezi kutokea. Hakuna mazungumzo kati ya mtu anayepoteza (looser) na mtu anayefaidika (beneficiary). Mazungumzo na suluhu vitakuja vyenyewe ikiwa wote mnapoteza.

Kila kukicha tunasikia kiongozi wa CDM amechinjwa, mara amepotea, mara amekatwa katwa mapanga na kutupwa mtaroni, mwingine ametiwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya, wengine wanachomwa visu....hatusikii wa CCM wakifanyiwa hayo. Kwa hali hiyo, hakuna suluhu, kwa sababu anayepoteza (CDM) analialia, mnufaika (CCM) anafurahi. Lakini kama wote watalia, suluhu itakuja bila kuitwa.

Jambo wanalopaswa kufanya Chadema ni kujiandaa kifedha na kiintelijensia kabla ya 2020, la sivyo hawatapata jimbo hata moja.
Kujiandaa kifedha ni rahisi kuliko kujiandaa kiintelijensia. CCM hawana intelijensia zaidi ya kutegemea vyombo vya kiserikali. Lakini kama Chadema itawekeza kiuhakika kwenye intelijensia, ni Jeshi la wananchi pekee ndio litaweza kuidhibiti. "Jeshi" tu ndio chombo cha kogopa, na kuheshimu kiasi.
Idara ya usalama imejaa 'corrupts' na 'ignorant'. Wachache wanaojitambua hawawezi kufanya ujinga wa CCM, na hata wakirubuniwa hawawezi kufanya ujinga wa CCM kwa ufanisi wa kutosha. "Mtu anayefanya kazi kwa kurubuniwa au kulazimishwa hawezi kuifanya kwa ufanisi wa kutosha".
Zaidi wanaojitambua ndani ya vyombo vya dola, watakuwa radhi kutoa ushirikiano kwa Chadema kuliko CCM.
Na kwa hiyo, Chadema ikitaka kuunda intelijensia imara, itahitaji watu wa kujitolea. Ogopa mtu anayejitolea kupambana. Lakini pia anayejitolea anaweza kuwa 'ametumwa'.
Anyway! Jambo la msingi ndio hilo, kujiandaa. La sivyo, hakuna jimbo litaenda Chadema mwaka 2020. Kwanza hakutakuwa na uchaguzi zaidi ya vituko, na kama kweli Chadema wanataka kuirudisha nchi kwenye mstari, ni vema kujiandaa na vituko hivyo. Haipaswi hata kidogo kusubiri "Rais Mstaarabu" ili kupambana, hapana. Anayestahili "kupigwa" ni mtu asiye na ustaarabu. Mwaka 2020 unapaswa kuwa mwaka wa kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu tunavyofanyiana watanzania wenyewe kwa wenyewe. Na njia pekee iliyobaki ya kukomesha vitendo visivyo vya kistaarabu, ni kuwafanyia hao wahusika, vitendo visivyo vya kistaarabu.

Msimamizi anayetangaza matokeo ya uongo, halafu akaendelea kuishi kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Mkuu wa polisi anayetuma polisi kutishia watu, kupiga raia na kusaidia CCM, akiachwa aendelee kula maisha kwa raha mustarehe, atarudia tena.

Kila kiumbe kinachofanya ujinga, kikaachwa kiendelee kuishi kwa raha mustarehe, kitarudia ujinga wake.

Kiongozi wa tume ya uchaguzi anayetumiwa na CCM kudhulumu demokrasia akiachwa aendelee kula maisha, atarudia tena.

Hao, wanatakiwa kukomeshwa, ili iwe funzo kwao na kwa wengine wenye tabia kama zao, na iwe funzo kwa anayewatuma.
Ukitaka kuua Nyoka, kata kichwa, ukishindwa, kata hata mkia, uwezekano ni kuwa atakimbia lakini tayari umempumguzia nguvu.

Nani mwenye uwezo wa kuwakomesha, bila kujiingiza katika mgogoro wa kisheria? Ndio hapo pa kuandaa intelijensia imara. Lawama ni bora kuliko fedheha, na katika hili anayestahili lawama ni CCM, na fedheha ni kwa Chadema. Mwaka 2020, Chadema ni vema walaumiwe kuliko kufedheheka.

Hata hivyo viongozi wakubwa wa Chadema hawapaswi kujiingiza katika hayo, kwasababu watakamatwa na kufungwa mara moja.
Na sisi wengine, tu waumini wa ubinadamu, ni rahisi zaidi kuachana na siasa kuliko kufanya hayo, hatuwezi hayo.

mr mkiki.
Hivi Mungiki sera yao ilikuwaje
/
 
Mkuu sehemu yoyote huku duniani kama kuna machafuko jua kabisa kuna ukiukwaji ama wa haki za kibinadamu, ref kupotea kwa @Ben Saanane, kuuliwa kwa Alfonce Mawazo kupigwa risasi kwa kamanda Lisu..
Mkuu hii njia mbadala ya kutafuta haki(vita) imewahi kuleta suluhisho la kudumu popote pale duniani???
 
