Jamhuri ya Woga

Jamhuri ya Woga

Ninapoangalia yaliyowafanya vijana wa Uganda kuamua kujitolea muhanga kutaka mabadiliko, mengi ni yale yale yanayoendelea Tanzania: vijana kutokuwa na fursa, dhuluma ifanywayo na vyombo vya ulinzi, sheria kubanwa kwa uhuru wa kusema, uzuiaji wa mabadiliko ya siasa ya amani. ughali usiolezeka wa Maisha, Ufisadi na rushwa.

Lakini inakuwaje vijana wa Uganda wameyaona hayo na kuamua 'kuirudisha' nchi yao- na kabla yake WaKenya, Zambia nk; lakini jambo hilo linaonekana kuwa gumu Tanzania?

Nimekuja na nadharia:
Kwanza, ni ukweli lugha ya Kiswahili, hata kama naipenda, imetufanya tuwe 'docile'. Hii ni kwa vile lugha ni utamaduni. Utamaduni wa Mswahili ni 'kuvumilia' na kusema, 'hewalla yakhe'. Hilo limetuathiri kinafsia kwa kiasi kikubwa sana, na wala siyo eti uwepo wa amani.

Pili: Kutokana na 'kunyimwa' uelewa wa Kiingereza, tumejijengea kisiwa, kiasi ambacho uelewa nje ya kisiwa hicho ni wa watu wachache sana. Wengi hawajui hata yanayoendelea nchi jirani! Hii inafanya vigumu kwa watu wengi kuathirika na 'experiences' za wengine na kubakia kuimba wimbo mmoja tu!

Tatu: Tunatawaliwa na Chama cha watu 'smart sana' (in a bad sense) kwamba wanajua udhaifu wa Watanzania na wanajua vizuri kupima 'joto' lao. Kiasi kwamba kila joto linapopanda kupita kiasi wanalegeza kibano. Siyo kama ilivyokuwa vyama vya jirani zetu.
Lakini sababu kubwa Zaidi ni 'elimu'. Kwa kweli sasa naamini kuzoroteshwa kwa elimu Tanzania ni kwa kusudi kabisa. Mtu asiye elimu ni rahisi sana kumtawala kwani atakubali tu unayomwambia, kwa vile hajui kingine bora.

Mtu mjinga ni mwoga.
Mkuu nazan hujazuiwa kuingia barabarani..kama ww ni mwamba na unapenda mabadiliko ingia bas road kisha watakufuata hao vijana
 
Kwa akili yako Kama upo sahihi kwel unataka kuruka mkojo na kukanyaga......, Fanya analysis Nan anaweza fanya changes unazozitaka, chama kipi kinaweza fanya changes unazozitaka,maana chama kikuu cha upinzan Tz (CDM) hakina sifa yoyote inayohitajika kufanya mabadriko Tz, hakina Maendeleo tuu ndan ya chama licha ya kupata ruzuku na ufadhil mbalmbal, hakina uwaz, sijawah ona mapato na matumiz yake yakiwekwa waz, rushwa ndo kwao coz Mzee lowasa sidhan Kama aliingiaga hvhv Slaa akapigwa chin wakat alikuw kaleta challenge ya ukwel, mwisho kabisa, mnataka serikal uongoz ubadrike na chama chenu tuu kina utawala was kifalme( kurithishana) NB: ukitaka kuelewa hii kaa neutral bila kushabikia chama chochote na tumia logic rahis tuu utaelewa nachomaanisha na rudia tena
Chama ovu unaona chenyewe kinaweza.
 
Mkuu nazan hujazuiwa kuingia barabarani..kama ww ni mwamba na unapenda mabadiliko ingia bas road kisha watakufuata hao vijana
Ulichofanya ni kuthibitisha nadharia yangu: 'elimu'
 
Back
Top Bottom