Jamhuri ya Wadiya: Taifa la Afrika lisilotambulika

Jamhuri ya Wadiya: Taifa la Afrika lisilotambulika

Singidan

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
881
Reaction score
942
Ukitazama filamu iitwayo “The Dictator” iliyoingia sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2012 (sasa inapatikana katika mtandao wa Netflix na Youtube) utabaini kuwa kuna taifa barani Afrika linaloitwa Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya, maarufu kwa jina la Wadiya. Ni filamu iliyoigizwa katika nchi mbili tofauti, Uingereza na Marekani. Jina Wadiya pia ni jina la mji mmoja nchini Sri Lanka. Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya ni taifa ambalo halijulikani kimataifa kama ilivyo kwa jamhuri ya Dar El Kuti huko Afrika ya Kati.

Katika ramani unaweza kushangaa ni namna gani tafifa hilo limekaa. Pengine ni kama kikundi cha WhatsApp tu kilichounda dola yake na kujitangazia utaifa. Kulingana na filamu ya “The Dictator” eneo la taifa la Wadiya linalandana na eneo la taifa la Eritrea. Inaelezwa kwamba linapakana na Sudan, Djiboiti na Ethiopia.

Kwa mujibu wa mtandao wa taifa hilo, ni kwamba limekuwepo tangu zaidi ya miaka 200 iliyopita. Taifa hilo liliundwa katika maeneo ambayo sasa ni sehemu ya taifa la Sudan upande wa mashariki. Mwaka 1039 bwana Abrahamadeen alianzisha Ufalme wa Wadiya katika eneo tajwa hapo juu. Mwaka 1,187 taifa la Wadiya lilitwaa maeneo ya Kenya, Yemen, na Oman na kuunda himaya ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki.

Mwaka 1708 taifa hilo liliundwa upya kwa jina hilo hilo chini ya Mfalme Abrahamadeen. Mwaka mmoja baadaye vikazuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita hivyo vilidumu kwa muda wa miaka 7, yaani 1709 hadi 1716. Matokeo ya vita hivyo ni kunyang’anywa kiti mfalme aliyekuwepo na kuanzisha utawala wa kidemokrasia na kuundwa kwa Jamhuri ya Wadiya badala ya Ufalme wa Wadiya.

Jamhuri ya Wadiya ilisonga mbele kiutawala kama ilivyokuwa kwa Jamhuri ya Dar El Kuti. Jamhuri ya Wadiya ilidumu kwa muda wa miaka 127 kabla haijapokonywa mamlaka yake na taifa la Ufaransa. Hivyo, mwaka 1833 Jamhuri ya Wadiya ikawa koloni la Ufaransa. Wadiya ilipoachana utawala wa kifalme iliunda Jamhuri ya Kwanza ya Wadiya. Baada ya miaka 62 ya kutawaliwa na Ufaransa na kisha kupata uhuru mwaka 1896, ikaitwa Jamhuri ya Pili ya Wadiya. Hapo ikajidhatiti kuwa taifa tajiri barani Afrika na mshariki ya kati. Abdul Abrahamadeen alikuwa ni mtoto wa mwasisi wa taifa hilo, Mzee Abrahamadeen. Abdul aliona dalili za wazi kuwa Jamhuri ya Wadiya inakwenda kuwa tajiri sana, hivyo akanuia kuwa kiongozi wa taifa hilo ili apate utajiri.

Mwaka 1919, Abdul Abrahamadeen alianzisha chama cha RPIW (Royal Party of Imperial Wadiya) akiwa na lengo la kurudisha utawala wa kifalme ili adumu madarakani. Wakati wa uchaguzi wa mwaka 1921 chama chake kilishika nafasi ya 9 kwa kuwa na viti viwili pekee ukumbini, huku yeye mwenyewe kama mgombea wa kiti cha kuwa raia namba moja (Rais) katika taifa hilo akishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 11.98 ya kula zote zilizopogwa.

Kawaida ya mapenzi ya madara, mwenye penzi na madaraka akiamua kupenda basi anaweza kufanya lolote atakaloona litamsogeza karibu na kiti cha uraia namba moja (Urais) ili kuonyesha ukuu wake. Huenda Abdul Abrahamadeen alikuwa na ushawishi mkubwa jeshini katika taifa hilo. Hivyo, mwaka 1927 alilitumia jeshi hilo kufanya mapinduzi ambayo hayakuwa na ulazima zaidi ya kutamani tu kwenda Ikulu. Katika mapinduzi hayo alifaulu kumuua Rais wa wakati huo mheshimiwa Melan Jabarr. Kisha Abdul Abrahamadeen akaapishwa kuwa Rais mwaka huo huo 1927. Abdul akiwa Rais alitumia sehemu ya artiba zake kufuatilia namna Benito Musolini alivyokuwa akiiongoza Itali. Naye akaanza kufuata njia hizo ili awe dikteta. Pengine ndiyo nia yake kuu ilikuwa hiyo hata kuamaua kumuua Rais Melan Jabarr.

