Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Mimi ni Mkristo nisiyeamini katika makanisa na miujiza, maajabu na mazingaombwe.

Ila jana nilienda kusali kwenye kanisa moja nikiwa nimeambatana na rafiki yangu na baba mzazi wa rafiki yangu, huyu mzee anasema kila siku anawaona nduguze waliokufa siku nyingi wanamwita. Na nyakati nyingine amekuwa akiwaona hao wafu wanamuandalia party ya kula nyama mbichi za watu.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu hili kanisa waliambiwa na kiongozi wao kila mtu aendeshe gari lake, atoe mlio wa gari, aweke gia na kupiga honi za mdogo. Elekea kulia, kushoto, mbele, nyuma, kisha nenda nje ya kanisa ukapaki gari yako.

Wakati watu wakiwa busy na ujinga ule, mimi nilikuwa nimekaa kimya nawacheka tu kimoyomoyo.

Mchungaji naye alikuwa busy akizunguka huku na huko akiwagusa watu wake vichwani na kuwaambia gari lako na likadhihirike kwenye ulimwengu wa nyama.

Akiwa kwenye kuzunguka kwake ndipo akanikuta nimekaa sifanyi utaahira ule. Akaniuliza kwanini naleta roho za upinzani kanisani kwake?

Nikamjibu sileti roho ya upinzani, ila siamini kwenye mazingaombwe. Ndipo akawaita walinzi wake, yeye anawaita protocol wanitoe ndani na nisirudi tena mle ndani.

Nikamsikia akiongea kutoka kwenye maspika kuwa shetani amejidhirisha kanisani ili kuzuia muujiza wa watu kupokea magari.

Basi akaambiwa waanze kukemea roho zote za upinzani ambazo zinasababisha wao wasipokee magari yao.

Jamaa zangu nilipotolewa nje nao wakatoka tukarudi nyumbani.

Ndugu zangu watanzania magari hayapatikani hivyo. Utalitolea sadaka na kulipandia sana mbeg u gari lako, hadi ukome.

Waza nje ya boksi, kuwa mbunifu kwenye shughuli zako, boresha huduma zako, jali muda, uwe na matumizi mazuri ya fedha. Nidhamu ya fedha ndiyo itakayokuletea mabadiliko ya tabia zako.
 
Hili kanisa waliambiwa na kiongozi wao kila mtu aendeshe gari lake, atoe mlio wa gari, aweke gia na kupiga honi za mdogo. Elekea kulia, kushoto, mbele, nyuma, kisha nenda nje ya kanisa ukapaki gari yako.[emoji23]

 
Kilichonisukuma kuandika uzi huu hili kanisa waliambiwa na kiongozi wao kila mtu aendeshe gari lake, atoe mlio wa gari, aweke gia na kupiga honi za mdogo. Elekea kulia, kushoto, mbele, nyuma, kisha nenda nje ya kanisa ukapaki gari yako.
😂😂😂 at first nilijua ni magari ukweli kumbe walikua wanaigiza 😂😂😂
 
hili kanisa waliambiwa na kiongozi wao kila mtu aendeshe gari lake, atoe mlio wa gari, aweke gia na kupiga honi za mdogo. Elekea kulia, kushoto, mbele, nyuma, kisha nenda nje ya kanisa ukapaki gari yako.[emoji23]View attachment 2602028
Makanisa yote duniani bila mazingaombwe hakuna kanisa pamoja porojo za abunwasi ukitaka kuamini fatilia maubili yao pia viongozi wa makanisa ni mabingwa wa kupinga biblia,ukichunguza kwa akili ya ufahamu uliopewa na muumba utagundua kuwa makanisa yapo kupingana na biblia wanayo ibeba kwapani kila siku.
 
Makanisa yote duniani bila mazingaombwe hakuna kanisa pamoja porojo za abunwasi ukitaka kuamini fatilia maubili yao pia viongozi wa makanisa ni mabingwa wa kupinga biblia,ukichunguza kwa akili ya ufahamu uliopewa na muumba utagundua kuwa makanisa yapo kupingana na biblia wanayo ibeba kwapani kila siku
Nadhani sio yote
 
Back
Top Bottom