X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
"Nimekuita jamaa yangu kwani hali yangu kama unavyoiona. Rafiki zangu wote wamenikimbia, nimebaki na mama kama unavyoniona ila kumbuka nilikuwa mchezaji mkubwa, naomba jamii inisaidie.
Maisha yameenda kombo kwangu kwa sasa, nahitaji msaada kwani hapa wakati mwingine hata fedha ya kula mtihani. Nakubali kwamba nilikuwa 'supastaa' lakini kwa sasa mambo hayapo vizuri kama unavyomuona mama naye ni mtu wa kuhangaika, iambie jamii inisaidie. Katika maisha kila mtu anakosea, sawa, inawezekana nikawa nimekosea lakini siyo kiasi kikubwa hivyo. Besti andika na hili, vijana wanatakiwa wakumbuke kuna maisha baada ya soka, pia wakumbuke kuna nyumbani kwani maisha yanakwenda kasi.
MAMA ALEX ALIMLILIA MWANAE
"Mwanangu mwenzio kama hali yake unavyoiona anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida kwani kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu ambao ulimuanza muda mrefu lakini hakuweza kupata matibabu. Iambie jamii imsaidie ili aweze kupata fedha za matibabu".
Nukuu ya kiungo wa zamani wa Simba, Christopher Alex Masawe pamoja na mama yake mzazi wakiiomba jamii imsaidie Alex pesa za matibabu siku chache kabla ya kifo chake alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti la Dimba, Ramadhan Hassan.
Marehemu Alex anakumbukwa kwa kupiga penati ya mwisho jijini Cairo, Misri wakati Simba ilipoivua ubingwa wa Afrika klabu ya Zamalek mwaka 2003.