James Mbatia: Vyama vya siasa ndio vimeharibu kwa kuingilia uchaguzi wa Serikali za Mitaa

James Mbatia: Vyama vya siasa ndio vimeharibu kwa kuingilia uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Mifumo yetu ya sheria ina tatizo kubwa sana eti ofisi ya Rais ndio inasimamia uchaguzi halafu utegemee haki kwa vyama vingine.
Tatizo la Msingi hapa Tanzania ni ukosefu wa Katiba ya Wananchi na inayoheshimiwa,Hii iliyopo,pamoja na upungufu wake wote haifuatwi na Watawala wetu hawapo tayari kuirekebisha.Tulikosea sana mwaka 2014 kwa kuacha tupitwe na fursa pekee ya kurekebisha makosa ya nyuma kwa kuruhusu wanasiasa wateke mchakato wa Katiba ya Warioba.
Tunatakiwa kwa pamoja tudai Katiba ya Wananchi kwa manufaa ya Taifa letu.Wadau tuunganisheni tuweze kupaaza sauti zetu.
 
Utumiage akil kidogo na wewe. Huu mfumo wetu ndio kila mwaka tunavutana na kutoa damu. Saiz jafo ndio ameheuka kuwa mfumo sasa unasemaje ni bora kuliko huo ambao jamaa ameelza na kuonesha kama unamapungufu basi ni nafuu. Sikia sio kutetea kila ujinga wa tanzania ndip uzalendo sawa.

Kutetea nini?. Huwa sitetei chochote aslani, naongea ukweli ninanavyoona bila mapenzi au ufuasi kwa awaye yote
Mungubl ni mwema sana. Usiku mwema
 
Kifikra upo sahihi sana, lakini kimtazamo wa uhalisia Serikali inayowekwa na chama ndo yenye dola, na watumishi wake kutokana na kuangalia maslahi inawalazimu kuvaa ukijana ili wale green pasture vizuri, ni ngumu kuliepuka hilo kwenye zama hizi za viongozi wa maslahi binafsi.
Nilikuwa civil servant kwa 37 yrs mmoja wa wanasiasa niliofanya kazi nao ni Jiwe. Alikuwa hivi hivi ila alikuwa akikwaa kisiki unapokuja watumidhi tuliokuwa tunazingatia utaratibu wa serikali unaosimamiwa na wataalamu pia kilikuwa na delivery ya mipango ya serikali. Sasa hivi hata bajeti ya serikali ipo mfukoni mwa mtu. Pathetic kwa sababu kama watumishi wa serikali wangefanya kazi zao huu ujinga wote usingekuwepo na wanasiasa wangeheshimu serikali.
Kwa sasa tuna a failed state ambayo organ zote za serikali zimesurrender kwa chama dola.
Kifupi mamlaka ya serikali si wananchi tena. Sitaki kutabiri uvunjifu wa amani. Ila nina uhakika wa malipizi ya kujitoa mhsnga.
 
Hili nakubaliana nalo kwa sehemu kubwa , yaani kungetafutwa utaratibu viongozi wa serikali za mitaa na vijiji wasidhaminiwe na chama chochote bali wana jamii wawapate viongozi wao kwa namna nzuri uliowekwa na jamii husika. Mfano Kijiji kipendekeze majina ya watu sita kwa mfano wazee wawili, vijana wawili na wamama wawili. Hawa wanapigiwa kura na anayepata kura nyingi anakuwa ndiye mwenyekiti wa kijiji, mwanamke (Mama )anayefuata kwa kura anakuwa makamu mwenyekiti.

Mapungufu ya mfumo huu wa sasa ni kumomonyoa misingi ya amani na utulivu katika jamii. Uchaguzi wa vyama vijijini na mitaani umeleta ufa kubwa sana miongoni mwa wanajamii. Mfano kijijini kwetu kuna ukoo uligawanyika vibaya sana kwani mgombea wa CDM na CCM walitokea kwenye ukoo huo , matokeo yake wakagawa ukoo kabisa (uchaguzi wa mwaka 2014) . Katika uchaguzi huo huo baadhi ya waumini wa kanisa la RC ya pale kigangoni kwetu walisusa kanisa baada ya katekista kuwa ndiye mpiga debe wa CCM hatimaye waliojiengua wakaanzisha kanisa lao.

