JamiiForums Exclusive: Kiranga and Fellow members English Debate

JamiiForums Exclusive: Kiranga and Fellow members English Debate

Mbona hayo masihara ya kitoto tu?
Broh,
Hii lugha imenibidi nikajiandikishe pale British Council niwezwe pikwa upya.

Mana si kwa kigugumizi ninapokutana na wakenya. Hata hivyo ninampango wa kusoma MBA. Sasa ukiacha tu masharti yao ya kufikisha Marks ya 6.5 IELTS, pia kuna kimbembe cha kuandika pepa na presentations.

Ngoja nikajinoe.

Lkn Je, ni wapi hasa napaswa kuzingatia kwenye hii lugha?
Grammar na tenses?

Mana hata question tags zinanipasua kichwa!!

Hizi shule za jakaya bhana, una ufaulu mkubwa lkn lugha zero!
 
Mimi nimeanza kuhangaika na vitabu vya Charles Dickens tangu niko 13 years old, na kabla ya hapo nilikuwa na deal sana na comics nikitaka kufuatilia stories kwa picha na kamusi tangu niko 9 years old.

Kuanza mapema na kuwa na ufuatiliaji ni muhimu. Zingatia kuweza kuongea na kuandika kwa ufasaha, kuweza kusikiliza lahaja mbalimbali ni muhimu pia.

Hata kuangalia movies zenye subtitles au TV news tu ni kuzuri (shout outs to CTN, and DTV, bila kusahau TVZ "Mpainduzi Daima" kama Hegelian dialectics)

Kama kujifunza kitu chochote, muda utakaotumia na mbinu za kujifunza ni vitu muhimu sana.

Mimi nilikuwa najisikia vibaya sana kuona vitabu vya baba yangu vimejaza maktaba ya nyumbani, halafu mimi sijui kilichoandikwa, nikaifanya hiyo kuwa changamoto tangu niko mdogo. Kuna kipindi ilinibidi nisome hivyo vitabu huku natumia kamusi ya Kiingereza/Kiswahili ili kujenga msamiati.
 
Back
Top Bottom