JamiiForums imenisaidia nimepata kazi

JamiiForums imenisaidia nimepata kazi

nkwezi

Member
Joined
May 8, 2007
Posts
57
Reaction score
19
Alhamdullah, wana JF na mie nimepata kazi kwa kupitia matangazo ya humu.

Nawashauri sie tusie na marefa ukiona tangazo we tuma na umuombe Mungu tu, maana mie huu ni mwaka wa nne tangu nimalize chuo. Tusijikatie tamaa, tujaribu kufanya kazi hata za kujitolea kuongeza experience. Mungu awatilie wepesi wote wanaoendelea kutafuta kazi.

Mungu ibariki JF yetu isonge mbele.
 
Pamoja na shukrani nakuomba uchangie kiduchu kwa uongozi wa JF ili mtandao huu uzidi kuwepo kwa siku zote zijazo.
OTIS
 
Hongera zako mkuu,mi nina miaka 2 nautafuta wa 3!but kaz za bila malipo imekua ngumu kwangu, nimeomba sehem mbalimbali bila mafanikio,labda mnisadie ni makampuni ama taasisi gani zinapokea watu wa design yangu,nina postgraduate ya uhasibu.Pls help!
 
Hongera sana Nkwezi.....ni wachache sana wanaorudi kutoa shukrani zao.....
kila la kheri.....
 
Be blessed, but kupata kazi ni kazi hasa usipokuwa na kazi, but also go back kwa muumba wako pia umshukuru.
 
safi sana mkuu! tunashukuru kwa shukrani!
 
Hongera zako mkuu,mi nina miaka 2 nautafuta wa 3!but kaz za bila malipo imekua ngumu kwangu, nimeomba sehem mbalimbali bila mafanikio,labda mnisadie ni makampuni ama taasisi gani zinapokea watu wa design yangu,nina postgraduate ya uhasibu.Pls help!

Kwa Elimu uliyokuwa nayo Nakushauri uende JWTZ,japokuwa sifahamu utalipwa Kiasi gani. Ila ukiwa na DEGREE unaanza na Nyota 2. Wenye PGD sijajua waanzia vipi. Ni Ushaur wangu tu Mkuu
 
Wengi tu wanapata kazi bila marefa! Hongera sana. Kumbuka chezea mshahara usichezee kazi.
Kila la kheri, usibweteke.

Haya mambo ya marefa na kutojiamini yanatugharimu sana...tunakosa creativity au moyo wa kuthubutu kufanya hata yale yanayowezekana.
 
Kwa Elimu uliyokuwa nayo Nakushauri uende JWTZ,japokuwa sifahamu utalipwa Kiasi gani. Ila ukiwa na DEGREE unaanza na Nyota 2. Wenye PGD sijajua waanzia vipi. Ni Ushaur wangu tu Mkuu

Yah ni kwel mkuu hilo niwazo linalo nizunguka,nasikilizia nafasi zikitoka nijitupe huko.Shukran mkuu!
 
du hongera sana umetupa moyo sana kwa mim binafsi nilishaanza kukata tamaa kwa kweli pia n vema umerud kushukuru utabarikiwa zaidi
 
Mwanangu, nakupongeza kwa kukumbuka kutoa shukrani.

WASWAHILI WANAKWAMBIA MTU ASIYEKUWA NA SHUKURANI NI SAWA SAWA NA MNYAMA.

Hata mimi nawashukuru JF wamenisaidia kupata mtu aliyechukuwa duka langu nilikuwa natafuta mpangaji NAMI NIMEPATA.

GOD BLESS Jamii Forums na wanachama ambao kwa kweli wako sharp unapoweka jambo lako wana reply haraka....
 
Hongera sana kamanda! bt u didn't tell us where are you working,nevertheless,keep on encouraging those who are not yet employed.
 
Hongera sana kwa kupata kazi. Pia ni changamoto kwa wanaotafuta kazi usikate tamaa eti kwa sababu huna refa, jaribu kadri uwezavyo ndugu yangu....
Hongera Jamii Forums
 
Back
Top Bottom