James Gayo: Hulka ya Ushindi wa 100%

James Gayo: Hulka ya Ushindi wa 100%

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Kijana yatima kijijini aliyetamani kuoa alikuwa amekwama; hakuwa na uwezo wa mahari, achilia mbali pesa ya kuandaa harusi, na umri ndio ulikuwa unazidi kuyoyoma! Mawazo yalipomzidi akaamua kwenda kuomba ushauri kwa jirani yake - kikongwe aliyeishi peke yake baada ya kufiwa na familia yake yote.

Jamaa yetu aliposimulia shida yake, mzee akaingiwa na huruma sana. Mzee akamwambia kwa kuwa hakuwa na mrithi na siku zake za kuishi zilikuwa zinahesabika, basi kijana aingie zizini mwake na achukue ng’ombe tisa kati ya kumi aliokuwa nao! Jamaa aliyekuja kwa mzee akitegemea kupata ushauri wa hekima tu hakuamini kujipatia bingo ya ng’ombe tisa ghafla namna ile! Mapigo ya moyo yakamwenda kasi, nusura ashindwe kupumua! Ng’ombe wawili tu wangemtosha kutatua shida yake ya mahali.

Wakati akiswaga ng’ombe wake kuelekea nyumbani maswali mengi yalimsumbua: Ukarimu wa namna gani huu, hivi yule mzee ni mzima kichwani? Ng’ombe wawili tu wangetosha kulipa mahali, saba wanaobakia awafanyie nini, awauze au afuge?...

Usiku mawazo yaliendelea kumsumbua mpaka usiku akashindwa kulala. Ikafikia mahali akaanza kufikiria kuwa pengine angeielezea shida yake vizuri zaidi, mzee angeweza kumpa ng’ombe wote kumi! Jamaa akaanza kujilaumu kwa kuambulia tisa wakati angeweza kupata wote kumi!

Mawazo yalipozidi kumtesa, jamaa yetu akaamka usiku wa manane na kwenda kuiba ngo’mbe mmoja aliyesalia zizini mwa yule kikongwe!

©James Gayo
 
Binadamu ndivyo tulivyo, CCM ina kil kitu, imepora viwanja vya michezo vyote, imeidhibiti hazina, na kila kitu na kila kitu, ila bado hairidhiki tu, dah!!
 
Hadithi hii amekufundisha nani na inatufundisha nini?
 
Back
Top Bottom