The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amesema hakuna chama cha siasa ambacho ni kiranja kwa mwenzake, huku akivitaka vyama katika uchaguzi mkuu kushindana kwa hoja.
Sambamba na hilo, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha haki inatendeka kwenye uchaguzi huo kwa kusimamia sheria na kuwaondoa wale wote wanaotaka kuitia doa Tume hiyo.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na watiania 113 wa nafasi za ubunge kupitia chama hicho Tanzania Bara. Alisema Chama hicho ni cha kuunganisha Taifa na sio cha mkoa mmoja na kabila moja, hivyo kwenye uchaguzi vyama vishindane kwa hoja za msingi na si kwa propaganda.
“Wale wanaosema NCCR kinataka kufungua NGO ni ndoto za alinacha sisi upole wetu sio dhaifu…Na sio vyama vingine vitake tufuate mbinu zao, hakuna chama ambacho ni kiranja wa mwenzake hapa hakipo,” alisema.
Mbatia aliongeza: “Mbona kuna watu wengi waliondoka NCCR hatukulalamika na tuliwatakia kila la kheri wengine sasa wamerudi kwenye asili yao imeibuka minong’ono, hapa ndio asili ya mageuzi ya nchi, uwezo huo tunao na twende kifua mbele kwa kujiamini na tunaweza.”
Mbatia alisema katika uchaguzi Tume ihakikishe haki sawa inatendeka katika kampeni na uchaguzi. “Kwenye kura tupigiwe kura sisi halafu tutulie tuseme sisi ni watu wa utu hiyo hapana, yaani nione Selasini amepigiwa kura Rombo ameshinda, haki yetu lazima tuitafute kwa gharama yoyote lakini gharama ya amani, maelewano, sheria na kuifanya Tanzania kuwa sehemu salama ya kuishi,” alisema.
Aliviomba vyama vingine kutambua kuwa mambo ya uchaguzi ni shirikishi na kuvumiliana kwa kuwa na fikra tofauti.
“Itikadi yetu ni kati ya itikadi bora duniani, sisi tutahubiri yaliyomema, Watanzania tunaomba wachague madiwani, wawakilishi, wabunge wa NCCR Mageuzi,” alisema.
Kadhalika, alisema chama hicho kinaamini haki ya mtu binafsi kugombea.
Alisema kwa kuchagua wabunge na madiwani wa chama hicho ana uhakika kilio chao cha kupata Katiba mpya kitasikilizwa.
Chanzo: IPP Media