JamiiForums yapongezwa Bungeni kwenye Bajeti Kuu ya Serikali. Maxence Melo apongezwa kwa Uzalendo wa Ushauri Kodi Biashara ya Mtandao

CCM wameanza kuipenda JF tangu lini?

By the way hawa Kina Mello ndio wazalendo sio design kama yule kibaka wa Hai ndio waliitwa wazalendo awamu ya tano.
 
Mbona unawatag sana viongozi na ni wewe tu kwenye uzi huu ndio umetawala au unataka teuzi za kulamba asali ?
Niliendeleza tu pale alipoishia Mwandishi nguli Pasco. Na kuhusu uteuzi, hapana! Sina sifa.
 
Sasa vijana wawache matusi ya ovyo na kuita wenzao wanaowahoji 'wajinga, wapumbavu, zezeta.....'

Kisa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na majizi ya kura? Kimsingi hatuoni sifa yoyote ya hili jukwaa kusifiwa na watu wasio na uadilifu wowote.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mwigulu awe real? Kesi dhidi ya Maxence zilifunguliwa Waziri wa Mambo ya ndani akiwa Nani? Acha kumwamini Huyo Mnafiki, anaona Mello habadili msimamo na watu wanampenda anajifanya kumpongeza ili aungwe mkono JF.
Nadhani kama kuna 'post' yenye Akili katika huu Uzi wote ni hii yako Mkuu kwani umemaliza kila Kitu na tena tukupe 'Likes' hata 'Trillion' kabisa. Wenye Akili tumekuelewa vyema na Kukubaliana nawe 100% zote.
 
Kama wanaikubali kazi ya Maxence Melo wampe tuzo.
Wampe Tuzo Mtu ambaye Wanampenda na wanamchekea Kinafiki lakini Moyoni Wanamchukia hakuna Mfano kwakuwa Mtandao wake Unaibua mengi wasiyoyataka na Kuwaumbua pia?
 
Kisa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na majizi ya kura? Kimsingi hatuoni sifa yoyote ya hili jukwaa kusifiwa na watu wasio na uadilifu wowote.
Kwani mtu akithamini kazi uliyofanya ndiyo amekusifia? Haijalishi kama anakupenda au la lakini angalau amethamini ule muda uliotumia kuifanya ile kazi.

Kwa hivyo siyo lazima tuwe negative siku zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…