Jamii inayopendelea kukaa kwenye kelele, hasa za muziki, huwa na ufikiri finyu na dumavu

Jamii inayopendelea kukaa kwenye kelele, hasa za muziki, huwa na ufikiri finyu na dumavu

Vibe la kelele nakuwa nalo ijuma asee. bila kelele sielewi elewi sawasawa
 
Mimi tangia zamani sio tu kelele hata MTU anayeongea Sana ananiboa napenda kumsikiliza MTU DR Mpango

Muziki wa taratibu Kama country music .

Kelele zinaboa Sana hasa ukiwa introvert
Watu hawajali wao wanakutwisha kelele,mimi nyakati hizi nikipita au kukaa kwenye kelele ,usiku nkilala zinarudi zote kichwani
 
Umepatia sana kizazi kipya cha bongofleva za kina necha TMK vs Kina GK east cost. Hawa GenZ ndio wanapenda mikelele kila siku kila saa
Nyimbo zao zilikuwa na ujumbe lakini ukiachana na hizi pevu
 
Kuna mstari mwembamba sana kati ya Kupenda makelele na Umasikini,

Starehe ya tajiri hua ni kupenda utulivu na starehe ya masikini hua ni kupenda makelele.
Yan hata nikiwa kwenye basi lenye mziki mkubwa huwa nachukia sana,ninapenda sana utulivu huenda nikawa tajir ajaye inshaAllah

Hata prince Charles alisubir ufalme for 70's yrs
 
vispika vya masokoni kama Karume ni wendawazimu mtupu, sijui hao wafanyabiashara wanaovifungulia wenyewe wanawezaje kuishi navyo hapo siku nzima siku saba kwa wiki.
 
Kwenye maisha ya nyakati hizi,makelele hasa ya muziki yamekuwa ni kiashiria cha usasa,na kuonesha shangwe. Watu hawapendi tena unyamavu na kufikiri ,kelele zimekuwa ndio kiburudisho ,Jamii ya namna hii kamwe haiwezi kuwa na mawazo pevu kwa mambo kadhaa ya maisha.Muziki wa kelele unatumika kama dawa ya ganzi dhidi ya uchungu wa maisha.

Vijana wakishanunua sabufa,basi ni kufungulia muziki mnene,mpaka mtaa wa pili wanasikia ,duh kwanamna hio hakuna akili zitafanikiwa hapo kuwa na mawazo chanya,kizazi chenye uhaba wa tafakari,maamuzi ya mihemko, chenye upungufu wa kumbukumbu,yote sababu ya kukaa sehemu yenye kelele!.

Ukimya umegeuka kuwa adui wa watu.Mojawapo ya athari kubwa za utamaduni huu wa kelele ni kupungua kwa nafasi ya kutafakari.Fikra zimekuwa za haraka kama muziki unaowapigia kelele usiku kucha.

Wasanii wa muziki wenye kelele kubwa wanapewa nafasi zaidi kuliko walimu, wanafalsafa, na wanataaluma.Tunaishi katika kipindi ambapo mtu anasikilizwa si kwa sababu ya hekima yake, bali kwa ukubwa wa spika yake. Jamii inazidi kuwa kipofu wa fikra, huku ikipiga makofi kwa ujinga unaotolewa kwa mapambo ya burudani.mazingira haya yanaua nidhamu ya akili. Mtu anayelelewa katika kelele hutegemea msisimko wa nje ili aendelee kuishi.

Burudani inapochukua nafasi ya tafakuri, ndipo ujinga hupandwa na kuota mizizi.
Hii ni fact , kuna kaukweli ambacho hakijathibitishwa kitaalamu, high IQ huwezi kuwakuta maeneo yenye makelele, na ukiwakuta basi kwasababu wamelazimika kwa sababu kuna tukio linalowalazimu kuwa pale
 
Mh! mkuu nimeelewa ulichoandika japo haujaingia ndani zaidi kwa mwengine anaweza kuanza hata kuchukia muziki kwa huu uzi wako maana umekazia pale uliposema "hasa kelele za muziki!".

Muziki haupo kwaajili ya kelele isipokuwa tu ni matumizi mabaya ya baadhi ya watu, umeongelea muziki general kitu ambacho si sahihi maana hata wale wanaohubiri nakuweka masipika makubwa nao ni walewale zogo tu mitaani!.

Tukirejelea kwenye muziki hukupaswa kwenda in general sema kuna baadhi ya viashiria ndio huwa inaleta tabu sana!, zaidi zaidi ni haya masingeli yao yamekuja kuchota watu akili hata namna ya uchezaji umekuwa ni wa hovyo!. vilevile hata baadhi ya miziki ya bongo flavour imekuwa ya namna hiyohiyo mi nafikiri kila nyenzo ikitumika mahali sahihi na kwa wakati sahihi haiwezi kuwa shida.

Komenti yangu mimi nakupinga hapo kuweka muziki in general, kwani kupenda aina fulani fulani ya miziki huelezea pia hulka ya mtu sasa na ndio huko ulipotakiwa uende!, ninavyofahamu hata watu ambao walikuwa na IQ kubwa tu walikuwa ni watu wanaopenda muziki mfano Albert Einstein.
Nafikiri ni hapo tu ndio nimeona tofauti ila nje na hapo no problem.

huwezi kuita muziki kama huu ati ni kelele labda utakuwa nashida fulani, kuna tofauti kati ya muziki kuupiga kwa kelele na muziki wenyewe kuwa kelele😂
 
Back
Top Bottom