Maswali yangu ni haya?
1. Hivi hizi zinaweza kuongozwa na ilani tatu tofauti za uchaguzi kwa pamoja? maana huo uwezekano upo.
2. Serikali ya Muungano itapata wapi fedha za kuendesha Serikali yake pale ambapo let say upande mmoja utakapo amua kufuta ushuru wa bidhaa aidha kutokana na mikataba ya forodha ya regional bodies kama EAC, SADC, COMESA, EC ili kuruhusu ushindani wa soko wa bidhaa kati ya nchi hizo?
3. Kama Elimu haitokuwa ni jambo la muungano kama ilivyo sasa lakini angalau kuna namna fulani ya kushahabiana kwa sasa hivi,litakuwa Taifa gani moja kama haliunganishwi na mfumo mmoja wa Elimu? Maana kupitia elimu iliyoratibiwa kwa pamoja ndipo unaweza kujenga Taifa moja. Kuna watu watasema mbona hata sasa hivi kuna shule tofauti na systms tofauti lakini angalau kuna jitihada za kuhakikisha yale masomo maalumu yanafundishwa hata ikiwa kwa kichina, kiingereza au kiswahili.
4. Hivi lets say upande mmoja wa muungano utakapoimarika kiuchumi labda kutokana na kutokana na sera za ilani ya uchaguzi ya chama tofauti au kuwa na mangira mazuri ya kiuchumi ya kiasili hivi serikali hii ya muungano ya chama tofauti ambayo haisimamii mambo ya uchumi pande zote mbili itaweza kuleta uwiano wa kiuchumi au kuleta mpango mahsusi wa kunusuru upande mwingine wakati haina mamlaka ya mambo ya uchumi?