JamiiForums Usiku wa manane

Hapo kwenye storyteller imenifanya nikumbuke kuna uzi mmoja ulikuwa unasema mtu ana andika story kisha mtu mwingine anakuja kuendelea sijui unaukumbuka?, mule wewe ma madame B mliua ilikuwa kama mnandika story moja
 
🌱 Umuhimu wa Kuwa na Mipaka Kwenye Maisha
Kuwa na mipaka kwenye maisha si kujiona bora kuliko wengine, bali ni kujua thamani yako na kujua ni mambo gani unaruhusu yaingie kwenye maisha yako na yapi huyaruhusu.
Mipaka inakusaidia:
Kujiheshimu
Unapoweka mipaka, unawaonyesha wengine namna unavyotaka kutendewa.
Kuepuka kutumiwa
Si kila mtu anayekuja na shida yake anapaswa kupewa nafasi ya kutumia muda, nguvu au mali zako bila kikomo.
Kulinda amani yako ya moyo 🕊️
Kuna watu na mazingira yanayokumaliza kihisia. Kujua wakati wa kusema “hapana” ni sehemu ya kujilinda.
Kujenga mahusiano yenye afya
Mahusiano mazuri hayahitaji mtu mmoja kuvumilia kila kitu. Kila upande unapaswa kuheshimu nafasi, muda, maamuzi na hisia za mwingine.
Kujua wakati wa kuondoka
Si kila jambo linahitaji kupiganiwa mpaka mwisho. Wakati mwingine hekima ni kutambua kwamba mahali fulani hapakufai tena na kuondoka kwa heshima.
Kuepuka kuishi kwa ajili ya kuwafurahisha watu
Ukijaribu kumfurahisha kila mtu, mwisho wake unaweza kujikuta umempoteza mtu muhimu zaidi: wewe mwenyewe.
Kumbuka:
Kusema “hapana” si ukatili. Kuweka mipaka si kiburi. Na kuondoka mahali ambapo huthaminiwi si kushindwa.
Maisha yanakuwa mepesi unapojifunza kwamba si kila mtu anastahili access sawa kwenye muda wako, moyo wako, nguvu zako na maisha yako.
“Heshimu watu, wapende watu, wasaidie watu, lakini usisahau kuweka mipaka. Moyo wako nao unahitaji ulinzi.” 🌿
 
🤣🤣🤣 Sio kweli blaza tunajificha tu katika hicho kichaka...! Wanaoelewa pattern wananisumbua tu.🤣
Iko hivi,yani lazima utakuwa na vijielement kidogo vya swaga zako

Binafsi sio ucheshi wa humu,kiasili ni mcheshi na mtu happy,yani ukisikia kagombana na mimi utashangaa

Kwahiyo my point is,huwa hatutofautiana n vile tulivyo,yani lazima kuna kielement flan hv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…