Jamhuri, Morogoro: Mtibwa FC 0 -1 Simba SC, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara

Jamhuri, Morogoro: Mtibwa FC 0 -1 Simba SC, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara

Mbona Hawa wamevaa suti za kike?
rangi ya lipstick Na maua rose
this-is-simba-jpg.739127
 
Hahahaaa. Bora umenijua Mtani wangu nilitaka kukufuata huko PM.

Ahsante sana nimekaribia rafiki. Nami nilikumiss pia ujue.

Ila leo sijui kama mtatoka Mtani.
Anhaa Mtani Tuombee Dua Basi Twaweza Toka Mtani,

Inabidi Umuombee Mema Mwenzio Unajua..

Nilikuwa Nakuona Ona Ila sikuwa Nahakika Kama Niwewe Ndo Nini Kukimbia Ivyo.
 
Leo ni kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania bara ambapo mnyama simba atashuka dimbani kuumana na Mtibwa Sugar.

Ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa kipekee kwani Mtibwa wamekuwa wanazikazia timu kubwa za Dar ikiwemo Simba, Azam na Yanga.

Katika mechi iliyopita ambapo Simba walikuwa nyumbani, Mtibwa iliikazia Simba baada ya kuifunga goli la mapema. Goli lililodumu mpaka dk 90. Simba ilifanikiwa kuchomoa kupitia faul iliyopigwa na mshambuliaje wake mahiri Emmanuel Arnold Okwi kutoka Uganda na kufanya mpira kumalizika kwa sare ya 1-1.

Leo mtibwa wapo uwanja wao wa nyumbani Jamhuri Morogoro na wanawakaribisha wekundu hawa wa msimbazi ambao ni vinara wa ligi kuu kwa sasa. Japo mechi iliyopita kati ya Simba na Njombe mji, simba iliibuka na ushindi wa 2-0.

Kitendawili kinabaki, Mnyama huyu mkali kabisa mwituni atafanikiwa kuwararua wakata miwa hawa na kuzitafuna miwa?

View attachment 739131

Kikosi cha Mtibwa Sugar

Benedict Tinoc, Kibwana Shomary, Hassan Mganga, Hassan Isihaka, Dickson Daudi, Shabani Nditi, Salum Kihimbwa, Henry Joseph, Stamil Mbonde, Hassan Dilunga, Ismail Mhesa

Kikosi cha akiba

Shaban Kado, Cassian Ponera, Saleh Khamis, Ally Makarani, Ayoub Semtawa, Haruna Chanongo, Hussein Javu

View attachment 739127

Hiki hapa kikosi kamili cha Simba
Aishi Manula; Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Paul Bukaba, Yusufu Mlipili; Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Nicholas Gyan, Shiza Ramadhani; John Bocco, Emmanuel Okwi

Kikosi cha akiba
Said Nduda, Mohamed Hussein, Haruna Niyonzima, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Rashid Juma, Laudit Mavugo

Wachezaji wameshaingia uwanjani
Muda wowote mpira utaanza

0'Mpira umeanza hapa dimba la Jamhuri.

1'Bocco anafika langoni kwa mtibwa na kutaka kumtoka kipa, hatimaye kipa anautoa mpira nje.

02'Kipa wa mpira yupo chini anagangwa. Kipa wa akiba anapasha

03'Shomari Kapombe anapiga shuti kali, linatoka nje kidogo ya lango

06'Mtibwa wanafanya shambulizi kali kwenye lango la simba ila wanadhibitiwa na mabeki

07'Mtibwa wameamka baada ya kukoswakoswa na simba, wanaishambulia simba

09'Faul inapigwa kuelekea simba

10'Simba sasa wanaliandama lango la mtibwa

14'Mtibwa wanapiga kona ya kwanza.

16'Okwi anapiga shuti kali golini, lakini kipa anaokoa
tupewe mwendelezo wengine hata tbc taifa wametukatia mitambo na tupo mashamban
 
Anhaa Mtani Tuombee Dua Basi Twaweza Toka Mtani,

Inabidi Umuombee Mema Mwenzio Unajua..

Nilikuwa Nakuona Ona Ila sikuwa Nahakika Kama Niwewe Ndo Nini Kukimbia Ivyo.
Hahaaa. Inabidi nijitahidi Mtani. Hivyo jumatano na wewe utaniombea Dua. Lol.

Ndio mie rafiki. Wacha tu rafiki. Nitakupa mchapo baadae.
 
Hahaaa. Inabidi nijitahidi Mtani. Hivyo jumatano na wewe utaniombea Dua. Lol.

Ndio mie rafiki. Wacha tu rafiki. Nitakupa mchapo baadae.
Usijari Mtani Dua Yangu Utaipata Tuu.
 
Back
Top Bottom