DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, James Mbatia, ametoa wito kwa taasisi za kikanda kuwatuma viongozi wastaafu wenye ushawishi barani Afrika kusaidia kuratibu mchakato wa kuweka ukweli hadharani na kuhakikisha haki inapatikana kufuatia matukio ya siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza na Jambo TV tarehe 24 Novemba 2025, Mbatia amesema hatua iliyofikiwa sasa inahitaji hekima na uongozi wa juu kutoka kwa “wazee wa Afrika” ili taifa lipate njia sahihi ya kuponya majeraha ya kisiasa na kijamii.
“Kwa moyo wa dhati kabisa, ninaomba wazee wa bara letu la Afrika wenye uadilifu wa hali ya juu waweze kutusaidia kuratibu jambo hili ili ukweli ujulikane na uwajibikaji kuwepo,” amesema.
Ameeleza kuwa viongozi kama Rais mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, pamoja na aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa watu wanaoweza kusaidia kuongoza hatua hiyo nyeti kwa sababu ya uzoefu na heshima waliyojijengea barani. Amesema kuwa hatua hii ni muhimu ili kuzuia hali isiendelee kuzorota, akionya kuwa kusubiri tatizo lijitokeze tena kutakuwa ni kujitafutia majanga mapya.
Ameonya kuwa kunakoelezwa kutokea tarehe 9 Disemba ni miongoni mwa sababu za kuharakisha hatua za kinga, akisisitiza umuhimu wa usimamizi wa kitaasisi na ki-uwazi, akisema kuwa kushughulikia matukio ya uchaguzi inapaswa kuanza na kukubali ukweli na kuweka hadharani maelezo ya kilichotokea, ili kujenga msingi wa uwajibikaji.