- Source #1
- View Source #1
Wakuu nmeona video ikielezea kuwa miongoni mwana ukoo wa mwanzilishi wa Whiskey alimnunua binti wa miaka kumi huko Congo miaka ya 1880 na kisha kumtizama akiuliwa na kuliwa.
- Tunachokijua
- James Sligo Jameson muwindaji, mvumbuzi na mtaalamu wa mitishamba ni mjukuu wa Jameson Irish Whiskey muanzilishi wa kinywaji maarufu cha Jameson Whiskey. James alizaliwa 17 Agosti, 1856 na kisha baadaye kuwa mrithi wa kinywaji cha Whiskey na mali za ukoo wao. James kipindi cha uhai wake alipenda kuwa mtembezi na hivyo akiwa na miaka 20 tu aliweza kwenda maeno mbalimbali ikiwemo Kusini mwa Afrika, Hispania na Algeria.
Baadaye akajiunga na msafara uliojulikana kama “Emin Pasha Relief Expedition” ulioongozwa na Henry Morton Stanley, lengo la msafara huu ulikuwa ni kumuokoa Emin Pasha gavana wa Equatorial ambayo kwa hivi sasa ni sehemu ya Sudani Kusini ambaye alikuwa katika hatari dhidi ya vikosi vya Mahdisti.
Madai
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zikieleza kuwa James Jameson mrithi wa utajiri wa Jameson Whiskey miaka ya 1880’s alimnunua mtumwa binti wa miaka 10 na kumshuhudia akiuliwa na kuliwa huko nchini Congo.
Uhalisia upoje?
JamiiCheck imefuatilia machapisho na makala mbalimbali za kihistoria na kubaini kuwa madai hayo ni ya kweli. Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa James alipokuwa Congo alitekeleza kitendo hiko na kisha kuchora picha za tukio hilo.
Tovuti ya Bizzaro kupitia makala yao yenye kichwa kilichosomeka “Six Handkerchiefs for the cannibals: The Infamous ‘Jameson Affair’ ” waliyoichapisha katika tovuti hiyo waliandika kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo lililojulikana kama Ribakiba ambapo kwa hivi sasa linajulikana kama Lokandu.
Makala hiyo inaendelea kwa kueleza kuwa Kwa mujibu wa Assad Farran ambaye alikuwa ni mkalimani wa James, wakati James anakutana na viongozi wa kikabila wa eneo hilo, ilionekana kuwa James alikuwa na kiu sana ya kufahamu kuhusu taarifa alizokuwa akizisikia kuhusu kitendo cha watu kuua binadamu wenzao na kisha kuwala katika eneo hilo. James alisema kuwa “Uingereza tumesikia sana kuhusu watu wanaokula watu, lakini mimi kuwepo katika eneo hili nitatamani sana kuona kwa macho yangu”
Viongozi hao wa eneo hilo walimwambia James kuwa ni kweli jambo hilo ni la kawaida na kama anahitaji kushuhudia basi hana budi kumnunua mtumwa kutoka katika kijiji cha jirani na hapo ndipo vitambaa sita vikatumika kama malipo ya kumnunua mtumwa huyo wa miaka 10.
Kupitia diary yake yeye mwenyewe James ambayo imehifadhiwa hapa mwezi wa tano mwaka 1888 aliandika kuhusu tukio hilo kwa kuandika kuwa baada ya kuzungumza na viongozi hao mtu mmoja akamgeukia na kumwambia “nipe kipande cha nguo kisha ujionee”. Baada ya muda James alimtuma kijana wake awape watu wale leso (vitambaa) sita na kisha baada ya muda akaona binti wa miaka kumi akiletwa mbele yake.
“Na kisha nikaona maono yakutisha sana niliyowahi kuyaona maishani mwangu Aliingiza kisu haraka kwenye titi la binti mara mbili, na akamwambia usoni, akigeuka upande wake. Ndipo watu watatu wakakimbia mbele, wakaanza kuukata mwili wa yule msichana; hatimaye kichwa chake kikakatwa, hakubaki hata chembe, kila mtu akachukua kipande chake kuelekea mtoni kukiosha. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba msichana yule hakutoa sauti yoyote, wala kutetereka, hadi akaanguka”. James aliandika.
James anaeleza kuwa lilikuwa tukio la kutisha sana kulishuhudia kwani lilikuwa la kuogofya mno ingawa wakazi wa pale hawakuonesha kushtuka na baada ya muda alienda kwenye makazi yake na kuchora picha ya tukio hilo ikiwa bado ya moto kichwani mwake.
“Msichana alikuwa ni mtumwa aliyetekwa kutoka kijiji kilichokuwa karibu na mji huu, na wale waliokuwa wakila nyama ya binadamu walikuwa ni watumwa wa Wacusu, na wenyeji wa sehemu hii, waliitwa Mculusi”.
“Niliporejea nyumbani, nilijaribu kuchora michoro midogo ya tukio hilo nikiwa bado na kumbukumbu nzuri, si kwamba inaweza kamwe kupotea kutoka katika kumbukumbu yangu”. Aliandika James.
Aliyekuwa mkalimani wa James, aliyeitwa Faran alitoa kiapo chake ambacho kilichapishwa na New York Times mwaka 1890 alieleza kuwa;
"Alipofika kwenye vibanda vya asili msichana, ambaye aliongozwa na mtu aliyemleta, aliwasilishwa kwa cannibals. Mwanamume huyo aliwaambia: “Hii ni zawadi kutoka kwa mzungu. Anataka kuona jinsi unavyomla”. Msichana alichukuliwa na kufungwa kwa mikono kwenye mti. Wenyeji wapatao watano walikuwa wakinoa visu. Kisha mtu mmoja akaja na kumchoma kisu mara mbili tumboni. Msichana hakupiga kelele, lakini alijua kinachoendelea. Alikuwa akitazama kulia na kushoto, kana kwamba anatafuta msaada. Alipochomwa kisu alianguka chini na kufa. Kisha wenyeji walikuja na kuanza kumkata vipande vipande. Mmoja alikata mguu, mwingine mkono, mwingine kichwa na matiti, na mwingine alichukua sehemu za ndani nje ya tumbo lake. Baada ya nyama kugawanywa, wengine waliipeleka mtoni kuiosha, na wengine walienda moja kwa moja nyumbani kwao. Wakati wote Bwana Jameson alishikilia daftari na penseli mkononi mwake, akitengeneza michoro ya awali ya eneo hilo"
Ingawa inaelezwa kuwa baadaye alikuja kutishwa na hivyo kukikataa kiapo hiko.