JAMVI la wanawake: Maono na ushauri wa wazazi

JAMVI la wanawake: Maono na ushauri wa wazazi

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Ushauri gani ulipewa na mzazi, iwe ni baba au mama, ukaufuata na umekusaidia kufika mpaka hapo ulipo?

Naanza:
“Atayekulisha ni mwema, ila utampa pia uwezo wa kukulaza njaa wakati wowote atakapoamua - jishughulishe na hakikisha hauwi tegemezi”. Ushauri kutoka kwa baba yangu (Mungu amrehemu), alikua anatupa huu ujumbe mara kwa mara. Zaidi ya hapo, niliona namna mzee alikua anasapoti shughuli za mama, kielimu wakati anajiendeleza na elimu ya juu na kwenye utafutaji wake wa ziada kibiashara. Wote walikua wafanyakazi waajiriwa, mzee alibeba majukumu mengi ya kifamilia, ila mama pia alikua na uhuru wake kiuchumi. Baba alipotangulia mbele za haki, mama alisimama na familia bila kuyumba.

Ushauri wa mzee, ulinisaidia sana kuwa na mentality ya kujitafutia changu na si kumtegemea mtu. Mambo mengi nimeyaepuka sababu ya hili.

Ladies, share upande wako tujifunze.
Gents, leo tunawakaribisha pia Jamvini.

CC:
nakwede97Aaliyyah
Leejay49 Ms Billionaire
Sister AbigailBantu Lady
realMamyQashy Lilith
Atoto
Niwaheri
Lamomy
To yeye
Msweet
Chujio
Demi
ledada
Midekoo
Carleen
ABJ magwamaka
Numbisa Mrs Byesige Kelsea
Lily Tony cocastic
Nuzulati rubii

Mama MwanaSweetyCandy
Ellerie Bexley
 
Nilivomaliza chuo Mzee akanitafutia biashara Tena biashara ambayo sikuwaza kama ningeweza kufanya ila nashukuru mungu imenifungua upeo wangu wa utaftaji kwamba sio lazma ni ajiriwe pia nisichague kazi Sasa nimeweza kujifanyia shughul zangu bila usimamizi Wala kusaidiwa na so called a man
 
Tunawashukuru sana wazee wetu kwa kutujenga kweli 🙏
 
Back
Top Bottom