JamiiForums inastahili tuzo, imetusaidia wengi

Alikuwa naibu meya wa Arusha kupitia ccm baadae aliachana na ccm na kujiunga chadema na sasa ni m/kiti mkoa wa Geita CHADEMA
Asante kwa maelezo yako mdau. Hapo nimemsoma mtoa mada.

Tukija kwenye dhumuni kuu la mada, hakika JF imenisaidia hata mimi pia. Hapa unapata 'ilim' adimu sana kutoka kwa wadau tofauti, burudani na taarifa muhimu.
 
Daima tunakukumbuka
 
Nikikumbuka zioe clips zake dakika za mwisho[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] walimwegu wabaya sana.
 
"Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi"

Aisee, hizi haya mbili zimenigusa sana, hasa unapofikiria kwamba aliyeziandika ametangulia mbele za haki ukizingatia na aina ya kifo chake. Roho yako iendelee kupumzika kwa amani kaka Mawazo.
 
Nimeguswa sana na bandiko hili!.
Kumbe Kamanda Alphonse Mawazo aliaga kabisa!.
Mimi ni muumini wa karma, walio waza kunuondoa, waliisema kumuondoa, waliopanga Kumuondoa, na waliotekeleza kumuondoa, wote watalipwa sawa sawa na uovu wao!.
RIP Shujaa Mpiganaji Shupavu Kamanda Alphonse Mawazo.
P
 
R. I.P kamanda mawazo, maneno magumu saana haya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…