Jamhuri Morogoro: Mtibwa vs Simba hakuna mbabe

Jamhuri Morogoro: Mtibwa vs Simba hakuna mbabe

Msimu huu naona marefa wameamua kutenda haki,mikia mtajuta
Kwani wakati wanasema goli liwe kona, au wanakataa magoli ya azam au walipotoa penati nje ya box na kadi nyekundu dhidi ya kagera mbona mlikuwa hamuongei ila Eymel alipowaambia hamjui mpira mko kama manyani na kubweka kama majibwa mkasema kawatukana kumbe alikuwa anawaambia ukweli
 
Napingana na wanaosema eti uwanja ulikuwa mbovu wakati mwaka jana kwenye uwanja huo huo Simba simba ikiwa na wachezaji hao hao ukimwondoa tu Morison ilishinda goli 3. Wakati huo huo Simbandio kwanza imetoka kushinda kwenye viwanja vibovu mechi tatu mfululizo kuanzia Sumbawanga, Arusha na Mbeya.

Simba imeambulia sare kwa Mtibwa na sababu zifuatazo ndio zilizochangia sare hiyo:-
1. Kosa la Manula kufuata mpira wa krosi bila mahesabu matokeo yake akadaka hewa nyuma ya kichwa mtu badala ya kudaka mpira mbele ya kichwa cha mfungaji. Kwa kipa yoyote mzuri hawezi kuufuata mpira wa krosi bila kuwa na uhakika wa kuupata ni heri mara mia kipa abaki golini asubiri matokeo yoyote kwake kuliko kufanya safari hewani kuufuata mpira ambao hana uhakika wa asilimia 100 kuupata. Na siku zote Manula anafungwa magoli hayo hayo ya krosi lakini cha ajabu ni mzuri mno anapoangaliana na mshambuliaji uso kwa uso kwani hakuna kipa anayemfikia hapa bongo (tazama alivyookoa goli la Jafary Kibaya dakika za mwishpo mwisho). Sijui hayo mapungufu ya Manula kwenye krosi na kona alumiwe nani kati ya Manula au kocha wa makipa Simba kwani ni tatizo la muda mrefu lilikosa suluhisho.
2. Mtibwa lazima wapewe sifa kwani kipindi cha pili chote walicheza vizuri mno kuizidi Simba kiasi Simba walipoteana. Muda mwingi walilikamata dimba la kati na kuwapoteza viungo wa kati wa Simba ambao ni bora kabisa kwenye ligi yetu. Hongera kwake kocha Katwila.
3. Wachezaji wa Simba walionekana wamechoka hasa kipindi cha pili na hii inaweza kuwa imetokana na kucheza mfulullizo hata baada ya ligi kuisha tofauti na timu nyingine ukiacha Namungo. Hapa kocha kwa kuwa ana kikosi kipana anapaswa awaamini na wachezaji wengine ambao hawajacheza ila waingie taratibu kwenye kikosi huku akiwapumzisha mmoja mmoja wale ambao wamecheza mfululizo kuanzia ligi iliyoisha, FA na Ngao ya jamii.
4. Safu ya ushambuliaji ya Simba inabidi kocha wao aingalie kwa jicho la tatu. Kama washambuliaji wa Simba wangekuwa makini mechi dhidi ya Mtibwa ingekwisha ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza. Kukosa kwao magoli mengi ya wazi kipindi cha kwanza ndio kuliwajengea Mtibwa kujiamini sana na kutawala kipindi chote cha pili kiasi na wao Mtibwa wangeongeza umakini kidogo hakika mnyama alikuwa anakufa kifo cha aibu pale Jamhuri - Morogoro.

Yote kwa yote Simba inabidi wajipange sana kama wanataka kutetea ubingwa wao kwani ligi ya mwaka imeonyesha toka mwanzo sio ya mchezo mchezo kila timu inakaza kweli kweli.
 
LIVE KUTOKA KAWE, TAMASHA LA WAFANYAKAZI NA WAFANYABIASHARA- BONIPHACE MWAMPOSA
LIVE KUTOKA BIAFRA. UZINDUZI WA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE KWA TICKET YA CCM ABBAS TARIMBA.
LIVE KUTOKA GHETTO, KUNA BINTI ANAPATA MIMBA ITAKAYOKATALIWA
Mimba itayokataliwa zipo nyingi,na zinazochoropolewa ni nyingi tu.

Live kutoka Chato, MAGUFULI anasaini mara ya pili ttena ujenzi wa bomba la mafuta, yaani atasaini mara ya tatu
 
Back
Top Bottom