Katika zama hizi za mitandao, kuna kundi la watu wengi wamejigeuza kuwa mabingwa wa kutoa motisha. Huko TikTok, Facebook, YouTube kila kona zimefurika na wasemaji wanaotaka kuwashawishi wengine kwa nguvu, lakini wamekosa adabu moja ya msingi:
kusikiliza.
View attachment 3574600
Leo, mtu anaweza kukushambulia kwa muda mrefu akijaribu kukuthibitishia kuwa hakuna Mungu kabsa, lakini anapokutana na hoja yako ya imani, anakatisha mazungumzo na kukimbia. Huu si uhodari wa kutoa hoja yake, bali ni
ugonjwa wa kisaikolojia unaoitwa
‘kutovumiliana kwa mawazo kinzani’.
View attachment 3574601
Watu hawa wana dalili za ugonjwa wa uwazimu:
kujiona ndio wajuaji pekee muda wote. Wanadhani kusema kwa sauti kubwa au kurudia maneno kwa ukali kutawafanya wawe na ushawishi. Lakini wanasahamu kuwa hata wanafalsafa kama
Aristotle na
Plato, kabla ya kuwashawishi watu, walikubali kuketi kitako, kusikiliza na kuthamini maoni tofauti. Hilo ndilo alama ya msingi ya mtu mwenye akili timamu.
View attachment 3574603
Mtu anayekataa kusikiliza maoni yako kuhusu uweza wa Mungu, halafu anadai kukuthibitishia kuwa Mungu hayupo, huyu si mwenye hoja, bali ni mtu anayesumbuliwa na
kiburi cha kisaikolojia. Anajiona kama mungu mdogo duniani mwenye mamlaka kamili, anayeweza kubadilisha ukweli kwa maneno yake tu.
View attachment 3574604
Wapo pia wanaozungumzja kuhusu mifumo ya dunia: anaweza kulalamika kwamba kila kitu kimevunjika, lakini akikataa kuthamini mambo madogo madogo yanayofanya kazi vizuri (kama jua linachomoza, maji yanayotiririka, au mtu akiwa na furah), basi wewe ni mgonjwa kama mgonjwa mwingine.
View attachment 3574605
Ugonjwa huu unaitwa
‘kutokuwa na uwezo wa kuthamini na kusikiliza kabla ya kujibu’. Matibabu yake ni rahisi: kaa kimya, funga mdomo, nyamaza, sikiliza, fahamu kuwa wengine wana ukweli wao, kisha ndipo jadiliana kwa heshima. Vinginevyo, jamii yetu itajaa watu wenye wazimu wa kusema bila kusikia, na wataendelea kulazimisha watu wabadilike ili wafurahie.
View attachment 3574606
Nyie inspirational speaker: kabla ya kuwashawishi wengine, fungua nafsi yako kwanza. ACHA KUWA MUCH KNOW, UTAHARIBU MKUU.