JamiiForums inastahili tuzo, imetusaidia wengi

Namshukuru Mungu kwa kuniunganisha na familia hii kubwa, nawashukuru sana wanafamilia wa mtandao huu na zaidi sana waasisi wake.

Hivi majuzi nimepokea zawadi kutoka Marekani kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA(BAWACHA) na Mbunge wa viti maalumu Suzanne Lyimo.

Alipokuwa kule alikutana na watu waliomuuliza kama ananifahamu, walimpa dola kadhaa, wakaahidi kunisaidia zaidi siku za usoni. Zaidi sana wamenitumia video camera ambayo nitaipokea kesho kutwa. Walinifahamu kupitia JamiiForums.

Kule Norway kuna kijana wa kitanzania ambaye amekuwa akifuatilia tunachofanya huku, mwaka jana alijitolea kulipa ada ya dogo (mwanangu) mpaka amalize darasa la saba, kwa mwaka ni sh.1.7 million.

Zaidi sana kaandika kijitabu kinachohusu harakati zangu chenye title "HARAKATI NA MAWAZO YA KAMANDA MAWAZO".

Kijitabu hiki kinasisimua sana,hata kama ningekiandika mwenyewe nisingekiandika kwa umaridadi mkubwa kiasi hicho.

Nakushukuru sana Andrew.

Ninapotazama nilikotoka na mbio hizi za kisiasa kuna ka umbali kakubwa. Nimejikwaa mara kadhaa, nimewakanyaga wasafiri wenzangu kwa bahati mbaya, kuna wakati flani nilidondoka, ni nyie hao hao marafiki zangu mlioniambia niinuke, nijifute vumbi na nisonge mbele.

Kuna wakati tunatofautiana kimtazamo wa namna ya kuijenga nchi yetu, Tunachachafyana, hitilafiana, zogoana na wakati mwingine lugha zetu zinakuwa Kali kiasi, nawaambieni ukweli vitu vyote hivyo ndo vinatukomaza, vinatukuza na ndiyo maana halisi ya family.

Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi.

Asanteni marafiki, asante JamiiForums.

Jioni njema
Damnnn..!!!
RIP
 
"Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi".

IRP KAMANDA.
 
Nilitaka niandike Kama wewe, lakin hii shukrani yako imeniwakilisha saana.

JF imenifanye kulipenda taifa langu kuliko chama.

Nimelelewa katika familia ya CCM na mzee wangu alikuwa amenijengea mentality ya kuchagua viongozi kimazoea.

Sasa wana JF wamenijenga Sana na Nina sema nimekuwa nikiwajenga watu wengi wa mtaani about our nation...

JF ni familia kubwa na ukiitumia vzr ni zaidi ya leadership college.

Thanks JF.
Hii ndiyo ilikuwa JF kweli kuacha hii ya majinga akina Lucas Mwashambwa
 
Mungu azidi kuipumzisha Roho yako mahali pema peponi Kamanda
Namshukuru Mungu kwa kuniunganisha na familia hii kubwa, nawashukuru sana wanafamilia wa mtandao huu na zaidi sana waasisi wake.

Hivi majuzi nimepokea zawadi kutoka Marekani kupitia kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA(BAWACHA) na Mbunge wa viti maalumu Suzanne Lyimo.

Alipokuwa kule alikutana na watu waliomuuliza kama ananifahamu, walimpa dola kadhaa, wakaahidi kunisaidia zaidi siku za usoni. Zaidi sana wamenitumia video camera ambayo nitaipokea kesho kutwa. Walinifahamu kupitia JamiiForums.

Kule Norway kuna kijana wa kitanzania ambaye amekuwa akifuatilia tunachofanya huku, mwaka jana alijitolea kulipa ada ya dogo (mwanangu) mpaka amalize darasa la saba, kwa mwaka ni sh.1.7 million.

Zaidi sana kaandika kijitabu kinachohusu harakati zangu chenye title "HARAKATI NA MAWAZO YA KAMANDA MAWAZO".

Kijitabu hiki kinasisimua sana,hata kama ningekiandika mwenyewe nisingekiandika kwa umaridadi mkubwa kiasi hicho.

Nakushukuru sana Andrew.

Ninapotazama nilikotoka na mbio hizi za kisiasa kuna ka umbali kakubwa. Nimejikwaa mara kadhaa, nimewakanyaga wasafiri wenzangu kwa bahati mbaya, kuna wakati flani nilidondoka, ni nyie hao hao marafiki zangu mlioniambia niinuke, nijifute vumbi na nisonge mbele.

Kuna wakati tunatofautiana kimtazamo wa namna ya kuijenga nchi yetu, Tunachachafyana, hitilafiana, zogoana na wakati mwingine lugha zetu zinakuwa Kali kiasi, nawaambieni ukweli vitu vyote hivyo ndo vinatukomaza, vinatukuza na ndiyo maana halisi ya family.

Kwa vile hatujui siku wala saa ya kutoka duniani hapa, leo Shehe mkuu katutangulia mbele ya haki, hatujui kesho ni zamu ya nani! Tusameheane.

Lengo letu kuu liwe moja, kuiona au kuiacha nchi yetu ikiwa sehemu salama ya kuishi, tuache misingi imara kwa wanetu, wabishane lakini wasipigane au kuuana, watofautiane lakini wasiigawe nchi.

Asanteni marafiki, asante JamiiForums.

Jioni njema
 
Najuta kutokumfahamu mapema kamanda Mawazo nimekuja kusikia story zake baada ya kuzikwa kama mwaka hivi asee.
 
Back
Top Bottom