Mwaka 1939, Rais Abdul Abrahamadeen alijiunga na Axis Powers kujifunza udikteta wa Kinazi wa Adolf Hitler. Baada ya kupigwa kwa Axis Powers, serikali ya wadiya ikafanywa kuwa ya kikomunisti chini ya Rais Abdul Abrahamadeen. Lakini alipinduliwa baadye na madaraka kutwaliwa na Rais Ahemd Niarra. Mwaka 1956 taifa la Wadiya likafanywa kuwa la kijamaa, Jamhuri ya Kijamaa ya Wadiya. Ikiwa katika ujamaa ilianguka kiuchumi na kuwa dhaifu.

Madarka yanadumu lakini awaye madarakani hadumu milele. Ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Abdul Abrahamadeen. Aliaga dunia mwaka 1968 akiwa na umri wa miaka 72 nje ya Ikulu. Ni baada ya kuugua homa ya mafua makali. Baada ya mazishi, mawawe mkubwa wa kiume akabadili jina la familia hiyo kutoka Abrahamadeen na kuwa Aladeen ili naye apate kukumbukwa. Baada ya kifo cha Rais Abdul Abrahamadeen, yalitangazwa maomboleza ya mwaka mmoja.

Mwaka 1969, Jamhuri ya Wadiya ikaingia vitani dhidi ya Sudan. Matokeo ya vita hivyo ni kwamba Jamhuri ya Kikomunisti ya Wadiya ilishindwa na ikapoteza mpaka wake upande ambao sasa ni mashariki ya Sudan.
Rais mpya wa wakati huo (baada ya Abdul Abrahamadeen) mheshimiwa Omar Aladeen (baada ya Ahmed Niarra) alibadili mfumo wa taifa lake na kuachana na ukomunisti. Inaelezwa kwamba Omar Aladeen alipenda mno matajiri kuliko wafanyakazi wa kawaida.

Mwaka 1975 nchi hiyo ikaitwa Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya, na Omar Aladeen akawa Rais tena baada ya kushindwa kuunda upinzani feki, na kaka yake Tamir Aladeen akawa mshauri mkuu wa Rais. Wawili hawa wanakumbukwa kwa utawala wao wa kibabe na usiofuata haki za binadamu ipaswavyo. Huenda hiyo ilikuwa ni kudhihirisha jina la taifa lenyewe yaani Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya. Zama hizo taifa likaingia katika umaskini zaidi.

Madaraka yatadumu lakini awaye madarakani hatadumu kamwe. Mwaka 1992, Rais Omar Aladeen alifariki kutokana na tatizo la sratani. Madaktari walisema, Rais huyo alipata saratani kutokana na uvutaji mkubwa wa sigara. Alikuwa akivuta sigara nyingi kwa siku. Tamir Aladeen alikuwa mwenye tamaa ya mali kulingana na vyanzo mbalimbali vya taarifa za taifa hilo. Baada ya kusimamia ujenzi wa Ikulu mpya ya Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya yenye eneo la ukubwa wa kilometa 3 za mraba, alikuwa na mali nyingi huku raia wakiteseka kwa njaa na hasa watoto kushambuliwa na utapiamlo.

Kama kawaida ya baadhi ya matiaf ya Ulaya kuingilia mambo ya mataifa ya Afrika, baada ya kuona Hafez anatawala kwa mabavu kupita kiasi, uliitishwa uchaguzi maalumu ili kupata kiongozi ambaye atakuwa na huruma kwa raia wake. Matokeo ya uchaguzi yalimpa ushindi Hafez Aladeen wa silimia 99.99 ya kura zote! Kwa muibu wa matandao wa fandom.com kutoakana na sheria kali kama Korea Kaskazini, Jamhuri ya Wadiya ikawa na mahusiano yasiyoridha na mataifa mengine na hivyo kukosa wawekezaji.

Mwaka 2012 Haffaz Aladeen alitangaza kuwa taifa lake lina vinu kadhaa vya silaha za nyuklia. Hapo umoja wa mataifa ukaipanga NATO kuishambulia Jamhuri ya Kidikteta ya Wadiya. Ili kulinda usalama wa raia wake, Aladeen akaenda kuhutubia Marekani kuwa ataachana na udikteta na kisha kuunda serikali ya kidemokrasia na kuandika katiba mpya. Siku tano baadaye, Aladeen alimsweka mjomba wake Tamir gerezani akimtuhumu kuwa ni haini, kisha akaandik katiba mpya ya kimekrasia. Uchaguzi ulipofanyika akashinda kwa asilimia 99.98 ya kura zote.

