peter msuku
Member
- Nov 26, 2017
- 7
- 5
JAMII MASKINI KWENYE ARDHI TAJIRI
(MSANGANO MOMBA)
BY
MSUKU PETER
(MSANGANO MOMBA)
BY
MSUKU PETER
UTANGULIZI
Umasikini. Ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile malazi, mavazi na chakula. Lakini pia maji safi na salama, huduma za afya, kutokana na kukosa uwezo wa kununua au kulipia. Hii pia hujulikana kama umasikini ulio kithiri au ufukara.
Umasikini katika jamii. Ni kuwa na raslimali au mapato madogo/machache kulinganisha na mahitaji ya jamii husika. lakini pia kwa kulinganisha na jamii zingine.
Lakini pia, umasikini unaweza kusababishwa na watu katika jamii kushindwa kutumia raslimali zinazowazunguka katika katika jamii ili kuwaletea maendeleo.
RASILIMALI NI NINI
Rasilimali ni kitu chochote ambacho kinaweza kumfanya mtu aweze kupata mabadiliko chanya kuelekea kwenye maendeleo akikitumia ipasavyo.
Kwa mujibu wa kamusi ya oxford inasema Rasilimali ni jumla ya mali alizonazo mtu, shirika,nchi au jamii.
Rasilimali inaweza kua maji, ardhi, wanyama, madini nk.
MSANGANO
Msangano ni moja ya kata zilizopo ndani ya wilaya ya momba mkoa wa songwe, Tanzania. Wakati wa sense ya mwaka 2012 kata ilikuwa na wakazi wapatao 15770. Wenyeji wa kata ya msangano ni kabila la wanyamwanga, na shughuri yao kubwa ni wakulima wa mpunga (zao la biashara), mahindi, mtama, maharagwe, na kwa kiasi kidogo alizeti. Pia hivi karibuni wameanza kulima matikiti maji, pamoja na vitunguu. Ardhi ya msangano ni moja ya ardhi chache zilizobaki na rutba kiasi kwamba wanaweza kulima bila kutumia mbolea yoyote na wakapata mazao. Lakini pia jamii ya kata ya msangano hujishughilisha na ufugaji wa ngombe.
Ndani ya kata ya msangano ambayo wananchi wake ni wakulima zaidi ya asilimia 80 ya wakazi ni masikini, na zaidi ya asilimia 50 wanaishi kwenye umasikini wa kupindukia. Kwani kipatochao hakifiki hata dola moja kwa siku na wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.
MASWALI YA KUJIULIZA.
- Ni kwanini wanachi hawa wanaishi kwenye dimbwi la umasikini wa kupindukia licha ya kubalikiwa kuwa na ardhi yenye rutba na shughuri yao kubwa ni wakulima.
- Kwanini vijiji vya kata ya msangano vinashindwa kumudu kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za kijamii kikamilifu.
- Ni nini mwarobaini wa sababu zinazo fanya jamii hii ibaki nyuma kwenye mambo ya kimaendeleo.
Katika jamii yoyote umasikini huna na chanzo chake, hasa ukifikilia kwanini jamii moja na nyingine zinaweza kutofautiana kimaaendeleo, hivyo ni jambo la msingi kujiuliza kwanini jamii hii inaonyesha kuwa na maendeleo kuliko jamii nyingine. Ukijiuliza hivyo unaweza kupata sababu zilizo nyuma ya maendeleo hayo, au umasikini katika jamii husika. Hivyo zifuatazo ni sababu za kwanini wananchi wa msangano ni masikini.
IMANI POTOFU.
Moja ya kasumba kubwa miongoni wa wananchi wa msangano ni kuamini kwamba bila nguvu za giza huwezi kufanikiwa, hivyo kila mtu anaefanikiwa huanza kuwekewa vikwazo na watu kuanza kujiuliza kamuua nani paka kapata mali. Na huweka mbali juhudi zako hata kama wanakuona unavyohangaika usiku na mchana kutafuta riziki. Pia kunawatu wengi wameshuhudiwa walikua wachapakazi wazuri, wakapata fedha nzuri za kuwakizi mahitaji yao. Lakini badala ya kuhakikisha wanatafuta njia sahihi za kutunza pesa zao wanaanza kuzunguka kwa waganga waweze kuwekewa ulinzi kwenye pesa zao mwisho wasiku wanajikuta wanatumia gharama kubwa kwa waganga, na mwisho wa siku wanajikuta wamefilisika.
MIKOPO ISIYO RASMI.
