Jamii Forums kwanini tusimwombe Profesa Shivji awe anatufundisha sheria kwa lugha ya Kiswahili hapa jukwaani?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Najua Prof. Shivji ni mwalimu wa sheria hapo school of Law.

Sina hakika kama huwa anapata muda wa kuielezea au kufundisha sheria kwa lugha ya kiswahili.

Mimi kiukweli baada ya kutoa somo lake la sheria ya umiliki wa ardhi kwa lugha ya kiswahili nimejikuta nakua mpya kabisa kichwani kuliko nilivyokua nakalili kwa lugha ya kiingereza.

Sasa mimi ninachoomba Jamii Forum ingemwomba hata awe anatuandikia nyuzi za mambo ya sheria kwa kiswahili ili wengine tupate kuelewa. Mimi nipo tayari kujifunza kwa lugha yetu ya kiswahili

Mfano: Itapendeza sana akitufundisha hizi sheria kwa lugha ya kiswahili.

1. Sheria ya madini.
2. Sheria mafuta na gesi.
3. Sheria ya mazingira.
4. Sheria biashara.
5. Sheria ya familia.
6. Sheria ya kodi

Nawasilisha.
Ahsante.
 
Unahisi amebobea ktk maeneo hayo yote? Fatilia kwanza kabobea wapi ndio akufundishe eneo hilo.
Sina hakika Ila walau anaweza kutafsiri hizo sheria ndugu kwa kiswahili. Tutajisomea wenyewe walau tupate mwanga zaidi.
 
Unahisi amebobea ktk maeneo hayo yote? Fatilia kwanza kabobea wapi ndio akufundishe eneo hilo.
SIDHANI KAMA TUNAHITAJI MBOBEZI KATIKA HILI, TUNACHOKIHITAJI NI ELEMENTARY KNOWLEDGE TU. TUJUE ABC YA SHERIA TUWE NA PA KUANZIA KUTAFUTA/KUTETEA HAKI ZETU
 
Mkuu umenena vyema sana. Mfano mimi kuhusu sheria ya ardhi saivi mtu haniambii kitu kabisa. Hata nikisimama mahakamani nafungua na document kabisa naanza kuvichakata vifungu.
 
SIDHANI KAMA TUNAHITAJI MBOBEZI KATIKA HILI, TUNACHOKIHITAJI NI ELEMENTARY KNOWLEDGE TU. TUJUE ABC YA SHERIA TUWE NA PA KUANZIA KUTAFUTA/KUTETEA HAKI ZETU
Unahisi utampata? By the way hairuhusiwi kufanya hivyo kwa mujibu wa code of conducts za ma advocates unless uwe na kibali maalum toka TLS cha kutoa hiyo elimu bure.
 
Wengine watalichukulia kama mtu anajitangaza kijanja kwa kujifanya anatoa elimu kwa jamii na kujitangaza kwa mawakili hairuhusiwi mpendwa.
 
Huu ni ubinafsi wa elimu, kwahiyo watanzania wanakufa na maarifa yao
 
Yaani leo nijitolee kuelimisha maarifa yangu kwa wazalendo wenzangu kw uzalendo mseme hairuhusiwi?
 
Yaani wewe mwenye fani ushindwe kuelewa fani yako mpaka ufundishwe kwa mara ya pili halafu uje utusumbue na sisi tuelewe
 
Najua Prof. Shivji ni mwalimu wa sheria hapo school of Law.

Sina hakika kama huwa anapata muda wa kuielezea au kufundisha sheria kwa lugha ya kiswahili.

Mimi kiukweli baada ya kutoa somo lake la sheria ya umiliki wa ardhi kwa lugha ya kiswahili nimejikuta nakua mpya kabisa kichwani kuliko nilivyokua nakalili kwa lugha ya kiingereza.

Sasa mimi ninachoomba Jamii Forum ingemwomba hata awe anatuandikia nyuzi za mambo ya sheria kwa kiswahili ili wengine tupate kuelewa. Mimi nipo tayari kujifunza kwa lugha yetu ya kiswahili

Mfano: Itapendeza sana akitufundisha hizi sheria kwa lugha ya kiswahili.

1. Sheria ya madini.
2. Sheria mafuta na gesi.
3. Sheria ya mazingira.
4. Sheria biashara.
5. Sheria ya familia.
6. Sheria ya kodi

Nawasilisha.
Ahsante.
Mtafute huko aliko akufundishe mengi.
Si wengine yote tunayajua!
 
Huu ni ubinafsi wa elimu, kwahiyo watanzania wanakufa na maarifa yao
Ndo hivyo mkuu, hata kile kipindi cha ITV cha ijue sheria waliwahi kupigwa biti kuwa ni kujitanganza....titizo lipo kwenye hiyo Etiquette yenyewe ya wanasheria haielezei ni nini kina maanisha matangazo kwa wanasheria ndio maana elimu za kisheria unaona hazitolewi kirahisi rahisi tu.
 
Unahisi utampata? By the way hairuhusiwi kufanya hivyo kwa mujibu wa code of conducts za ma advocates unless uwe na kibali maalum toka TLS cha kutoa hiyo elimu bure.
Nilidhani haina option, kumbe ipo..!
 
Back
Top Bottom