Kamamaa
Member
- Feb 12, 2010
- 15
- 4
Rushwa. Kila mmoja anapozungumza huona huonekana kama kitu kilichopo mbali sana naye. Mara nyingi inapozungumzwa rushwa inawahusu vigogo au watu walio na nyadhifa katika taasisi mbalimbali.
Inawezekana kuwa sahihi lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanajamii ndio wanaotengeneza viongozi wala rushwa. Kwa mfano unapomchagua kiongozi ambaye ambaye ametoa hongo maana yake mmetengeneza makubaliano kwamba naye atajilipa mbele ya safari.
Hutarajii kiongozi aliyepata madaraka kwa rushwa asiwe mla rushwa. Jamii inatengenezwa mchwa hawa ambao baadaye huwagharimu wenyewe. Wapo baadhi ya viongozi wamewahi kuwakebehi wananchi kuwa uongozi walionao waliununua kwa hiyo watafanya vile wanavyoona itafaa.
Ni mara ngapi umemsikia mwanajamii akimshangaa kiongozi aliyekufa maskini? Ni wengi tu. Hata Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere huzungumzwa kama shujaa kwa kuwa alikuwa alikufa akiwa maskini. Jamii inastaajabishwa kiongozi mwenye wadhifa kufa maskini wakati alikuwa na uwezo wa kufanya chochote ili ajilimbikie mali.
Kwamba Hayati Moringe Sokoine alikuwa na pea mbili za viatu ni habari ya kutisha na kustaajabisha. Inawezekanaje kiongozi akaishi namna hiyo. Hakuna anayejaribu kuufahamu mshahara wa kiongozi huyo ili alinganishe na matokeo anayoyaona katika maisha yake.
Hata pale kiongozi anapoonekana kuzubaa kuchangamkia fursa, wapambe na ‘machawa’ humfunua macho kumuonyesha namna anavyoweza kupiga pesa na kujinufaisha na kuwanufaisha wao pia.
Utii wa kinafiki kwa kiongozi unaofanywa na baadhi ya watu umekuwa ukiwavimbisha vichwa na kuwabadilisha mitazamo ambayo baadae hugeuka kuwa mwiba kwa wanaowaongoza.
Wananchi huwanyenyekea viongozi wakiwafanya kuwa miungu watu na kuwaonyesha kwamba akitoka Muumba kwa uwezo wanaofuata ni wao. Lakini hii yote inakuja kwa sababu waliwapa madaraka hayo kwa nguvu ya rushwa inabidi wajinyenyekezi kwa mabwana wakubwa hao.
Wafanyabiashara hutengeneza mitandao kabisa kwa kuwahonga viongozi ili wajilinde. Kila mra tunasikia wafanyashara wamechangia chama hiki au kile. Kila mmoja hujaribu kujiweka karibu na kiongozi kwa manufaa yake.
Sio kwamba viongozi hawaombi rushwa, lakini mianya mingi ya rushwa hutengenezwa na wanajamii. Kwa mfano wafanya biashara wanapotoa hongo ili waweze kufanya biashara zao kwa namna inavyowapendeza.
Ni mara ngapi Mtanzania husimulia kwa makeke pale anapopata huduma nzuri katika ofisi za umma kama vile hospitali au shuleni?
Sifa humwagiwa nesi au daktari kwa kuwa mnyenyekevu kwa mgonjwa au kuwasikiliza ndugu na jamaa. Daktari huyu atakuwa gumzo, ndugu hawataacha kujichanga wampe chochote kwa kuwa amekuwa mwema kwao.
Jamii ya wala rushwa haikumbuki tena kwamba huduma nzuri inaweza kupatikana bila kutoa chochote. Haiamini tena katika utumishi uliotukuka bila kutoa mlungula. Ndio maana kitendo cha daktari huyu kimewastaajabisha. Haiwezekani lazima apewe chochote.
Ili kukomesha vitendo vya rushwa nchini
Kinachotakiwa kufanya ni kubadili mitazamo ya jamii juu ya haki zao. Wakati huu unasoma hapa kuna mjumbe wa chama fulani nchini anasubiri uchaguzi ufike auze kura yake kwa mgombea.
Kuna mwingine anajiandaa kununua kura za wajumbe wa kata yake ili awe mjumbe wa wilaya nako kwa lengo la kwenda kuuza kura yake kwa anayetaka kuwa mjumbe najiandaa kununua kura za wajumbe wa kata yake ili awe mjumbe wa wilaya nako kwa lengo la kwenda kuuza kura yake kwa anayetaka kuwa mjumbe wa mkoa.
Jamii ieleweshwe kuwa kupata huduma nzuri ni haki yake na anayempa anatimiza wajibu wake na wala si upendeleo kwake.
Madhara ya kuuza kura yaanishwe waziwazi ikiwamo niliyotaja hapo juu kwamba inawanyima haki ya kuwawajibisha viongozi wao.
Kwamba kiongozi anatakiwa kuabudiwa ifundishwe kuwa ni kinyume cha haki zao kwani huyo ni mtumishi wao anapaswa kuwajibika kwao.
Mzizi wa tatizo la rushwa upo kwenye jamii kwa hiyo ili kukabiliana nalo upo umuhimu wa kuwekeza nguvu katika kutoa elimu ya uraia.
Msingi uanze kwa kuwepo somo maalumu la rushwa mashuleni kuanzia madarasa ya awali kabisa. Wanafunzi wafundishwe haki zao na wajibu wao kwa Taifa.
Kutotoa rushwa ni wajibu wao katika ujenzi wa Taifa. Mipango mingi ya maendeleo nchini hukwama kutokana na vitendo vya rushwa, hivyo upo umuhimu wa kuwekeza katika elimu na kuifanya kuwa ajenda ya kitaifa.
Wafundishwe madhara ya kuchagua viongozi watoa rushwa kuwa hutumia muhula wao kujilipa kwa uwekezaji walioufanya kupata kura huku wakiwaacha wananchi wakiendelea kukosa maji, elimu, huduma za afya na nyingine nyingi.
Ni takribani miaka 60 sasa tangu nchi yetu ilipopata uhuru lakini kumekuwa na mkwamo kutokana na viongozi kuwa na fikra zinazofanana. Mimi naamini jamii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya viongozi kuwa hivi.
Janga la rushwa nchini linaweza kukomeshwa na wananchi wala si polisi au mahakama.

Upvote
0