Uchaguzi huu ndiyo umekuwa balaa zito , naambiwa mtendaji anaishi kama digi digi kwa kujificha baada ya kumuengue mgombea ambaye vijana waliapa kumpa uenyekiti, Sasa maisha haya hayafai kijijini yaani huko kwetu mtu anaibiwa mifugo watu wakijua ni wa ccm au wa chadema wengine hawatokei kusaidia kisa eti huyo si wa chama chao. Hali itakuwa tete sana kwa siku zijazo
Hiki chama cha kijani cha mamumiani wa CCM kimeharibu sana hii nchi.
 
Kwamba local governments iwe ni wagombea binafsi tu ila sidhani kama vyama vya siasa vitaepukwa kirahisi hivyo ni lazima vitajipenyeza tu.

Angalia chaguzi za serikali za wanafunzi kwenye taasisi za elimu vyama vinavyofanya, itakuwa hivyo pia.

Naamini wanaovuruga hizi chaguzi wanafahamika kikubwa watu tuheshimiane tu na taratibu zifuatwe kama ni mbovu zibadilishwe.
vyama vitaingilia tu hasa chamadola lakini itajulikana kama inavyojulikana sasa kwenye vyuo. kigezo kimojawapo cha kuenguliwa kwenye uchaguzi huo kiwe kuingia kinyanganyiro kwa mbeleko ya chama chochote kile. shime inawezekana. hakuna dhambi kuiga uganda tukaboresha zaidi hata wenyewe wakaiga tulichoiga kwao- very well refined!
 
Kwamba local governments iwe ni wagombea binafsi tu ila sidhani kama vyama vya siasa vitaepukwa kirahisi hivyo ni lazima vitajipenyeza tu.

Angalia chaguzi za serikali za wanafunzi kwenye taasisi za elimu vyama vinavyofanya, itakuwa hivyo pia.

Naamini wanaovuruga hizi chaguzi wanafahamika kikubwa watu tuheshimiane tu na taratibu zifuatwe kama ni mbovu zibadilishwe.

hata makansani ccm inapenyeza wat
 
Mseven siyo dictator ila ukitaka kumtambua vizuri tangaza nia ya kugombea uraisi alllooooo utaisoma namba na ndo utamjua kuwa mseven ni nan
Naona wewe umeweza kusoma katikati ya mistari. Kulingana na matatizo ambayo Uganda imepitia tangu ukoloni, nguvu za utamaduni (hapa tunakosea kwa kuuita ukabila) ambavyo vilipelekea hadi kuibuka mtu dizaini ya Iddi Amin ni wazi utawaliwaji wake hauwezi kuwa rahisi rahisi.
M7 anajua siasa za Kiafrika na ndio maana akaja na huu ukweli kwamba ni lazima kuwepo na demokrasia ya kweli kwenye glassroots na ndio maana unakuta hata uchaguzi wa wabunge pamoja na kuwa chama tawala lakini haki inatendeka kwa kiasi cha juu sana. Mfano huyo Bobi Wine aliweza kushinda ubunge kwa kura lakini ingelikuwa nchi ya kusadikika labda ungelishuhudia mtu anakimbia na box la kura mcha kweupe alafu baada ya masaa kadhaa linarudishwa na upigaji kura unaendelea, mwishowe uchaguzi unatukuzwa kuwa "ulikuwa huru na haki haijawahi kutokea katika awamu zote" 😎
 
Nadhani hujaelewa wanachozungumzia hapa. Ni hivi: Uchaguzi wa serikali za mitaa usiwe unahusisha vyama. Uwe ni uchaguzi wa kuchagua viongozi bila kushirikisha vyama. Sasa unaposema anamaanisha CCM una maana ndicho chama cha siasa pekee kilichopo, kumbe viko vingi.
Kama ni hivyo kwani Mbatia hajui kuwa Tanzania hakuna mgombea binafsi?.
 
tatizo ni CCM wanataka kushinda kwa kutumia maguvu.
 
