Jamhuri ya Woga

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Ninapoangalia yaliyowafanya vijana wa Uganda kuamua kujitolea muhanga kutaka mabadiliko, mengi ni yale yale yanayoendelea Tanzania: vijana kutokuwa na fursa, dhuluma ifanywayo na vyombo vya ulinzi, sheria kubanwa kwa uhuru wa kusema, uzuiaji wa mabadiliko ya siasa ya amani. ughali usiolezeka wa Maisha, Ufisadi na rushwa.

Lakini inakuwaje vijana wa Uganda wameyaona hayo na kuamua 'kuirudisha' nchi yao- na kabla yake WaKenya, Zambia nk; lakini jambo hilo linaonekana kuwa gumu Tanzania?

Nimekuja na nadharia:
Kwanza, ni ukweli lugha ya Kiswahili, hata kama naipenda, imetufanya tuwe 'docile'. Hii ni kwa vile lugha ni utamaduni. Utamaduni wa Mswahili ni 'kuvumilia' na kusema, 'hewalla yakhe'. Hilo limetuathiri kinafsia kwa kiasi kikubwa sana, na wala siyo eti uwepo wa amani.

Pili: Kutokana na 'kunyimwa' uelewa wa Kiingereza, tumejijengea kisiwa, kiasi ambacho uelewa nje ya kisiwa hicho ni wa watu wachache sana. Wengi hawajui hata yanayoendelea nchi jirani! Hii inafanya vigumu kwa watu wengi kuathirika na 'experiences' za wengine na kubakia kuimba wimbo mmoja tu!

Tatu: Tunatawaliwa na Chama cha watu 'smart sana' (in a bad sense) kwamba wanajua udhaifu wa Watanzania na wanajua vizuri kupima 'joto' lao. Kiasi kwamba kila joto linapopanda kupita kiasi wanalegeza kibano. Siyo kama ilivyokuwa vyama vya jirani zetu.
Lakini sababu kubwa Zaidi ni 'elimu'. Kwa kweli sasa naamini kuzoroteshwa kwa elimu Tanzania ni kwa kusudi kabisa. Mtu asiye elimu ni rahisi sana kumtawala kwani atakubali tu unayomwambia, kwa vile hajui kingine bora.

Mtu mjinga ni mwoga.
 
Bila kuiondoa ccm tutaendelea kuishi maisha ya kubahatisha miaka yoote
 
Mbowe chama kimetoka kuwa na wabunge 100 mpaka Mbunge mmoja lakini bavichaaa wako kimyaaaa
Naona unalazimisha kuolewa na mh Mbowe, ila tambua kuwa mh Mbowe ni tayari ana ndoa yake.
 
Mimi concern yangu Kwako ni ndogo sana tu Ndugu je, katika hii Jamhuri ya Watanzania Waoga Wewe pia tupo wote au labda ulishajitoa tayari?
 
Hapo uganda kwa kuwa bwana yule elienda kamsaidia ili ashinde lakini kwa kweli nilichoona kule huenda atapinduliwa tuu ni suala la mda rusubirie tuone.

Naomba niishie hapo
 
Mbowe chama kimetoka kuwa na wabunge 100 mpaka Mbunge mmoja lakini bavichaaa wako kimyaaaa
Hivi huwezi jenga hoja bila ya kumtaja mtu Fulani na chama chake?
Mpaka mnapoozesha mijadala yenge positive contribution.
 
Chadema ndio mazezeta mbowe tangu mwaka 2003 enzi za Mkapa ni mwenyekiti hana jipya kwa sasa anaganga njaa tu,aachie damu changa ameshaexpire.
 
Kwa akili yako Kama upo sahihi kwel unataka kuruka mkojo na kukanyaga......, Fanya analysis Nan anaweza fanya changes unazozitaka, chama kipi kinaweza fanya changes unazozitaka,maana chama kikuu cha upinzan Tz (CDM) hakina sifa yoyote inayohitajika kufanya mabadriko Tz, hakina Maendeleo tuu ndan ya chama licha ya kupata ruzuku na ufadhil mbalmbal, hakina uwaz, sijawah ona mapato na matumiz yake yakiwekwa waz, rushwa ndo kwao coz Mzee lowasa sidhan Kama aliingiaga hvhv Slaa akapigwa chin wakat alikuw kaleta challenge ya ukwel, mwisho kabisa, mnataka serikal uongoz ubadrike na chama chenu tuu kina utawala was kifalme( kurithishana) NB: ukitaka kuelewa hii kaa neutral bila kushabikia chama chochote na tumia logic rahis tuu utaelewa nachomaanisha na rudia tena
 
Mmoja wa punguani waliokosa elimu.Utawaza nn zaidi ya hayo.
 
Vijana wa kizazi hiki tz kiukweli tu waoga sana , haya yanayoendelea sasa mfanosakata la Heslb zaman watu wako road
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…