Oktoba 26, 2024 baadhi wa Watendaji wa JamiiForums walifanya Mjadala na Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Feza na kujadili mbinu za kulea watoto katika nyakati Dunia ya Utandawazi na Digitali.
Timu ya JF ikiongozw ana Mkurugenzi Mtendaji, Maxence Melo ilifanya majadiliano ya kina kwa takriban Saa 3 na kubadilishana mawazo na mbinu mbalimbali za jinsi ya kuwalinda watoto dhidi ya hatari zilizopo mtandaoni.
Mjadala huu ni sehemu ya jitihada endelevu za #JamiiForums za kushirikiana na jamii na Taasisi mbalimbali ili kuhakikisha Watoto wanakuwa salama mtandaoni.
Mafunzo mnapeleka feza tu jf kwenu mnakukacha??
Kama mlishawahi kuyatoa hapa wekeni link ama lah tuelezeni hicho mlichofundisha huko na sisi tufaidike na tufundishe wengine.
Mkuu Maxence Melo hayo mafunzo mnaweza mkayaweka na humu iii sisi Wazazi tunaosomesha watoto wetu Magomeni Mzimuni tuyasome na tukawafundishe watoto wetu ? 🤔