James Mbowe ameonesha ana kipaji kikubwa cha uongozi, achukue fomu kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimefuatilia kwa karibu shughuli za kisiasa za ndugu James Mbowe. Nimeridhika kabisa anafaa kukamata nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.



Ni mwanamageuzi kindakindaki, amepikwa kisiasa akaiva, na amekuwa mstari wa mbele katika harakati za chama.

Nashauri CHADEMA wafikirie kumpa Uenyekiti wa chama taifa.

Pipooooz.....!!!!
 
Ili akishapewa CCM muanze kupiga kelele za wanarithishana uongozi, propaganda zenu bado sana.
Nahisi mleta mada ndio James Mbowe mwenyewe, labda baba yake kamtuma kuja kupima upepo na kuwandaa watu kisaikolojia.

Hizi ndio siasa zilizoasisiwa Tanzania.
 
Mkuu James mbowe kakupa Shilingi ngapi maana umekuja na bandiko kana kwamba Kila mtu anamfahamu
 
Mmmmm kuna royal family somewhere, baba ex president mama ni MP,mtoto ni minister, na upumbavu huu unaonyesha madhara ya middle class ya kushindwa ile reading to the meaning, mtoa mada ametoa maoni yake na CDM ina utaratibu ndani ya katiba yake kuhusu nafasi ya Chairman, haigawiwi kama vyeo vya U DC ambao wengi humu wanajitoa ufahamu ili wapewe u DC!,ngoja niendelee na mbeta zangu za ulanzi hapa lingusenguse
 
Chama cha ccm ndio family affairs!,makambas, kikwetes,kawawas, etc etc...
 
Ni kiongozi mzuri sana, Ila anahitaji muda na malezi zaidi kuelekea kubeba majukumu makubwa zaidi katika Uongozi.
 
Acha wivu mkuu! Mbona Makamba na Makamba junior, Mhe Kikwete na Junior pia yupo tena Naibu Waziri. Tatizo nini

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…