SoC02 Jamii ina uelewa kuhusu matumizi ya kondomu?

SoC02 Jamii ina uelewa kuhusu matumizi ya kondomu?

Stories of Change - 2022 Competition

Angina

Senior Member
Joined
May 13, 2018
Posts
142
Reaction score
137
KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke kwa lengo lakuzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI.

Kondomu ilitambulika miaka mingi na ilkuwa moja ya njia ambayo watu walikuwa wanatumia Kama njia ya uzazi wa mpango. Hadi kufikia 1960 ambapo vidonge vya majira viligundulika hivyo matumizi yake yalipungua kidogo tofauti na awali.

Matumizi sahihi ya kondomu ya kiume aukike hujumuisha uvaaji wa kondomu kwa usahihi kabla ya kuingiliana kimwili mpaka wakati wa mshindo au kupiga goli na kisha kuvua na kuvaa nyingine kama mnaendelea na ngono.

Matumizi yasiyo sahihi ya kondomu hupunguza ufanisi wake na kuleta hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, VVU na mimba zisizotarajiwa.

JE, KONDOMU NI SALAMA
Tafiti znasema kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haiwezi ruhusu upitishaji wa vitu.

Lakini tafiti znaonesha kondomu in uwezo wa kupitisha mbegu za kiume hivyo kusababisha mimba.Wakati wa sex kunakuwa na misuguano mingi ambayo huwa sababu ya kudhoofisha kondomu.

Hivyo kondomu hazina uwezo wa kuzui upitaji wa mbegu za kiume japo swala hili sio la mara kwa mara.

Upana wa kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni makroni
0.1.Maana yake mbegu za kiume ni kubwa mara hamsini ukilinganisha na kirusi cha ukimwi.
Vile vile tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.Hivyo kondomu haiwez kuzuia kwa asilimia mia moja virusi vya ukimwi.

Baadhi ya njia ambazo sio sahihi kwa matumizi ya kondomu
Kuvaa kondomu baada ya kuingiliana sehem za siri hata kama hamjafika mshindo.

Kuvaa kondomu nusu bila kufika adi mwisho wa uume.

Kutumia vilainishi vya mafuta.

Matumizi sahihi ya kondomu

Zingatia yafuatayo kabla hujaanza tumia kondomu

Angalia kondomu kwa umakini ili uhakikishe ya kwamba kondomu haija expire kutoboka , kupasuka au kuharibika

Usitumie kondomu uliyoihifadhi kwenye mfuko wa suruali wa nyuma, waleti au sehemu ya kuwekea glovu kwenye gari

Kondomu isihifadhiwe sehemu yenye joto kali, mwanga mkali sana wa jua au mgandamizo.

Namna ya kuvaa kondomu kwa usahihi

Hakikisha uume umesimama vizuri

Fungua kondomu yako kwa kutumia mikono miwili.

kata kwa makini pembezoni mwa kasha la kondomu kuwa makini usije haribu kondomu.Na usitumie vitu vyanye ncha Kali wakati unachana iyo kondomu.

Minya chuchu ya kondomu yako kwa nje kisha iweke kwenye uume uliosimama na usiikunjue kondomu Kama bado hujaiweka kwenye uume na kunjua taratibu kondomu adi mwisho wa uume wako.

Hakikisha hautumii mikono yako yote kushusha kondomu maana itapunguza mafuta ambayo ni kilainishi.Na hakikisha unaachia nafasi kidogo mbele ya uume lengo ni kukusanya shahawa.

Sasa uko tayar kutumia kondomu na unapofik mshindo toa kondomu uume ukiwa bado umesimama.

FAIDA ZA KUTUMIA KONDOMU

1. Kondomu ni Kama Kinga ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono mfano UKIMWI ,kaswende ,kisonono na UTI
2. Kondomu haina gharama sana ni rahisi Sana kupatikana na kwa bei rahisi

3. Kondomu huongeza Radha ya tendo la ndoa

4. Kwa asilimia kubwa kondomu ina uwezo wa kuzuia mimbo hivyo yaweza tumika katika mpangilio wa mimba na uzazi wa mpango

UDHAIFU WA KONDOMU

1. Udhaifu wa kiufundi
Kondomu zaweza kuzuia kwa kiwango fulani mambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.

Kondomu huaribika tafiti zinasema ubora wa kondomu hupungua siku ad sku.Mtu anaetumia kondomu baada ya miaka 2 au zaid tangu imezalishwa kiwandani yupo katika hatari zaidi kuliko yule anaetumia mda mfupi baada ya kondomu kuzalishwa .Na baadhi ya tafiti znasema kiwango cha kondomu kupasuka kinaongezeka kutoka 3.6% kwa kondomu ambazo hazijatumika adi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka 2 au tatu baada ya kuzalishwa.

2. Udhaifu katika matumizi.

Matumizi mabaya yaaani kutovaa vizuri, kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.

Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi. Pia kutokana na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi na wakati mwingine kondomu hubakia ndani ya uke wa mwanamke.

Kutumia kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.

Lengo la mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi, anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia vizuri ili mwenzake ambaye anaamini hajaambukizwa aweze kuambukizwa .

3. Udhaifu wa kimazingira

Vyombo vya usafirishaji na usalama wa vyombo hivyo;

Kondomu zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na kiwango hafifu katika ubora wake.

Udhaifu wa sehemu ya kuhifadhi kondomu pamoja na vyombo vya kuhifadhia.

4. Baadhi ya watu hupata mzio au aleji baada ya kutumia kondomu.Hii hupelekea kuvimba na kuwashwa sehemu za siri.Na baadhi wanasema watumiapo kondomu hawapati raha yoyote.
 
Upvote 14
Kwa hiyo kuna wana wanapiga mlege hadi kwenye kuvaa condom, mamæ dunia simama nishuke[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]
Eeeh Kaka watu wanapiga mirege[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mnanichanganya sentesi zinapingana
Hizo ni tafiti kumbuka tafiti znatofautiana kutoka eneo moja adi lingine

Na Kuna point nmesema ubora wa kondomu unapungua kadiri unavochelewa kuitumia tangu imezalishwa
 
Kuna mtaalamu humu alisema mafuta mgando yaweza kutumika kama mbadala wa helmet kwa mtu aliyekosa kabisa hicho kifaa, hii ina ukweli wowote?
 
mafuta mgando yaweza kutumika kama mbadala wa helmet
Haishauriwi mkuu

Hua kuna lubes maalum za hayo masuala au kwa kiswahili virainishi sio mafuta mgando au mafuta ya maji maana uke hauiingii chochote tu ni km mdomo wako
 
Kuna mtaalamu humu alisema mafuta mgando yaweza kutumika kama mbadala wa helmet kwa mtu aliyekosa kabisa hicho kifaa, hii ina ukweli wowote?
Hapana sio sahihi na usije thubutu kuyatumia
 
Haishauriwi mkuu

Hua kuna lubes maalum za hayo masuala au kwa kiswahili virainishi sio mafuta mgando au mafuta ya maji maana uke hauiingii chochote tu ni km mdomo wako
Kweli kbsa Kaka nakuunga mkkono kwa hilo
 
Back
Top Bottom