Leo ni kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania bara ambapo mnyama simba atashuka dimbani kuumana na Mtibwa Sugar.
Ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa kipekee kwani Mtibwa wamekuwa wanazikazia timu kubwa za Dar ikiwemo Simba, Azam na Yanga.
Katika mechi iliyopita ambapo Simba walikuwa nyumbani, Mtibwa iliikazia Simba baada ya kuifunga goli la mapema. Goli lililodumu mpaka dk 90. Simba ilifanikiwa kuchomoa kupitia faul iliyopigwa na mshambuliaje wake mahiri Emmanuel Arnold Okwi kutoka Uganda na kufanya mpira kumalizika kwa sare ya 1-1.
Leo mtibwa wapo uwanja wao wa nyumbani Jamhuri Morogoro na wanawakaribisha wekundu hawa wa msimbazi ambao ni vinara wa ligi kuu kwa sasa. Japo mechi iliyopita kati ya Simba na Njombe mji, simba iliibuka na ushindi wa 2-0.
Kitendawili kinabaki, Mnyama huyu mkali kabisa mwituni atafanikiwa kuwararua wakata miwa hawa na kuzitafuna miwa?
View attachment 739131
Kikosi cha Mtibwa Sugar
Benedict Tinoc, Kibwana Shomary, Hassan Mganga, Hassan Isihaka, Dickson Daudi, Shabani Nditi, Salum Kihimbwa, Henry Joseph, Stamil Mbonde, Hassan Dilunga, Ismail Mhesa
Kikosi cha akiba
Shaban Kado, Cassian Ponera, Saleh Khamis, Ally Makarani, Ayoub Semtawa, Haruna Chanongo, Hussein Javu
View attachment 739127
Hiki hapa kikosi kamili cha Simba
Aishi Manula; Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Paul Bukaba, Yusufu Mlipili; Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Nicholas Gyan, Shiza Ramadhani; John Bocco, Emmanuel Okwi
Kikosi cha akiba
Said Nduda, Mohamed Hussein, Haruna Niyonzima, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Rashid Juma, Laudit Mavugo
Wachezaji wameshaingia uwanjani
Muda wowote mpira utaanza
0'Mpira umeanza hapa dimba la Jamhuri.
1'Bocco anafika langoni kwa mtibwa na kutaka kumtoka kipa, hatimaye kipa anautoa mpira nje.
02'Kipa wa mpira yupo chini anagangwa. Kipa wa akiba anapasha
03'Shomari Kapombe anapiga shuti kali, linatoka nje kidogo ya lango
06'Mtibwa wanafanya shambulizi kali kwenye lango la simba ila wanadhibitiwa na mabeki
07'Mtibwa wameamka baada ya kukoswakoswa na simba, wanaishambulia simba
09'Faul inapigwa kuelekea simba
10'Simba sasa wanaliandama lango la mtibwa
14'Mtibwa wanapiga kona ya kwanza.
16'Okwi anapiga shuti kali golini, lakini kipa anaokoa