JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
JamiiForums kwa kushirikiana na StarTV itaendesha Mjadala kuhusu Nafasi ya Wanasheria Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024
Mjadala utaongozwa na Mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba) akiwa na Wadau wa Masuala ya Sheria wakiwemo Onesmo Olengurumwa (Mratibu THRDC), Jebra Kambole, Amne S. Kagasheki, Leonard Manyama, Dickson Matata na John Mallya
Soma Pia: Mjadala JamiiForums & Star TV: Nafasi ya Vyombo vya Habari kuelekea Uchaguzi wa Seriali za Mtaa
Fuatilia Mjadala huu Mubashara kupitia StarTV kuanzia Saa 3 Usiku leo Novemba 23, 2024.
Odemba: Unahisi kiini kikuu cha watu kukatwa na kuenguliwa ni nini
Jebra Kambole: Ni Mfumo wa Uchaguzi ambao kwa Mfumo wake jinsi ulivyo unafanya Wasimamizi wa Uchaguzi wapendelee chama kimoja kwa mfumo jinsi ulivyo kwa sababu hawa Wasimamizi jinsi Walivyo, namna walivyopatina na utendaji wao unategemea mtu aliyepo madarakani.
Mkurugenzi anayesimamia Uchaguzi au huyu DAS anayesimamia Rufaa hatua ya mwisho kabisa yupo pale sababu ya chama tawala ambacho ndicho kimekuweka madarakani. Uchaguzi uipita asiposhinda yule mtu wake harudi tena kwenye nafasi ile mwakani. Kwahiyo, obvious utasaidia yule mtu wako unayemtaka apite lakini mimi sioamini kwamba Wagombea wa CCM ndiyo wataalamu zaidi kujaza fomu kuliko Wagombea wa vyama vingine. Mimi naamini kwamba tunahitaji Uchaguzi ambao utakuwa huru na haki ambao mtu atapiga kura ataenda kulala lakini sio mtu apige kura na hana usalama wa hakika ya kura yake.
John Mallya: Kosa kubwa ambalo lipo wala halipo katika vyama vya Siasa vya Upinzani, kosa kubwa lipo kwenye aina ya Uchaguzi tunaotaka kuufanya na sheriailivyotengenezwa, leo tunazungumza kwa mfano leo tunazungumza jambo la Wagombea kukatwa majina yao.
Mimi nitazungumza wakati wa Kampeni kanuni ambazo zimetungwa Jebra kazitaja kwa namba hapa hazisemi kwa mfano mtu anapoingilia ratiba ya mwingine anapewa adhabu gani ya kiuchaguzi, kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mujibu wa Sheria zetu uizidisha muda, ukiingia ratiba ya mwingine kuna penalties za kiuchaguzi ambazo unazipata kwa mfano unaweza kufungiwa kampeni siku moja au siku mbili.
Jana umeona kilichotokea kule Songwe, kama CHADEMA wanadaiwa kuingilia ratiba ya watu wengine walipaswa wapewe adhabu ya kiuchaguzi sio Polisi wanakuja, wanawakamata, wanaharibu utaratibu wote wa Uchaguzi, unaweza kuona kanuni zimetengenezwa kuwanufaisha wale waliopo madarkani hiyo imeanza tangu kuanza kwa mchakato wa uundaji wa sheria yenyewe na kanuni.
Nini kifanyike? Kwa maoni yangu mambo haya yawe rectified mathalani kama Mgombea kakosea kujaza fomu adhabu yake siwe kumkata mtu, mwambie umekosea umeandika Chadema andika Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili wananchi wapate uwanda wa kuchaguzi watu wanaowataka badala ya kulazimishwa kumchagua mtu mmoja. Tuwe na sheria ambayo inaentertain Demokrasia na uchaguzi, uchaguzi sio kuwaambia watu wamchague mtu fulani bali ni kuchagua kwamba unataka A au unataka B.
Leonard Manyama: Mpaka hapa tulipo mambo yote yanaenda kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa kanuni tulizo nazo za nchi zinazosimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kila Kitu kinaenda kwa mujibu wa sheria, Ratiba, taratibu na muongozo iliyotolewa.
Odemba: Jukumu lako kubwa kama Mwanasheria, jukumu lako kama Wakili katika Uchaguzi huu tunaoenda ni lipi? Je unatambua nafasi yako katika Jamii hasa kwa wakati huu wa Uchaguzi?
Jebra Kambole: Kabla sijasema Jukumu langu niseme kitu kimoja Wanasheria wa Nchi hii tumegawanyika katika makundi matatu:
- Kuna Wanasheria ambao wapo Serikalini
- Kuna Wanasehria wa Kujitegemea
- Kuna Wanasheria ambao wamekaa kwenye vyombo vya maamuzi
Wanasheria ambao wapo mahakamani wana Wajibu wao, Waliopo serikalini wana wajibu wao na sisi tulio private tuna wajibu wetu. Wajibu wetu Mkubwa kama Wanasheria wa kujitegemea kushiriki katika michakao ya kiuchaguzi kwanza kabisa kwa kuisaidia jamii na kuipa elimu kwa sababu sisi Mawakili ndiyo Mainjinia wa mfumo wa Sheria za nchi hii.
Wanasheria ambao bado wapo mitaani wanao wajibu wa kuoba nafasi wasiwaachie tu Walimu, tukikosa basi tuwe Mawakala au Wasimamizi huru