Julio nimjuavyo mie ana kinyongo na kuwepo kwa kocha mkuu mzungu Simba ndio maana anaweza kufanya lolote kuhujumu timu. Hata katika moja ya kauli zake wakati akihojiwa baada ya mojawapo ya michezo alisema anasikitishwa sana na baadhi ya waandishi kutokuwathamini makocha wazawa na hukimbilia kwa wazungu kupata information.... Alisema hivi baada ya kocha mzungu kuuchuna kuzungumzia kipigo kimojapo cha timu hiyo na waandishi kumgeukia Julio.
Julio ni kocha mwenye mafanikio makubwa na Simba na mara nyingi inapotokea ukata au timu kufanya vibaya mara nyingi viongozi na wanachama humwangukia na kumwomba aokoe jahazi. na amekuwa akifanya vyema.... sijui ni kwasababu ya mbinu zake za kiufundi au ni kwa maneno yake ya majigambo pale anapokaribia kukutana na timu fulani, hasa Yanga... na amekuwa akifanya vyema sana. Yanga watafurahia sana kutimuliwa kwa Julio.
Simba walipopata kocha mwingine walipaswa kumweleza Julio na kumweka kando... kwani mafahari wawili hawalali zizi moja. Hili lingeondoa msuguano na kunyosheana vidole kama ilivyo sasa.
Nilipata kuiona Simba katika mechi mbili za Kombe la ubingwa afrika mashariki... Kiwango ilichokionyesha kilikuwa cha juu mno na ni moja ya timu iliyoogopewa sana, si kwa jina lake bali kiwango cha ubora wake. Mojawapo ya mechi hiyo ni ile dhidi ya Tusker ya Kenya. kwahiyo hivi vipigo vinavyoiandama Simba vina sababu nyingine zaidi ya uwezo wa Timu uwanjani. Simba ile si ya kufungwa mfululizo na timu kama Azam au Ruvu JKT. Wachezaji ni walewale, na klabu ni ileile, kuna kitu... na kuondoka kwa Julio kunaweza kuwa ni Suluhisho pia.