JamiiAfrica (Tanzania), IMS (Denmark) na Splice Media (Singapore) waja na “The Good Commons”

JamiiAfrica (Tanzania), IMS (Denmark) na Splice Media (Singapore) waja na “The Good Commons”

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Good Commons imejitolea kukusanya euro milioni 1.5 kusaidia jamii mbalimbali duniani ambazo zinaunda upya namna teknolojia inavyohudumia umma. Tofauti na kampuni kubwa za teknolojia na mifumo mikubwa ya akili bandia (AI) inayojengwa kwa misingi ya ufuatiliaji wa watumiaji na faida, jamii hizi zinaunda majukwaa salama na ya ushirikishwaji, yenye misingi ya maadili ya uandishi wa habari, uaminifu wa umma na ushirikiano wa kiraia.

“Majukwaa mbadala yanapaswa kulelewa, kuigwa na kupanuliwa huku yakibaki yakiwa karibu na jamii yanazozihudumia. Ndiyo sababu tumeanzisha Good Commons,” alisema Rishad Patel, mwanzilishi mwenza wa Splice, kampuni ya vyombo vya habari yenye makao yake Singapore na mojawapo ya taasisi waanzilishi wa Good Commons.

Ahadi ya kukusanya fedha hizo ilitolewa wakati wa Mkutano wa Copenhagen kuhusu Uadilifu wa Taarifa, ulioratibiwa kwa pamoja na IMS (International Media Support), Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, na Digital Democracy Initiative (DDI). Mkutano huo uliitishwa wakati Denmark ikiwa Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya.

“Hapa Tanzania tuliamua kutochukua njia ya Big Tech ya ‘suluhisho moja kwa dunia nzima.’ Tulijenga na kukuza JamiiForums, jukwaa la ndani linalosaidia watu kufanya maamuzi sahihi. Sasa tunataka kusaidia jamii nyingine kufanya vivyo hivyo,” alisema Maxence Melo, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, taasisi nyingine mwanzilishi wa Good Commons na inayoendesha JamiiForums – moja ya tovuti maarufu zaidi nchini Tanzania.
============
Good Commons commits to raise EUR 1.5 million to support communities around the world that are redefining how technology serves the public. In contrast to Big Tech and Big AI models built on user surveillance and profit, these communities are creating safe, participatory digital spaces rooted in journalistic values, public trust and civic collaboration.

“Alternative platforms must be nurtured, replicated and scaled while remaining anchored in the communities they serve. That is why we built Good Commons”, said Rishad Patel, co-founder of Splice, a Singapore-based media start-up and one of the founding organisations behind Good Commons.

The pledge to raise funds was made during the Copenhagen Conference on Information Integrity. Co-organised by IMS (International Media Support), the Ministry of Foreign Affairs of Denmark and the Digital Democracy Initiative (DDI), the conference was convened as Denmark holds the presidency of the Council of the European Union.

“In Tanzania we decided not to go Big Tech’s way of ‘one solution fits the world.’ We built and scaled JamiiForums, a local platform that helps people make informed decisions. Now we want to help other communities do the same,” said Maxence Melo founder and executive directe from JamiiAfrica, another founding member of Good Commons and the organisation running JamiiForums – one of Tanzania’s most popular websites.

On Thursday in Copenhagen, Good Commons is bringing together alternative platforms from Colombia, Denmark, India, Moldova, Tanzania and the United Kingdom to learn and grow more resilient together under the headline Common Ground.

photo_2025-11-12_22-34-35.jpg
 
Back
Top Bottom