Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Just take good note of this: tarehe 26 April 1964 Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tarehe 29 Oktoba 1964 jina la nchi likabadilishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ilikubalika tangu awali Zanzibar ibakie na uhuru mkubwa wa kujitawala (autonomy) ndani ya Muungano.

Swali kubwa: ni nani alikuwa mhandisi wa muungano huo na lengo lake kuu lilikuwa lipi hasa? Bila kusahau muungano wa kisiasa wa 5 Februari 1977 uliounganisha TANU na ASP kuunda CCM. Hakuna kinachotokea hivi hivi tu na wananchi pande zote za muungano hawakushirikishwa. Hakukuwa na referendum. Walikusanywa kushangilia tu.

Just take good note of this: tarehe 26 April 1964 Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tarehe 29 Oktoba 1964 jina la nchi likabadilishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ilikubalika tangu awali Zanzibar ibakie na uhuru mkubwa wa kujitawala (autonomy) ndani ya Muungano.

Swali kubwa: ni nani alikuwa mhandisi wa muungano huo na lengo lake kuu lilikuwa lipi hasa? Bila kusahau muungano wa kisiasa wa 5 Februari 1977 uliounganisha TANU na ASP kuunda CCM. Hakuna kinachotokea hivi hivi tu na wananchi pande zote za muungano hawakushirikishwa. Hakukuwa na referendum. Walikusanywa kushangilia tu.

Ilikubalika tangu awali Zanzibar ibakie na uhuru mkubwa wa kujitawala (autonomy) ndani ya Muungano.[emoji3064]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani Mshana yuko sahihi

TANU na ASP ziliungana 1977 ikazaliwa CCM

Baada ya hapo ndio Zanzibar ikaanza kuchachamaa kudai Mamlaka kamili, tunawakumbuka Akina Jumbe, Faki, Maalim Seif na sasa Othman Masoud

Jiulizeni, Mamlaka Kamili ni nini?

Watakapopata Mamlaka Kamili ndipo Mshana jr ataipata hiyo Tanganyika!
Kwahiyo kama Sheikh Abeid Karume akifufuka Leo anajua chama kinachoongoza Zanzibar ni ASP !
 
Kwa sababu Marais waislam ni wabinafsi na wanakuwa wanapendelea Waislam wenzao wa Zanzibar.
Hiyo ni hofu tu ya wagalatia tu!
Waislamu hawajawahi kuwa na upendeleo kwa sababu wanapoingia madarakani hutawala huku wakiogopa sana jicho la kanisa.
Ukiangalia idadi ya viongozi wa serikali na taasisi zake zote tangu uhuru kwa awamu zote sita wakristo ni zaidi ya 60% bila kujali kuwa rais ni muislamu au ni mgalatia.
 
Mshana anatoa hoja kwamba kuna baadhi ya vitu zanzibar inajiamulia kama nchi na ina serikali yake lkn Tanganyika haina!! Yaan Tanganyika inategemea serikali ya Muungano. Ndio maana akatoa na mifano ya baadhi ya mamlaka mfn TRA(ZRA), TPA(ZPA) etc. Sasa wew wapi umeona anapiga vita dini ya uislam????
Kabla ya hapo Wana rais na huku bara Kuna rais , Wana Baraza la wawakilishi, na huku bara Kuna bunge, Wana bendera , na huku bara Kuna bendera.... Kuna vitu vingi tu amabavyo wanavyo na huku vipo kwahiyo hapo hakuna jipya. Ilivyokuwa rais wa Zanzibar anasimamia mambo ya Zanzibar ambayo siyo ya muungano huku rais wa muungano akiangalia mambo ya muungano basi taasisi zilizopo Zanzibar ni hivyohivyo zipo kwa ajili ya mambo Maalumu ya wazanzibari ambayo siyo ya muungano. Kama vile ndani ya wizara ya afya na wizara ya elimu Kuna mambo Maalumu yanashughulikiwa na wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI )kwahiyo utakuta hospitali na shule iliyopo kwenye wilaya yako inapata bajeti na miongozo Toka wizara ya afya (muungano) na TAMISEMI (siyo ya muungano) nimeeleza hivi kama mfano tu wa mambo ya muungano na Yale ya Zanzibar ambayo siyo ya muungano.
 
