Jamii isipuuze vipaji vya watoto

Jamii isipuuze vipaji vya watoto

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Vipaji vya sanaa mbalimbali watoto huzaliwa navyo, wengine hujifunza kwa kuona kwa watoto wenzao na kuweza kumudu na hatimaye kuwa na uwezo katika sanaa husika. Mara nyingi vipaji vya watoto wetu vimekuwa vikichukuliwa kama sehemu ya michezo ya utotoni na hivyo mtoto kukosa msisitizo wa kuendeleza au kuona kuwa anachofanya kina umuhimu katika maisha yake na ya wengine.

Kwa Jamii zetu za Kiafrika hususani hapa kwetu Tanzania hatuna utamaduni wa kuibua, kuviendeleza na kuvitunza vipaji vya watoto wetu. Tunachukulia ni sehemu ya makuzi au michezo yao watoto na mara nyingine kuwaadhibu kwa kuhisi ni watundu waache kumbe tunawatia hofu na kuwafanya waache na vipaji vyao hufa, lakini kwa mataifa ya wenzetu hasa wa mabara mengine wao huanza kumfatilia mtoto tangu kazaliwa anapendelea kufanya vitu gani ili waweze kutambua uwezo wake na kung'amua kipaji au vipaji alivyonavyo ili waweze kumuendeleza na kukitunza kipaji hicho.

Tabia hii ya kwetu imesababisha kuua vipaji vya watoto wengi sana au kuvidumaza, hii inakuwa tofauti na wenzetu ambao tangu mdogo wakijua ana kipaji cha mpira humuendeleza katika mpira, wakijua anapenda kuimba humuendeleza katika kuimba nk. hivyo mtoto hukua katika sanaa husika na hivyo kuwa bora katika tasnia yake na kuja kuwa nyota baadaye na kulifaa Taifa au yeye mwenyewe.

Wazazi ikiwa umeona mtoto wako anapendelea fani fulani mtie moyo, muwezeshe akiwa bado mdogo ili kukuza sanaa hiyo kwani ni ajira yake, ukiwa na uwezo wa kumpeleka shule ambayo atapata mafunzo yanayohusika na kipaji chake fanya hivyo, na usimzuie mtoto akijiunga na vikundi vya sanaa kama shuleni kwani hiyo itamfanya akue kisanaa.

Fanya hivi kuendeleza kipaji cha mtoto
  • Mtie moyo katika kipaji ulichogundua kwa mtoto. Mf, michezo yake anapendelea kucheza mpira basi mwambie anajua na anaweza kufanya vuzuri akawa mchezaji mkubwa.
  • Muwezeshe kupata vufaa vya michezo au kukutana na watoto wenzake walio na fani moja.
  • Mpeleke shule ya kipaji hicho kama uwezo unaruhusu.
  • Msisitize katika mazoezi kama ya kuimba, ngoma kucheza mpira nk
  • Akiumia katika michezo yake, mtie moyo na kumsaidia kisaikolojia bila kuonesha kuwa huo mchezo ni hatari kwake.
  • Mtafutie mtu wa kumuangalia kama mfano kwake.
 
Maweeeee!! Nafwa mie wazazi wenyewe hawa wabongoooo!!.....bora basi uishi kwa wazazi waelewa!!!! lkn mtu baki utasikia hili toto michezo tuuuuu!!! kutwa nzimaaa!! mbona sie hatukuwa hivo??? tulikuwa na adabu.

yaani watakisema kitoto mpaka kijifie!!...akifail sasa mitihani mawee atasemwa huyooooo!! heee!...bora baba awe msomi! muelewa siyo wale wasomi waliokimbia umande au basi wa division ooo00000ooooooo0000
 
Back
Top Bottom