Moja ya jambo kubwa ambalo linawaingiza wananchi hawa katika umasikini wa kutupwa ni mikopo isiyo rasmi maarufu kama “molosi” kwa kawaida sharia inawataka wakopeshaji wote mikataba yao ipitie tume ya ushindani. Ili kujiridhisha kama inafaa kutumika . lakini mambo ni tofauti ndani ya jamii kwani kunawatu wameibuka na kuleta mikopo ambayo si rafiki kwa wananchi. Kwani riba yake inafika paka asilimia 70 paka 100 kitu ambacho kiukweli ni wizi na hakikubaliki. Rai yangu kwa serikali za mitaa ni kwamba serikali za mitaa ndio ziko karibu na hawa watu, hivyo basi licha ya kusimamia sharia zarikali za mitaa niwalezi. Hivyo waweze kusaidia kudhibiti wizi huu kwani bila kufanya hivyo hatuwezi kujenga jamii inayokua kiuchumi kwani watu wachache wataendelea kuwanyoya walio wengi. Kwa mfano ndani ya kata ya msangano tumeshuhudia kunawatu wamekimbia kijiji kisa mikopo hii isiyo rasmi.
MATUMIZI YA POMBE KUPINDUKIA.
Pombe ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuongoza kwa tuwatia watu katika mazingira ya umasikini wa kupindukia. Ndani ya kata ya msangano pombe ni moja ya starehe chache zinazopatikana kiurahisi hivyo kupelekea wimbi kubwa la watu kujiingiza kwenye matumizi ya pombe. Mbaya ni pale ambapo watu wanashindwa kujizuia kiwango cha pombe wanacho kunywa. Mbaya zaidi huanza kunywa pombe asubuhi paka manane ya usiku. Hawa watu wanatakiwa kufanya kazi ili kujiingizia kipato. Hivyo kuangusha nguvu kazi, na shughuri za uzarishaji kusimama. Napendekeza serikali za vijiji viweze kutunga sharia ndogondogo za ngazi ya vijiji paka kata ili kuzibiti matumizi mabovu ya pombe. Hasa kuhakikisha mda wa kufanya kazi watu wawe kazini ili wajiingizie kipato. Kwani bila hivyo wataendelea kuzalisha maovu mengine. Na jamii za watu hawa kuendelea kuwa masikini.
SHUGURI MOJA YA KIUCHUMI.
Moja ya sababu nyingine kubwa ya kwanini wananchi hawa wako katika umasikini mkubwa ni kuwa na kazi moja tu ya uchumi wao. Na wanafanya kwa msimu mmoja tu kwa mwaka mzima. Kilimo ndo kazi yao kubwa na kwamwaka mzima wanalima kwa msimu mmoja, hivyo wakishavuna wanasubiri tena mwaka ujao. hapa katikati hawana kazi nyingineya kufanya hivyo wanaishi kwa kula matunda ya mavuno. Kwa hali hiyo huwezi kutegemea maendeleo. Ni vyema wananchi hawa wawe na utamaduni wa kuwa na kazi zaidi ya moja. Kwani jinsi unavyokua na vitegauchumi vingi ndivyo unajiongezea nafasi ya kufanikiwa kiuchumi.
KUKOSEKANA KWA NISHATI YA UMEME.
Nijambo lisilopingika kwamba nishati ya umeme ni miongoni mwa nishati muhimu sana kwa dunia ya leo. Umeme umetumika kuajili watu wengi. zaidi ya nishati nyigine yoyote. Paka naandika nakala hii januari 2020 nishati hii muhimu bado haijafika kata ya msangano. Kunauwezekano mkubwa kukosekana kwa nishati ya umeme kukawa ni moja ya sababu kubwa sana ya umasikini katika kati hii. Hivyo ningeshauri serikali iweze kuharakisha mchakato kwa kupeleka umeme vijijini kwani itaweza kusimamisha uchumi wa watu wake kikamilifu.
UBOVU WA BARABARA NA MIUNDOMBINU MINGINE.
Katika uchumi wowote duniani kote, sekta ya usafiki ni moja ya kipaombele kinachoweza kuchochea uchumi uweze kukua kwa kasi. Na ndio mana serikali mbalimbali zinawekeza kwenye sekta ya miundombinu. Kukosekana kwa barabara nzuri kata ya msangano ni moja ya jambo linalopelekea umasikini uzidi kushamili. Kwa mfano. Mtu yuko tayari auze mpunga msangano kwa bei ya hasara kuliko kuupeleka kwenye mashine za kukoboa ambapo ni umbali wa kilomita 60 tu. Kwasababu ya ubovu wa barabara naishauri serikari iweze kufanyia kazi ili kuwapa hauweni wananchi hawa.
UWAJIBIKAJI FINYU WA VIONGOZI.