Kuna kitu waislam mmekuja nacho sio kizuri kabsa. Sasa ivi kiongozi mweny kusadikika ana imani ya kiislam akikosolewa kdg tu ata kama kweli kakosea nyie hamuoni kosa lake mnakuja na milio mingi kusema kisa ni Muislm dah acheni hii tabia italeta hatari kubwa sana.
Maneno ya William Lukuvi aliyoyasema kanisani wakati wa mjadala wa Zanzibar ni nchi au siyo nchi mnayakimbuka au hamkuyasikia au mnajifanya kuyasahau ??!!
 
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Serikali huru ya Tanganyika (hii iko wapi?)
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuna umuhimu mkubwa kuanza kuuhoji muungano huu. Kuna kitu kilikosewa ama kilisahauliwa kwa makusudi na kamwe hakijawahi kuhojiwa popote!

Kwanza lazima tukubaliane hakuna uhuru wa Tanzania bali kuna uhuru wa Tanganyika.. Maana tuliungana tayari Tanganyika ikiwa huru

Baada ya muungano/muunganiko wa mataifa haya mawili nchi huru ya Tanganyika na nchi huru ya Zanzibar kukazaliwa taifa liitwalo TANZANIA.. Kwa maana ya kwamba serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zilikufa rasmi na kuundwa serikali moja ya Tanzania iko wapi hii?

Hili kosa kubwa na la wazi ndio linatusumbua mpaka leo hii
Baada ya muungano wa haya mataifa mawili, taifa la Zanzibar likabaki na utambulisho wake kama taifa, lakini taifa la Tanganyika likaukana utambulisho wake asilia

Kwa taifa la Zanzibar kubaki na utambulisho wake kama taifa kukawapa nguvu ya kuunda serikali yao inayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Kwa kuukana utambulisho wake asilia kama taifa, serikali ya Tanganyika ikakosa nguvu ya kuunda serikali yake ambayo ingeitwa serikali huru ya Tanganyika

Kilichotokea ninini sasa badala ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika kukawa na serikali ya jamhuri ya Tanzania ambayo kwayo ni sehemu ya muungano..
Serikali ndio chombo cha kiutawala kinachoendesha nchi

Zanzibar ana faida mbili tayari ndani ya muungano
1. Utambulisho wake upo
2. Ana serikali yake
Kwa hiyo linapokuja swala la kuamua mambo yake ya ndani kiutawala.. Zanzibar ina chombo chake huru cha kufanya hivyo. Na linapokuja swala la kuamua mambo ya muungano ipo serikali ya Jamhuri ya muungano

Hapo ndipo Tanganyika alipopigwa bao la kisigino kwenye huu muungano.. Ndio maana leo hii watu wa Zanzibar wanaweza kuvuka maji na kuja kuwa viongozi Tanganyika kwa kofia ya muungano lakini mtanganyika kamwe hawezi kuvuka maji na kwenda kuwa kiongozi kule!

Muungano ni mzuri, kuungana kuna faida nyingi, USA ni muungano wa majimbo, UAE ni muungano wamajimbo pia.. Tunaziona faida za kuungana.. Lakini ni lazima uwe ni muunganiko wenye mizania sawa..
Suala la dpw litutoe sasa kwenye hii ganzi tuliyopigwa itutoke tuwe na mwanzo mpya sasa hasa kwenye huu muungano. Tungekuwa na utambulisho wetu wa Tanganyika ina maana tungekuwa na serikali yetu huru na hili suala la bandari lisingeamuliwa na serikali ya Muungano na kutufikisha hapa tulipofikia

Tuurejee mkataba wa muungano upya! Utambulisho wa Tanganyika uwepo ili tupate nguvu ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika... Tukiliacha tena hili...TUTAHUKUMIWA NA WAKATI

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact
 
Mnakumbuka zile harakat za kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili 2013 kama sikosei zilikja zikiendshwa na mashehe waliounda umoja wao wakaupa jina uwamsho kule Zanzibar kupelekea mpaka wale mashehe kufungwa miaka 9 gerezan kwa ajili ya kuidai Zanzibar yenye mamlaka kamili ?

Wanachi walikua na muamko mkubwa mpaka kufikia kuandamana bila ya hofu yoyote Imagine toka miaka iyo wazanzibar walikuwa na uwelewa juu ya huu muungano na bado walikua hawautaki wakaupinga wazi wazi.

Ninachotaka kusema ni ivi kuipata Tanganyika sio rahisi kama mnavyodhania. Kwanza mkianzisha harakat kama za kule Zanzibar kuidai Tangayika mtapewa kesi ya uhaini. Ila kuidai Zanzibar yenye mamlaka kamili sio uhaini
 
b20612b409c6ef730aa8a699a8f2e4e8.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom