Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

Jamii ya watu weusi inaangamia kwa kupenda miujiza, maajabu na mazingaombwe badala ya kupenda kuwajibika kwa juhudi na maarifa

Viongozi wengi wa Makanisa wametumia Shida na misongo ya mawazo ya Waumini wao kama mtaji wa biashara zao.

Kuna Kanisa niliiacha kuabudu baada ya kuombwa Nipeleke SalarySlip yangu ili wanipangia Sadaka ya Fungu la 10, yaani Kodi ya Serikali nilipe na Wale wahuni wapige hela zangu kama tunasaidiana kuzitafuta.

Nimeamua zile asilimia 10 walizokuwa wanazitaka kwa nguvu nawasaidia wenye Uhitaji na Masikini wenzangu huku mtaani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hadi wewee???? Uwiiiih
 
Hivi unafikiri wanaosema waafrika ni wajinga unadhani ni utani.Vichwa vyetu sio vizima kabisa.Ujinga tunaoufanya uku afrika ni mkubwa zaidi kuliko unaofanyika uko walikotuletea hizi dini.Kwa mfano angalia hili jambo la mapenzi ya jinsia moja,nakuhakikishia japokua kwasasa linaonekana ni jambo dogo na liko chini chini ila kwa vichwa vyetu baada ya miaka 10 litakua kubwa sana uku kwetu kuliko uko liliko toka.Dini zilianza hivi hivi polepole ila sasa hivi kuna wanaojifanya niwadogo zake na yesu kabisa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] haswaaaah
 
Unakuta libaba jitu zima linalia jiiiiiiiiiiim.... jiiiiiiiiii jijiiiiiiiiiiiiii mhhhhhhh anabadilisha magia utadhani anaendesha Scania 113 akiamini eti ndio atapata semi trucks
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimechekaa kwa sautii, hadi watu wananishangaaaa, khaaah.

Afu ukute kuna baba kati ya hao ana kitambi pia, mbavu zangu mie uwiiiii.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hadi mbaba mwenye kitambi na mindevu yake nae anaendesha gari hewa[emoji23]
Hebu imagine ndo anakanyaga gia, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], nacheka km mwehu hapa.
 
Longtime niliepelekagwa kwa mama rwakatare,kipengele hicho cha kutaka gari sasa ,mnakaa mkao wa kushika usukukani na kukanyaga break
Huku mnaombewa [emoji1]

Ova
Hadi wee?? Ujanja wotee huu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapana sitakiii kuamini,
Mweeeeh
 
Longtime niliepelekagwa kwa mama rwakatare,kipengele hicho cha kutaka gari sasa ,mnakaa mkao wa kushika usukukani na kukanyaga break
Huku mnaombewa [emoji1]

Ova
Dah...
Huwi tajiri kamwe kama hamna watu uliowafanya misukule. Misukule ya dini mpo?
 
Ukishaamini Mungu tu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, umeshaamini muujiza.

Na unakuwa ushaingia katika matatizo uliyoyataja.
Karibu utoe neno Mr, hujawahi niangushaa hata.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hebu imagine ndo anakanyaga gia, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], nacheka km mwehu hapa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah [emoji23][emoji23]yaani nimewavutia picha nikajikuta nacheka mbaya kabisa. Mara mmama na mimba yake, mbaba na likitambi wanapichana kama robot.

Hawa wahubiri Mungu anawaona[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi ni Mkristo nisiyeamini katika makanisa na miujiza, maajabu na mazingaombwe.

Ila jana nilienda kusali kwenye kanisa moja nikiwa nimeambatana na rafiki yangu na baba mzazi wa rafiki yangu, huyu mzee anasema kila siku anawaona nduguze waliokufa siku nyingi wanamwita. Na nyakati nyingine amekuwa akiwaona hao wafu wanamuandalia party ya kula nyama mbichi za watu.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu hili kanisa waliambiwa na kiongozi wao kila mtu aendeshe gari lake, atoe mlio wa gari, aweke gia na kupiga honi za mdogo. Elekea kulia, kushoto, mbele, nyuma, kisha nenda nje ya kanisa ukapaki gari yako.

Wakati watu wakiwa busy na ujinga ule, mimi nilikuwa nimekaa kimya nawacheka tu kimoyomoyo.

Mchungaji naye alikuwa busy akizunguka huku na huko akiwagusa watu wake vichwani na kuwaambia gari lako na likadhihirike kwenye ulimwengu wa nyama.

Akiwa kwenye kuzunguka kwake ndipo akanikuta nimekaa sifanyi utaahira ule. Akaniuliza kwanini naleta roho za upinzani kanisani kwake?

Nikamjibu sileti roho ya upinzani, ila siamini kwenye mazingaombwe. Ndipo akawaita walinzi wake, yeye anawaita protocol wanitoe ndani na nisirudi tena mle ndani.

Nikamsikia akiongea kutoka kwenye maspika kuwa shetani amejidhirisha kanisani ili kuzuia muujiza wa watu kupokea magari.

Basi akaambiwa waanze kukemea roho zote za upinzani ambazo zinasababisha wao wasipokee magari yao.

Jamaa zangu nilipotolewa nje nao wakatoka tukarudi nyumbani.

Ndugu zangu watanzania magari hayapatikani hivyo. Utalitolea sadaka na kulipandia sana mbeg u gari lako, hadi ukome.

Waza nje ya boksi, kuwa mbunifu kwenye shughuli zako, boresha huduma zako, jali muda, uwe na matumizi mazuri ya fedha. Nidhamu ya fedha ndiyo itakayokuletea mabadiliko ya tabia zako.
Upo sahihi kiongoz
 
Back
Top Bottom