Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Nimejikuta nikijiuliza swali hili leo baada ya kupokea simu ya shemeji yangu(mke wa rafiki yangu)akiniambia ametengana na mume wake!. . . . . .Swali lenyewe ni kwamba kati ya jamii yetu(ya sasa a.k.a dot com)na ile ya kale(ya wazazi,babu zetu a.k.a mwaka 47) ni jamii ipi ilikua sahihi katika dhana ya ndoa?. . . . . Zamani(Babu DC utanisahihisha hapa kama nitakosea) kijana akitaka kuoa swala la mke mpaka mahari lilikua la wazazi,yaani kijana wa kiume hakuhusika na kutafuta mke wala mahari.Muolewaji nae alikua anaandaliwa kwaajili ya kumheshimu mume TU.Na alikua ni mama wa nyumbani,mlezi wa watoto.Pia ilikua ni aibu mwanamke huyu kuachika.Ila ndoa hizi zilidumu saaaana. . . . . Kwa upande wa sasa ni kinyume chake,kijana anatafuta mke anaemwona anafaa,analipa mahari,harusi kubwa,mwanamke nae hivyo hivyo,halei watoto,watoto wanalelewa na h/girl.Kuachika sasa sio aibu tena!Na ndoa nyingi zinavunjika siku hizi!. . . . . . Swali linakuja ni jamii ipi ilikua sahihi katika dhana nzima ya ndoa?Yaani iliyokua sahihi na lengo la muanzishaji wa ndoa(Mungu)je zamani au sasa?Kama ni sasa kwanini ndoa nyingi zinavunjika?Kama ni zamani,why don't we go back to our fore fathers?