Jamhuri ya Kiislam ya Iran

Mkuu umeongelea hapo kuhusu nonArab Muslims. Kuna yule shehe mkuu wa wahabia anawaita non-Arab Mslims mbwa kwasababu tu kusilimu kwao kulitokana na upanga siyo hiari yao.
 

Mi sioni wanachokifuata saudia kufuata uislamu kisawasawa,sababu mwaka huu wanawake saudia wameruhusiwa kuendesha magari,kumiliki account bank nakadhalika umekichukuliaje hili mkuu.
Allah ni mjuzi zaidi yetu.
 
Mi sioni wanachokifuata saudia kufuata uislamu kisawasawa,sababu mwaka huu wanawake saudia wameruhusiwa kuendesha magari,kumiliki account bank nakadhalika umekichukuliaje hili mkuu.
Allah ni mjuzi zaidi yetu.
Dini ya uislaam ndio inasema wanawake wasiendeshe magari?[emoji22] wasifungue account?
 
Wasunni wakose usingizi kisa washia sasa bro Kwani mtu akiwa mshia haendi kuhiji makka? Kama anaenda sasa athari ya kiuchumi kwenye hao mahujaji iwapi ikiwa hata washia nao huenda kuhijia makka?

Mtu akiwa mshia anaenda kuhijj makka na atafanya umra makka pia sasa athari kwa saudia hapo n"nini?
 
achana naye huyo anaijua Iran kwenye radio na TV Aki advance sana kwenye vijiwe vya kahawa na Google...
hapo atakuwa anakupiga mikwara tu..
angekuwa mjuaji angeenda direct
hahahaa
 
Kinachowakera US kwamba Iran wanaishi maisha yao hawataki kufuatilia matakwa ya kidunia na sheria za UN kitu anbacho pia US wanagombana na NK i.e North Korea
fact ...
 
Haya mambo ya kidini yanahitaji elim tena elim ya dini kwelikweli. Hiyo qur'an na sunnah yenyewe inavyofundishwa na ushia ni tofauti na inavyofundishwa na wasunni. Vyovyote utavyosoma ni eidha iwe unasoma kishia au kisunni au kiahmadiyya au kiquraniyyun au vipi. Mtume hakuwa na dhehebu hii haina maana eti wewe hauna dhehebu. Mtume anasema tuswali kama yeye anavyosali je mtume aliswali vipi? Hapo utakuta wasunni wanayonamna yao na washia pia na madhehebu mengine pia na wote wanaclaim hivi ndivyo aliswali mtume, wewe unafuata ipia hapo? Utakuta hiyo namna yako uliyosomeshwa kwamba mtume aliswali hivi kwa wenzako wamefundishwa kinyume na wameambiwwa hivi ndivyo aliswali mtume.

Katika uislamu unlike christianity madhehebu yanatokana na eidha tofauti za kiitikadi au tafauti za kifiqihi. Tofauti za kiitikadi ndio hizi zinazoleta ushia, usunni uahmadiyya nk nk wkt tofauti za kifiqihi ni ndogo nazo zinagawanya hizi madhehebu kubwa pia. Mfano katika usunni kuna madhehebu nne zinazotokana na tofauti za kifiqihi.

Hapa inabidi elim kidogo ambayo mm sina kuweza kujua inakuwaje waislamu wa sasa wana madhehebu na hali ya kuwa mtume hakuwa nayo. Nafkiri kwa uchache wa uwezo wangu niishie hapa
 
Mkuu inaonesha huna hata moja unalolijua katika uislam, jaribu kusoma na kufanya utafiti ili uwajue hao mashia na vilevile hao wanaoipinga bakwata sio kwa dhehebu kama unavyodhani ni matendo yao hao bakwata ndo kinachofanya hao bakwata watu wasiwakubali.
 
Fact
 
Kwani Ushia sio Uislamu mkuu!?..
Halafu chanzo gani ulichonacho wewe kinasema Iran sio Jamhuri ya Kiislamu mbona mie kupitia Google inaniambia Iran ni Jamhuri ya Kiislamu!.
 
Aiseee " huwaga na waambia watu kuhusu hili lakini wanapinga " nawaambiaga kuwa hamuoni kwamba mmetengenezewa mikakati " yakuiona saudia kama nchi tukufu ili muende kudhuru halafu wao wapate kuongeza pato la taifa kupitia nyinyi " lakini ajabu huwa wananipinga
 
Kwani Ushia sio Uislamu mkuu!?..
Halafu chanzo gani ulichonacho wewe kinasema Iran sio Jamhuri ya Kiislamu mbona mie kupitia Google inaniambia Iran ni Jamhuri ya Kiislamu!.
Google sio chanzo maridhawa hasa ukikosa wapi pakupata habari sahihi.