Vyovyote vyombo vya habari visemavyo kuhusu Jamhuri ya Wadiya, Aladeen aliamini kwamba watu wote ni sawa. Inaelezwa kwamba katika utawala wake, Jamhuri ya Wadiya imekuwa kivutio kikubwa cha utalii barani Afrika.

Jamhuri ya Wadiya ina vivutio vingi vya utalii vikiwemo sanamu kubwa ya dhahabu ya Abrahamadeen yenye umri wa miaka 1017. Ikulu ya Jamhuri wa Wadiya ni Ikulu kubwa zaidi katika eneo kuliko Ikulu zote duniani. Ina ukubwa ambao ni sawa na viwanja 198 vya mpira wa miguu. Chumba cha Rais kina eneo la ukubwa wa meta 1,000 za mraba. Baaada ya kutangaza kuacha udikteta, Aladeen akawa Rais na pia Waziri mkuu yeye mwenyewe. Taifa la Eritrea lilisema kwamba eneo lote la Wadiya ni lake tangu mwaka 1991 lakini suala hilo halina nguvu.

Kutokana na udogo waktika eneo. Uchumi wa Jamhuri ya Wadiya ni kama unamilikiwa na Aladeen. Aladeen ana madaraka makubwa sana. Jamhuri ya Wadiya inatumia hele ya dhahabu kwa mujibu wa mtandao wa fandom.com.

Sehemu kubwa ya nchi hiyo ni jangwa linaloitwa Aladeen. Eneo hilo limekuwa maarufu kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali. Nchi ambayo haikuwa na miti ya kutosha, lakini imejitahidi kupanda miti na kugeuza eneo fulani la jangwa kuwa mbuga. Moja ya vipimo vya metriki katika nchi hiyo ni kipimo kiitwscho Aladeen. Meta 1 ya mraba ni sawa na Aladeen 1.5 za mraba. Miji mikubwa ni Wadiya City, Aladeenia, Omariland, Haffazland na Abdul City.

Kwa ujumla taifa hilo halitambuliki licha ya kuwa na watu wake. Ni taifa ambalo ni kama vile kikundi cha WhatsApp tu.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Gurdian, katika makala iliyoandikwa 29 Novemba 2015 na Nick Middleton, anaeleza kwanzz kisa cha visiwa vya Seborga kutojulikana kama sehemu ya Italia tangu mwaka 1079. Ni suala la miaka mingi iliyopita na hivyo watu wake kutojulikana ni wa taifa gani. Taiwan ilikuwa mwanachama wa umoja wa mataifa mpaka ilipojitoa mwaka 1971, Israel ni mwanacham wa umoja wa mataifa tangu mwaka 1949 lakini kuna nchi zaidi ya 30 hazitambui uwepo wa taifa la Israel.

Nick anasema kuwa kupatikana au kutambulika kwa nchi siyo kitu rahisi inagwa jibu rahisi zaidi kuliko yote ni kwamba lazima iwe inatambulika na umoja wa mataifa. Lakini hiyo haitoshi.

Vitabu vingi hueleza kuwa ili nchi iwe nchi halali ni lazima iwe na nguvu za kuunda serikali na kuwa na eneo lake lenye mipaka inayoeleweka. Lakini kwa sababu tu kwamba mataifa fulani yanakataa kukutambua haimaanishi kuwa haupo. Waulize watu wa Israel, Taiwan na Seborga. Ni kama taifa la Mapuche lilikuwa na utawala wake kwa miaka 10,000 huko Amerika ya Kusini. Leo ni sehemu za Chile na Argrntina. Seborga na Mapuche ni maeneo yasiyotambulika kama mataifa lakini yapo. Hivyo Jamhuri ya Wadiya imeonyeshwa zaidi katika filamu kama kumbukumbu. Pengine ndiyo sababu kwamba Jamhuri ya Wadiya kutotambulika kama ilivyo kwa Somaliland aman Puntland.

Credit: Kizito Mpangala.

Je, umewahi kusikia chochote kuhusu Jamhuri ya Wadiya?
Kama unafahamu chochote kuhusu taifa hili,tufahamishane Hapa chini....!!
 
Kiongozi wake niko hapa[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Siyo mchezo!!! lkn Mkuu kuna mataifa mengi tu hayajulikani kama Equatorial guinea na wana hela ya mafuta hao si mchezo, Sao tome and principe, st. Hellena!! Kingdom of Lesotho, Re-Union, Bermuda,

kwa hiyo haya hiyo wahadiya siyo ajabuuu!!! ajabu nyengine sasa siku nasafiri kwenda Lesotho Afisa uhamiaji hakuijua kabisaa hiyo nchi, anauliza ndiyo wapi huko? hadi alipoangalia Ramani! kwa maelezo yangu jamani!!! yule jamaa ni mburula bin Maimuna Khaa! tena nchi mwana chama wa SADACC? Waarabu tu ndiyo hawaijui Israel, Egypt aliikiri hadharani.
 
Back
Top Bottom