Magu ana roho ya uharibifu ataipasua nchi tuchukue tahadhari na kumzuoa
Ni kweli kabisa, mabavu ya Watawala kudhania kila kitu kinawezekana kwa kutumia nguvu kitalifikisha taifa pabaya kwani tulishashindwa kwenye korosho. Haiwezekani uchaguzi huu uharibiwe na mamlaka ya Ikulu kwani ndie Waziri wa Wizara husika. Wengi tulitia shaka baada ya serikali kutumia fedha na muda kuwapeleka Watendaji wa kata wote nchi nzima Ikulu. Matokeo ndio haya tunayaona na kwa mtu ye yote mwenye utashi ni aibu kubwa kwa Watawala na nchi kwa ujumla kwamba hatuwezi kujiongoza. Hawa watendaji wametenda jinai kwa sheria zetu za uchaguzi huu wa serikali za mitaa lakini hakuna anayeongelea jinai hiyo kwa hofu ya aliyeasisi hiyo jinai. Wamefanya jinai kwa kujiamini mno kwani haiwezekani mtendaji akafunga ofisi katika kipindi ambacho ni muhimu kwa ustawi wa demokrasi na amani lakini hakuna mtu anayeongelea hii jinai.
Jamani, hii Tanzania ni yetu sote na ni zaidi ya vyama vyetu kwani hivi vyama vinaweza kufa kama KANU kule Kenya lakini nchi yeu itabaki. Sidhani kuna anayependa kufikia hatua waliyofikia Sudan, Misri, Libya, Somalia, Syria n.k. bado tunapenda amani yetu iliyotokana na upendo itamalaki na si amani ya bunduki na polisi. Vyombo vyetu vya usalama na hasa TISS ni wakati wake sasa kumshauri Mheshimiwa Rais kuwa hali sio nzuri huku mtaani kwani watu wana hasira na chuki miongoni mwao imeanza kuwa kubwa kutokana na tofauti ya vyama.
Pia tunaanza kuiona hatari waliomo Watendaji ambao wametenda bila kujali kuwa wao bado ni vijana na wangependa kufika mbali katika maisha yao ya utumishi lakini kumbukumbu zimesha wekwa kuwa nani kafanya nini katika kuvuruga demokrasi ya nchi hii. Waliowatuma wana kinga na wana uhakika wa kuishi maisha yao yote yaliyobaki wakilindwa na sheria lakini wao sehemu kubwa ni vijana ambao wanaweza kuja kukabiliwa na jinai kwani jinai huwa haifi kisheria.
Yatupasa wote kumlilia Mungu na kusimama kuwa wakweli ili kuinusuru nchi na machafuko, tuache kuzika vichwa vyetu kwenye mchanga. Kila mmoja kwa nafasi yake bila kujali itikadi zetu tupaze sauti pasipo unafiki kwa masilahi ya nchi yetu pendwa Tanzania na vizazi vyetu.
Mungu ibariki Tanzania
 
Kwa akili zako unafikri anaposema vyama vya siasa ndivyo vinavyoharibu kwa kuingilia uchaguzi unafikri anamaanisha vyama gani zaidi ya CCM?ambayo imetufikisha mahali tulipo mpaka sasa,na hata kama itaachiwa tume bila wananchi kuthaminiwa katika matakwa yao mambo yataendelea kuwa vilele kwa sababu tume ya uchaguzi ndio watendaji wenyewe,waliokua wanafunga ofisi wapinzani wanapotaka kwenda kuchukua form.
Kwanini wapinzani wasiende masaa yaleyale pamoja na wa ccm? Kwani wao walitaka waende kwa masaa maalumu?
 
Kwanini wapinzani wasiende masaa yaleyale pamoja na wa ccm? Kwani wao walitaka waende kwa masaa maalumu?
Kila kitu kilikuwa shwari na kilifanywa kwa usahihi Kama inavyotakiwa na kwa wakati mwafaka, hizo zingine sijui wapinzani hakufanya hiki na kile mara walikosea kile hizo ni propaganda za CCM kwa kuwa wao ndio wameshika kwenye mpini.
 
Back
Top Bottom