Wafahamu watu wenye Vibration kubwa
Watu wenye msisimko mkubwa ni watu ambao huwa wana element fulani ambazo huashiria kwamba wana vibration kubwa
Watu ambao wapo happy muda wote,hawa huwezi kuwa kuta wakinuna nuna bila sababu,yani ni watu wenye kukunjua nafsi zao
Watu ambao wanapenda wengine wafanikiwe kwenye maisha,wanapenda kuona wengine nao pia wakifika sehemu fulani ambayo walau watakuwa wanajishikilia na maisha yapate kusonga mbele
Watu hawa hata ukiwaomba ushauri,huwa wanakupa ushauri wenye manufaa,watakwambia kile ambacho kitakuwa na maslahi na wewe hata kama kitakuudhi,kwasababu wamenyooka kama rula
Watu wenye kutoa msaada wa namna yoyote ile maadamu upo ndani ya uwezo wao
Kwa tabia zao ambazo ni murua huwafanya wapendwe na watu, watu wanajisikia amani wakiwa na watu hawa,hivyo huwafanya wawe watu ambao mara zote huzungukwa na watu
Mara nyingi huwa watu wenye amani,furaha na upendo kwasababu wamezungukwa na positive energy
Je,wewe ni mtu mwenye high vibration au low vibration?
Jikague na tengeneza mazingira ya kuwa kwenye kundi la watu wenye high vibration
Alamsik!