Moja ya sababuya umasikini pia. ni uwajibikaji finyu wa viongozi ndani ya kata katika maswala ya maendeleo na kuleta maendeleo. Kwa mfano Diwani wa kata ya msangano haishi msangano, huwa anakuwepo msangano pindi akiwa na kazi za kufanya, je mtu huyu anaweza kuwa na uchungu wa kuwasaidia wananchi hawa wanyonge wanaopata shida usiku na mchana. Kama mtetezi wa wananchi waliompigia kura je? Pindi ambapo yuko nje ya kata yake na watu wanahitaji huduma yake kama diwani wanafanyaje.
SIASA ZISIZO NA TIJA.
Chanzo kingine cha umasikini katika jamii hii ni siasa zisizo na tija. Kwa mfano toka uhuru wa Tanganyika na msangano kutambuliwa kama kata, chama kimoja ndo kinanguvu. Na kutokana na hilo, mtu wa chama kingine hata akiwa na hoja nzuri yenye nguvu. basi hawezi kuongea, hivyo wanayafunga mawazo yao na hawaruhusu kupata changamoto mpya ambazo kimsingi zingewasogeza kwenye maendeleo. Mbaya zaidi hata vizazi vinavyofwata wanakua huku wakijua kwamba kuwa chama pinzani ni ushetani.
UFISADI NA KUHUJUMU MALI ZA UMA.
Ni kwa mda mrefu sasa kumekua kuna uhujumu wa mali za uma pamoja na mapato ya vijiji ndani ya kata. Na hii imekua ni utamaduni wa mda mrefu. Kwani historia ya kata hii inaonyesha ufujaji umegundulika mala kazaa lakini wahusika hawachukuliwi hatua yoyote. Pia hata saivu watu wanatumia mapato ya vijiji kujinufaisha wao binafsi. Nimeweza kusoma taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji cha msangano ya mwezi septemba 2019 nilichokiona ni ufisadi mkubwa na kutokana na hilo namtaja bwana simon sichalwe aliekua mwenyekiti wa kijiji kipindi kile na bwana elia silumbwe mtendaji wa kijiji paka sasa. Kua uongozi wao ulijaa ufisadi usio na mfano. Ukipata fursa ya kusoma ripoti iyo utagundua asilimia 20 yamapato yametumika kwenye matumizi yasiyo ya msingi, asilimia 60 zimetumika kulipana posho, na asilimia 20 zilizobaki zimetumika kuendeshea ofisi ya kijiji. kiuhakika huwezi kuwa na matumizi ya namna hii na ukategemea maendeleo haiwezekani.
MFUMO MBOVU WA UWAJIBIKAJI.
Aliyekua rais wa marekani Barack Obama alivyowasili Kenya moja ya maneno yake kwenye hutuba alisema “afrika haihitaji viongozi mashuhuri sana ili kuleta maendeleo, afrika inaitaji mifumo imara” nini maana yake ni kwamba. Lazima kuwe na mfumo wa kuonyesha flani anawajibika kwa furani,(chain of command) nani anatoa amri na nani wa kuitekeleza kila mtu akifanya kazi kwa nafasi yake na kutimiza majukumu yake ipasavyo basi msangano umasikini utakua ni historia.
MIGOGORO MIONGONI MWA VIONGOZI.
Katika taasisi yoyote na jamii yoyote migogoro ni jambo ambalo haliepukiki katika harakati za kutafuta kuweka mambo sawa. Wataalamu wa mambo ya uongozi wanasema siasa za ndani ya taasisi ni kali na mbaya zaidi kuliko siasa za nje. Katika kata ya msangano kumekua na migogoro mingi,sana miongoni mwa viongozi jambo ambalo linadumaza kasi ya maendeleo katika jamii hiyo. Kwa mfano kumekua na kutoelewana kati ya mtendaji wa kata, diwani, wenyeviti wa vijiji,watendaji wa vijiji pamoja na wenyeviti wa vitongoji. Kiasi kwamba wameunda makundi. Mambo kama haya hayawezi kuwafikisha popote.
MWISHO
Kuzaliwa masikini sio sababu ya msingi kukufanya uishi ndani ya umasikini paka mauti. Nawasihi viongozi wa jamii hii ya kuyafanyia kazi mapungufu . na sababu zilizotajwa hapo juu ili kuhakikisha watu wanaweza kuishi vizuri na kutumia rasilimali zinazo wazunguka kuwaletea maendeleo. Kuhakikisha wanajenga misingi ya utawala bora. Na kuweka mbali itikadi za kisiasa panapoitajika kusimamia maslai ya uma.