Jana nilimwagiwa maji ya kuwasha na kulipuliwa mabomu ya machozi

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
3,732
Reaction score
6,561
habari za ushindi wa Tanzania dhidi ya Uganda sijazifurahia maana jana nimetoka huku bagamoyo hadi temeke ili nishangilie taifa stars lakini nikaambulia kulizwa na mabomu na kupigwa na maji yanayowasha bila sababu yoyote........

KWA KWELI INAUMA SANA KUUMIZWA VILE WAKATI MIMI NILIKUWA NATAFUTA JINSI YA KUONDOKA BAADA YA KUAMBIWA TIKETI ZIMEISHA, LAKINI KABLA SIJAFIKA MBALI NIKAKUTANA NA HIYO KADHIA.

Nawashauri POLICEwaangalie namna nzuri ya kudhibiti watu lakini siyo kunionea vile. Nimetoka mbali bagamoyo nakuja kupigwa na mabomu ya machozi.
 
Pole sana mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndo wanafanya kazi kwa weledi wa hali ya juuu! Walishapewa ruhusa
 
Ndio maana huwa siendi uwanja wa kibongo kuangalia mpira vurugu tupu
 
Watu wenye mapenzi na tukio kama la jana huwa wanalifanya kuwa special.
Wewe hukufanya hivo, ulitakiwa kufika mapema ukiwa tayari na tiket yako mfukoni unaingia uwanjani.
Sasa wewe ukurupuke huko af unakuja kulialia hapa kwanza mlivunja geti acheni ushabiki njaa.
Wenye mapenz ya ukweli na mpira wote waliingia ndani na walifurahi kweli.
Mashabiki njaa walivunja geti na waliishia kupigwa tear gas
 
Hiyo ndio ilikua stahiki yako na wenzio ambao hamkuonesha ustaarabu.
Mlitaka muingie kwa nguvu na ubabe wenu halafu muachwe tu.. ?? Acha hizo mdau
 
Kwamaisha hayo kwanini tusishike nafasi ya 153 kati ya 156 kwa watu wenye furaha duniani. Nadhani mwakani kwa juhudi za jiwe tunakuwa wa mwisho kabisa
 
Watu walikuwa na tiketi na bado walionja joto ya jiwe, inaonekana tiketi ziliuzwa nyingi kuliko uwezo wa uwanja. Sasa sijui zilikuwepo tiketi bandia ama vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…