Mnakosea sana kumfananisha Rais wetu na hao wengine.hapa kwetu mkuu hata awe mkali vipi au awe na mapungufu vipi lakini baada ya kipindi cha miaka kumi hupisha na kumuachia mwingine,hii ni tabia ya kuigwa na mataifa mengine yenye viongozi wanao ng'ang'ania madaraka,nionapo mTanzania anajaribu kudharau hili binafsi namchukulia siyo mTanzania au ni mTanzania mwenye shida kifikla.mtu anadharau tulichonacho ilihali mataifa jirani na mengine ya mbali ukienda unawasikia wakiisema vizuri Tanzania.tuna shida ya kuponda sana kilicho chetu chema na kusifia kilicho cha watu kibaya na kukigeuza kua ndiyo chema,kisa tu mapenzi ya vyama.tubadilike na tuwe wazalendo.Rais wa awamu ya 3 alikua mkali pia kama huyu wa awamu ya 5,lakini kipindi chake kilipoisha alipisha kwa amani kabisa na kumpa kijiti mkuu mwingine,lakini mtu anajaribu kufananisha na viongozi wa nchi nyingine ambao ni wababe na hawataki kutoka Ikulu,mtu anajua kabisa lakini anajifyatua akili na kusema maneno kana kwamba wanaosoma alichoandika ni hawana akili.tupende nchi yetu,tupende na kuwaombea viongozi wetu na tuache mihemko isiyo na maana wala faida.
JAH RASTAFARI MORNING AFRICA