Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai kupitia CHAUMMA, James Mbowe amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Hai, atahakikisha vijana wa kata zote 17 za Jimbo hilo wananufaika moja kwa moja na fursa zinazotokana na Mlima Kilimanjaro.
Ameeleza kuwa atatenga fedha za asilimia 10 za Halmashauri pamoja na fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana 50 katika kila kata.
“Tutawapeleka vijana kwenye mafunzo ya lugha ili waweze kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kupandisha wageni Mlima Kilimanjaro. Leo hii wageni wengi wanapandishwa mlima na watu kutoka nje ya jimbo letu, wakati vijana wetu wanakosa ajira, wanakaa vijiweni na wengine kujiingiza kwenye ulevi na uhalifu,” alisema Mbowe.
“Kijana anapokuwa hana cha kufanya, anakimbilia ulevi na vitendo vya uhalifu. Lakini kupanda mlima hakuhitaji digrii wala diploma, kunahitaji tu utayari na nguvu. Hii ndiyo nafasi ya vijana wetu kuamka na kujiinua kimaisha,” alisisitiza Mbowe.
Mbowe amewataka wananchi wa Weruweru na jimbo zima la Hai kumpa kura ili kwa pamoja wajenge mazingira bora ya vijana kupata kipato kupitia utalii wa Mlima Kilimanjaro na kukuza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.