Jamiiforums kuna matajiri tupu

Jamiiforums kuna matajiri tupu

Kwanza napenda kuwashukuru ndugu zangu kwa maoni yenu juu ya hili swala. nadhani tatizo letu kubwa hasa nchi maskini ni kuchanganya maswala haya mawili:- Siasa na Uchumi.
Hata kama wenzetu nchi zilizoendelea wao huchanganya basi utakuta siasa huingizwa tu pale panapoonekana kuna faida kwao ya kiuchumi. Uchumi ndio sura ya nchi, uchumi ndio kiwiliwiwli na na roho ya nchi kwa hiyo maamuzi yote ya siasa lazima yawe ktk kuijenga afya ya taifa na sio kinyume..
Ni kosa kubwa kuwa walafi yaani hatuchagui kinachoingia mwilini mwetu na pia ni kosa kubwa kutokula chakula bora (chenye nutrition) kwa sababu ya imani inayotokana na dhana.
Poloz,
Nakubaliana na wewe, binafsi swala la ajira lina uzito mkubwa sana kwa nchi yetu. na kulingana na mfano mdogo wa mwili hapo juu, sidhani kama kati yetu kuna mmoja wetu anayeweza kuwepo hapa na kuyazungumzia haya kama hana kazi! Ni matokeo ya hizo ajira tumeweza kuchagua nini tunachotaka kula ama kuujenga mwili wetu kwa chakula cha aina gani?.... chaguo la chakula halikutangulia kabisa mfuko wetu..yaani mapato yetu.
Kuna mbinu nyingi sana ambazo nashindwa kuelewa kwa nini viongozi (siasa) na wataalam (wachumi) wetu wameshindwa kabisa kuyatatua maswala haya kulingana na mazingira yetu. Sidhani kama elimu yao imeishia ktk kapu la taka na sasa kinachotumika ni ulafi na ubinafsi.
hata hivyo nitazidi kuchangia zaidi mada hii kila tunavyozidi kusonga mbele maanake mwanga wa mwenge wetu wa uhuru bado upo isipokuwa tunaupuuza na kutumia artificial theories ktk pango hili lenye kiza - Utandawazi.

Hahahaaa na hiyo ndo manake
 
Jembe afrika...! Mawazo mgando hayo kwenda nje kudrive na kuishi kwenye nyumba yako ni haki ya kila mtz claim it!!!
 
"Haki ya nane",ukiwa na roho ya kuku huingii tena JF!Full mikogo,na mbwembwe to the fullest...nyeee...!
 
Kwakweli huwa nacheka sana maana thread za huku ndani inaonekana kila mtu mambo safi, anadrive, ananyumba, ofisi safi, anaenda nje mara kwa mara, je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe, maana ukitafakari ni zaidi ya uswiss na marekani.

kwahio kwako wewe ANAEDRIVE,ANA NYUMBA,ANAFANYAKAZI OFISINI NA ANENDA NJE MARA KWA MARA NI TAJIRI??!
 
Ni vizuri pia tuwaige ambao wameshafanikiwa. Wengi wamo humu humu jf.
 
kwahio kwako wewe ANAEDRIVE,ANA NYUMBA,ANAFANYAKAZI OFISINI NA ANENDA NJE MARA KWA MARA NI TAJIRI??!

Uswahilini sio kudrive tu...bali ukimudu kuvaa vizuri na kunukia basi unawekwa kwenye kundi la matajiri....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Umesema kweli hapa nilipo nipo uturuki nageuza bongo kuna deal la milioni mia tano namalizia.nikifika bongo tukutane kwangu masaki kwenye ile range yangu nyeusi.

Mkuu hapa umenichanganya kidogo; kwamba "unaishi masaki kwenye range nyeusi"?
 
Kwakweli huwa nacheka sana maana thread za huku ndani inaonekana kila mtu mambo safi, anadrive, ananyumba, ofisi safi, anaenda nje mara kwa mara, je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe, maana ukitafakari ni zaidi ya uswiss na marekani.

mkuu sio kweli mbona hata sisi wakushi tumo humuu....tukisha maliza kutengeneza cutural pale mitaa ya kati.tuna barizi humu
 
Kwakweli huwa nacheka sana maana thread za huku ndani inaonekana kila mtu mambo safi, anadrive, ananyumba, ofisi safi, anaenda nje mara kwa mara, je sisi tuliopanga na tuna baiskeli tu

Tuendelee kulogging in au tusepe, maana ukitafakari ni zaidi ya uswiss na marekani.

Umeongea aisee! Nyingi sana hizi "wakati natoka japani....",nikiwa ofisini kwangu..." " gari yangu break zikafail.."" mabizness partier wangu kutoka UK..."nikachukua loan ya sh mil 700 ofisini". Yaaani ni hatari! Ukiwaza sana unaweza ukaogopa kuchangia post humu!
 
babagodi mbona mimi sio tajiri lakini juzi juzi tu nimetoka london na nilivyofika nyumbani bmw yangu gia zikagoma kuingia na sasa hivi inabidi nisubiri business partner wangu kule UK atume audi maanake nishachoka na hii bmw.....ha ha ha ha ha
 
Last edited by a moderator:

Hahahahahaha! Hivi tafsiri ya tajiri ni ipi mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom