NCCR Mageuzi
Member
- Oct 3, 2007
- 23
- 63
Septemba 19, 2020 Viwanja vya Polisi Himo, Moshi mkoani Kilimanjaro viliwaka moto huku ikishuhudiwa maelfu ya wanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na wakaazi wa jimbo la Vunjo kutoka kila kona ya Moshi wakimiminika kwenye viwanja hivyo kumlaki na kumsindikiza mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mgombea Ubunge jimbo la Vunjo Injinia Ndugu James Francis Mbatia kwenye uzinduzi wa kampeni ndani ya Jimbo la Vunjo.
Mbatia akiambatana na madiwani wa kata zote za Jimbo la Vunjo aliongoza ufunguzi wa mkutano wa kampeni kwa kueleza mambo ambayo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amewafanyia wana Vunjo.
Mbatia akiambatana na madiwani wa kata zote za Jimbo la Vunjo aliongoza ufunguzi wa mkutano wa kampeni kwa kueleza mambo ambayo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amewafanyia wana Vunjo.