Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Serikali huru ya Tanganyika (hii iko wapi?)
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuna umuhimu mkubwa kuanza kuuhoji muungano huu. Kuna kitu kilikosewa ama kilisahauliwa kwa makusudi na kamwe hakijawahi kuhojiwa popote!
Kwanza lazima tukubaliane hakuna uhuru wa Tanzania bali kuna uhuru wa Tanganyika.. Maana tuliungana tayari Tanganyika ikiwa huru
Baada ya muungano/muunganiko wa mataifa haya mawili nchi huru ya Tanganyika na nchi huru ya Zanzibar kukazaliwa taifa liitwalo TANZANIA.. Kwa maana ya kwamba serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zilikufa rasmi na kuundwa serikali moja ya Tanzania iko wapi hii?
Hili kosa kubwa na la wazi ndio linatusumbua mpaka leo hii baada ya muungano wa haya mataifa mawili, taifa la Zanzibar likabaki na utambulisho wake kama taifa, lakini taifa la Tanganyika likaukana utambulisho wake asilia
Kwa taifa la Zanzibar kubaki na utambulisho wake kama taifa kukawapa nguvu ya kuunda serikali yao inayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kwa kuukana utambulisho wake asilia kama taifa, serikali ya Tanganyika ikakosa nguvu ya kuunda serikali yake ambayo ingeitwa serikali huru ya Tanganyika
Kilichotokea ninini sasa badala ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika kukawa na serikali ya jamhuri ya Tanzania ambayo kwayo ni sehemu ya muungano. Serikali ndio chombo cha kiutawala kinachoendesha nchi
Zanzibar ana faida mbili tayari ndani ya muungano
1. Utambulisho wake upo
2. Ana serikali yake
Kwa hiyo linapokuja swala la kuamua mambo yake ya ndani kiutawala.. Zanzibar ina chombo chake huru cha kufanya hivyo. Na linapokuja swala la kuamua mambo ya muungano ipo serikali ya Jamhuri ya muungano
Hapo ndipo Tanganyika alipopigwa bao la kisigino kwenye huu muungano.. Ndio maana leo hii watu wa Zanzibar wanaweza kuvuka maji na kuja kuwa viongozi Tanganyika kwa kofia ya muungano lakini mtanganyika kamwe hawezi kuvuka maji na kwenda kuwa kiongozi kule!
Muungano ni mzuri, kuungana kuna faida nyingi, USA ni muungano wa majimbo, UAE ni muungano wamajimbo pia.. Tunaziona faida za kuungana.. Lakini ni lazima uwe ni muunganiko wenye mizania sawa..
Suala la dpw litutoe sasa kwenye hii ganzi tuliyopigwa itutoke tuwe na mwanzo mpya sasa hasa kwenye huu muungano. Tungekuwa na utambulisho wetu wa Tanganyika ina maana tungekuwa na serikali yetu huru na hili suala la bandari lisingeamuliwa na serikali ya Muungano na kutufikisha hapa tulipofikia
Tuurejee mkataba wa muungano upya! Utambulisho wa Tanganyika uwepo ili tupate nguvu ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika... Tukiliacha tena hili...TUTAHUKUMIWA NA WAKATI
= > Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958
= > Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?
= >
www.jamiiforums.com
= > Yajue mambo 22 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

ZAIDI UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
= > Lipo wapi tatizo kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tafakari!= > Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na Muungano wa Siria na Ejibti walioungana 1958
= > Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?
= >
Muungano wetu ulikuwa wa kubadilisha jina kutoka Tanganyika kuwa Tanzania kwani Zanzibar ipo vile vile ila Tanganyika haipo
Wadau MUUNGANO wetu ni Wa Nchi 2 Tanganyika na Zanzibar. Matokeo ya MUUNGANO huu yakaizaa Nchi ya TANZANIA. Jambo la AJABU NCHI ya ZANZIBAR imeendelea kuwepo licha ya kuungana na Tanganyika lakini Nchi ya TANGANYIKA HAIPO Swali Kwanini Tanganyika ilipotea Bali Zanzibar ipo? Kama Serikali ya...