Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
jaman kwetu ROMBO,KILIMANJARO MSISAHAUUUUUUUUUUUUU JF!Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisha upatikanaji wa maendeleo.
Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.
Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.
Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.
Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Jimbo la Pili katika mradi huu limekuwa la Nzega, litafuatiwa na la Kigoma mjini na kisha Sengerema. Majimbo ya Mtama, Kigamboni na Arumeru Mashariki yatafuatia.
Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.
Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.
Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.
Malengo ya Tushirikishane
Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:
i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.
Matarajio ya Mradi
Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:
i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.
JamiiForums itakuwa inakuletea matukio yote kuhusiana na mradi huu kwa kadiri utekelezaji wake utakavyokuwa unaenda katika kila Jimbo.
Nukuu toka kwa Maxence akimjibu Kichuguu:
=========
KATIKA PICHA:
View attachment 378807
View attachment 378808
Hatua ya awali katika uzalishaji wazo.
View attachment 378824
View attachment 378828
Timu ya Jamii Media ilipoenda Dodoma kuwashirikisha wabunge juu ya wazo la mradi
View attachment 378715
Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.
View attachment 378708
Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja
View attachment 378709
Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.
View attachment 378713
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Ijuganyondo(CCM) na Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA).
View attachment 378716
Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.
View attachment 378719
Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.
View attachment 378711
Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
View attachment 378710
Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.
View attachment 378770
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau
View attachment 378714
Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.
=======
NZEGA:
View attachment 379502
View attachment 379503
View attachment 380030
Warsha ikiendelea katika Ukumbi wa Lake Tanganyika
View attachment 380032
Sheikh na Mchungaji nao walishiriki
View attachment 380035
Picha ya pamoja na washiriki toka Nzega. Waliokaa ni madiwani
Kuhusu mjadala na taarifa za kinachojiri katika majimbo husika tembelea
TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini
TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega
TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini
TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni
TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Mtama
Hili nalo neno wabuni kitu kuhusu member WA jf maana tupo Kama familia wengine wapo since jf inaanzaNi wap sisi watuiaji wa jamiii forum tuahusika moja kwa moja katika hili . ?
Au ni program ya JF nje ya JF Blog.
wazo zuri sana nimefikiri sana kuhusu hili...Bro. Max atusaidie hapa!Ni wap sisi watuiaji wa jamiii forum tuahusika moja kwa moja katika hili . ?
Au ni program ya JF nje ya JF Blog.
safi sana wazo zuri,Safi kabisaaaa! Mabadiliko siyo tunayoyaombea bali tunayojiletea!..