Unajua kuna vitu huwa vinategemeana,yaani kimoja hakisimami bila ya kingine.

Irani nasema sio jamhuri ya kiislamu kutokana na itikadi na mienendo ya muasisi wa taifa hilo.

Muasisi wa taifa hilo ni mshia na Irani iko chini ya Ushia.

Sasa kama Ushia sio uislamu iweje taifa liwe la kiislamu ? Na kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho ni yule kiongozi wamuitae wa kidini,wa sasa ni Ali Khamenei.

Bro google huwa ina faida ukijua wapi pakupata ukweli kupitia google,mathalani sisi huwa tunaitumia google kama njia,tukishapata marejeo tunayatafuta marejeo hayo kwenye sehemu husika,namaanisha vitabuni tena sio soft copy bali tunanunua nakala zenyewe za kushikika,elimu iko vitabuni.

Sijajua kama wewe ni muislamu au la,kama ni muislamu naweza nikakueleza kutokana na upeo wako ili kufikia nukta unayoitaka kwa haraka.

Kama sio muislamu bali unataka kujifunza na kuujua ukweli,safari yako kidogo itakuwa ndefu na nitatakiwa kwenda wewe taratibu ili nikate kiu yako.

Kwa hapa kwanza tosheka na machache haya.
 
Jambo hili halipo wala halitakuja kuwepo. Saudia ni jina jipya halikuwepo kabla na mipaka inajulikana kijiografia na utukufu wa miji inajulikana tangu na tangu.

Mashia wana hila asikwambie mtu.

Kwetu sisi utukufu hauletwi kwa kura za veto wala vikao vya watu kadhaa wala kwa tume au jopo la watu wa chache,utukufu wa jambo,mtu,kitu au miji kwa maana ya mahali ni kwa ufunuo kutoka kwa Allah aliyejuu na mtume wake amani ya Allah imfikie.

Bro wa kuidhuru saudia kwa hakika hakuna na hatoweza hata wakuifitini.

Nakuuliza swali,hivi ushawahi kusikia saudia kumepiganwa vita ?

Hii ziada nakupa huwezi kuujua ukweli wa mambo kupitia vyombo vya habari hasa haya mataifa wala kupitia makala za wana habari. Kwa sababu kuna ukweli huwa unataka muda kuujua,yaani kutenga muda na kusoma hasa.
 
Kwani Google inasehemu wanapoandika yenyewe si inaniletea machapisho yote kuhusu nachotaka!.. Mfano mimi nikiuliza kuhusu Uislamu wa Shia na Sunni ikanipa maelezo yote toka origin halafu na wewe ukaja ukasema una maandiko tofauti nikakuuliza umeyapata wapi ukasema mtandaoni si itabidi tuanze kuverify sites ulizotembelea kwa kulinganisha na zangu!.
Tuanzie hapa Wewe ulipopata majibu google ukatafuta wapi hiyo 'kweli'?.. Sababu Shia vs Sunni kihistoria ni Tawi moja lililokataa kukubaliana kuhusu mambo fulani kama ilivyo Roman Catholic vs Orthodox Church!..
Halafu wewe ni nani kukataa Irani sio Islam State wakati Internationally inatambulika hivyo!?.. Sometimes mambo yenu ya migogoro ya kidini muibakize mkikutana misikitini, mkija huku nje mpiganie kitu kimoja.
 
aisee kweli imani imewajaa
 
Mi sioni wanachokifuata saudia kufuata uislamu kisawasawa,sababu mwaka huu wanawake saudia wameruhusiwa kuendesha magari,kumiliki account bank nakadhalika umekichukuliaje hili mkuu.
Allah ni mjuzi zaidi yetu.
Bro hili liko wazi sana,nakupa kanuni siku zote wafalme wanapoingia katika miji huwa wanaiharibu isipokuwa wale wachache ambao wana dini.

Taifa la saudia linatawaliwa kifalme,kwanza inabidi ujue ufalme sio haramu wala sio dhambi.

Watawala hawa wana madhaifu yao hili linajulikana ila ukilinganisha na mataifa mengine ya kiislamu Saudia wanafata sheria ya uislamu hasa kuliko mengine.

Hilo la kuhusu wanawake kuruhusiwa kuendesha magari nimelisikia sana ila sikulifatilia kiundani,kama nikiamua kulifatilia,lazima nianze kutafuta majibu ya maswali haya :

1. Je uislamu unasemaje juu ya mwanamke kuendesha vipando ?

2. Kama wameruhusiwa,je hakuna taratibu walizowekewa ambazo hazitaleta muingiliano na wanaume na kuondoa stara ya wanawake ?

Sijui kwanza wewe mwenzangu maswali haya umejiuliza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…