Mkuu sehemu yoyote huku duniani kama kuna machafuko jua kabisa kuna ukiukwaji ama wa haki za kibinadamu, ref kupotea kwa Ben Saanane, kuuliwa kwa Alfonce Mawazo kupigwa risasi kwa kamanda Lisu..
Uvunjifu na ukandamizwaji wa kisheria kama unavyoona wanavyofanya wateule wa rais. Kuwekwa mahabusu kwa diwani wa kitunda bila sababu za msingi. Kukataza wana siasa kufanya siasa wakati wamepewa haki hiyo na katiba, chaguzi zisizo za huru na haki.

Hayo yote hupelekea anayeonewa kuchoka na kutumia njia mbadala. Mwana Muzic Peter Tosh aliwahi kuimba....

Equal right n justice

Na kwa kifupi kabisa 'Amani' inayo 'Kanuni yake ,hivyo unapo fanya kinyume na 'Kanuni' inayo zalisha hiyoAmani basi Matokeo yake ni Ghasia/Machafuko na Amanihupotea.Amani hailindwi na Mitutu ya Bunduki kama Watawala wanavyo dhani ,Haki ndio Msingi Mkuu wa 'Amani'..
 
Hakuna anayejipendekeza, kwa taarifa yako tu ukiondoa Mwalimu Nyerere enzi zile nikiwa mtoto, sijawahi kuwa karibu na rais yoyote yule kati ya hawa waliomfuatia. Sina ndoto ya ukuu wa wilaya, ukurugenzi wala uwaziri. Najaribu tu kutumia haki yangu ya kutoa maoni kadri ninavyoyaona mambo ya nchi yetu.

Sihitaji cheo wala kitu chochote, ninachopinga ni hiki anachokisema mleta mada kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha, yaani ni kama anahamasisha watu waingie mtaani wafanye fujo!!.

Bado naamini tatizo lipo kwenye namna vyama vya upinzani vinavyokosa watu wanaoweza kuja na ideas mbadala kiasi ambacho CCM ikaonekana haifanyi la maana kwa wananchi. Baada ya uchaguzi wa 2015 CCM imefanya mapinduzi mengi ya ndani ya chama, CDM na wengine wameshindwa kuja kivingine, na inawagharimu.

Unaposema ccm imefanya mapinduzi toka 2015. Hayo mapinduzi na tija ni maisha ya wananchi, na sehemu ya kuonyesha mwitikio wa wananchi ni hizi chaguzi ndogo wangalau kwa sasa. Lakini ni ukweli ulio dhahiri box la kura haliheshimiwi na ushahidi upo. Sasa katika mazingira hayo unatuaminishaje kama hayo mapinduzi ndani ya ccm wananchi wameona tija yake huko eneo la tathmini ambayo ni watu kupitia kura hapaheshimiwi?

Sasa hvi hakuna mijadala ya wazi yenye kuweza kukosoa zaidi ya mijadala ya kusifia. Kuna mambo mengi hayako sawa na ni mwiko hayo kujadiliwa kwa kisingizio kwamba rais anafanya vyema. Sasa hivi sehemu pekee unapoweza kuona mijadala huru ni huku vichochoroni (social media) ambapo ID fake zimetamalaki. Ni kweli kuna mazuri machache yaliyofikiwa, lakini kwanini si ruhusa hayo mapungufu kujadiliwa wazi? Huu wizi wa kura, sorry uporaji wa kura unafanyika wazi kwani wanaofanya hivyo wana uhakika hakuna nguvu ya kuhoji. Huyu muanzisha uzi ni mmoj tu kati ya wengi wasiokubaliana na mwenendo mzima wa demokrasia. Na hii tabia yenu ya kukalia uovu kimya kisa unafanyw na unayemshabikia sio poa.

Mabadiliko ndani ya upinzani yanakuathiri nini ww? je wapinzani kutokufanya mabadiliko kwa utashi wa ccm ndio kuhalalishe wao kufanyiwa ukatili kwa matumizi mabaya ya cheo cha urais? Ingekuwa hayo mabadiliko yanayohubiriwa na ccm yafanyike ndani ya upinzani yana athari kwenye maisha ya wananchi ningekuelewa. Sasa mnasema ccm imebadilika inakuwaje itoke kwenye wizi wa kura mpaka uporaji?
 
Back
Top Bottom