Jana nimeona faida ya ukali kazini, hongereni Watumishi wakali kazini

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Kwanza kabisa pongezi kwa mkuu wa nchi kwa kuwa mkali.
Kabla ya Rais Magufuli discipline kazini ili 20% kwa sasa imepanda sana tunaweza kukadiria 80%. Ule ujinga wa "unanijua mimi ni nani"? Haupo tena.

Mada husika
Jana katika Ofisi za Manispaa ya Temeke niliona umuhimu wa Rais Magufuli na baadhi ya watumishi kuwafokea watendaji wa chini yao. Kumbe ukiangalia kwenye tv utaona kama wanaonewa ila kwa kweli Watanzania bila viboko hawafanyi.

Ofisi ilikuwa imejaa watu mbalimbali wanotaka kulipia leseni, ardhi n.k toka asubuhi mpaka saa 9 huduma zilikuwa slow sana kaz iliyotakiwa kufanywa na watu wa4 ilikuwa inafanywa na mmoja ukiuliza unaambiwa network inasumbua watu wakachoka wakaenda ofisi ya mkurugenzi mzee akaja aliwaka sana na wafanyakazi pale ndani ya dk 10 tu watu wote wakahudumiwa na kuondoka.

Swali likabaki je mkurugenzi alikuja na network?

Jibu wanalo wenyewe walikoromewa, KUMBE SIO KILA NETWORK INAYOSUMBUA NI KWELI, WAKATI MWINGINE NI KISINGIZIO TU CHA KUPOTEZA MUDA.
 
Tusimlaumu sana Magufuli. Waafrika bila viboko hatuwezi kusonga mbele.
Jana nimewaza sana asee hasa wakoloni walivyokuwa wanatuchapa. Mtu mweusi akila akishiba anawaza ujinga tu kaz basi
 
taasisi za serikali ndio wanaongoza kubeba mimba,sì ajabu kukuta staff wote wako likizo ya uzazi.

taasisi za serikali ndio wanaongoza kwa kwenda kula kula,kama wana minyoo.ni wahudhuriaji bora wa kipindi cha cha kula.mmepanga foleni haitembei mjinga anaaga anenda kula.

hii ya mtandao kusumbua ni sababu common sana.
 
Inakera sana foleni imejaa amebak m1 ufikiwe unaskia naenda kula...dah!
 
taasisi za serikali ndio wanaongoza kubeba mimba,sì ajabu kukuta staff wote wako likizo ya uzazi.

taasisi za serikali ndio wanaongoza kwa kwenda kula kula,kama wana minyoo.ni wahudhuriaji bora wa kipindi cha cha kula.mmepanga foleni haitembei mjinga anaaga anenda kula.

hii ya mtandao kusumbua ni sababu common sana.
Teh teh. Ofisi nzima wanabeba mimba. Si wana uhakika wa mishahara waache watinduane tu.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
taasisi za serikali ndio wanaongoza kubeba mimba,sì ajabu kukuta staff wote wako likizo ya uzazi.

taasisi za serikali ndio wanaongoza kwa kwenda kula kula,kama wana minyoo.ni wahudhuriaji bora wa kipindi cha cha kula.mmepanga foleni haitembei mjinga anaaga anenda kula.

hii ya mtandao kusumbua ni sababu common sana.
Mkuu agiza soda kwa mangi bill kwangu[emoji23],yaani sijui serikali ifanye kitu gani kuondoa huu ujinga.
 
Back
Top Bottom