JF haifai kutoa mafunzo ya kuwa salama mtandaoni na kutoa habari sahihi kwani imekuwa kijiwe cha uzushi na kutukana wale wote wasiofikiri na kuunga mkono mwelekeo wanaoutaka wao huku uongozi wa JF wakifumbia macho.
Tunaweza kufikiri na kuwa na mielekeo tofauti bila ya matusi,kejeli na uzushi wa kuchafuana.
Uongozi wa JF hawafuati terms zao kwenye utumiaji wa hii Forum.
Matusi,uzushi na fikra zisizojenga ndio zimekuwa mada zinazoshabikiwa hasa kwenye Jukwaa la Siasa.Azma iwe kukosoa ili kujenga sio kukomoa.Tanzania ni Nchi yetu sote ukitoboa mtumbwi tunazama wote.
Ni wakati sasa iwe we dare to speak freely but truthfully