Jamhuri Kihwelo (Julio) apata timu DSM

Jamhuri Kihwelo (Julio) apata timu DSM

Mributz

Senior Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
177
Reaction score
527
1681454228828.png

Timu ya Manispaa ya Kinondoni imetangaza kuvunja Benchi lake la Ufundi kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake na kumtangaza Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' kuchukua mikoba ya Thiery Hitimana.

''Bodi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) baada ya kukaa kikao mapema leo asubuhi imeamua kuvunja benchi lote la Ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Thiery Hitimana baada ya kufikia makubaliano kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu msimu huu.''- KMC

Wana Kino Boys hao @kmcfc_official wameongeza kuwa ''Hivyo basi Uongozi umefikia makubaliano na Kocha Jamhuri Kihwelo Julio ambaye atachukua timu akiwa na benchi lake la ufundi.''
 
Timu ya Manispaa ya Kinondoni imetangaza kuvunja Benchi lake la Ufundi kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake na kumtangaza Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' kuchukua mikoba ya Thiery Hitimana..
Ataishia kufukuzwa
 
Nina wasiwasi kama atamaliza hata msimu ujao wote ndani ya hiyo KMC!
 
Back
Top Bottom